Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,438
- 1,026
Toto lisilo lako utalijua tu.Linacheza mpira wa chandimu na wenzie,bahati mbaya wanakupiga na ule mpira,unauchukua na kuuficha,watoto wengine watakimbia,lenyewe litakuja kifua mbele kwa hasira huku likidai mpira kwa nguvu.Toto lisilo lako hata ukilipa adhabu,litalalamika sana huku likilia kwa uchungu kwamba umelionea tena litasema umeliadhibu bila hata kosa.Mtoto aliye wa damu yako hawezi kuwa jeuri kiasi hiki,ni lazima akuheshimu na kukuogopa pia.Kama una toto la namna hii ujue shemeji kakuchanganyia mayai ya jogoo jingine.