Utalijua tu!

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,025
Toto lisilo lako utalijua tu.Linacheza mpira wa chandimu na wenzie,bahati mbaya wanakupiga na ule mpira,unauchukua na kuuficha,watoto wengine watakimbia,lenyewe litakuja kifua mbele kwa hasira huku likidai mpira kwa nguvu.Toto lisilo lako hata ukilipa adhabu,litalalamika sana huku likilia kwa uchungu kwamba umelionea tena litasema umeliadhibu bila hata kosa.Mtoto aliye wa damu yako hawezi kuwa jeuri kiasi hiki,ni lazima akuheshimu na kukuogopa pia.Kama una toto la namna hii ujue shemeji kakuchanganyia mayai ya jogoo jingine.
 
Hapana hiki ni kiashiria tosha cha wewe kwenda kupima DNA.

sasa kuna mtoto unaweza mkuta kafanana na wewe kwa kila kitu isipokuwa hako katabia ka kulia lia kana kwamba ameonewa inakuwaje hapo?
 
:lol: hahahahahahahahahaha...................mkuu usijenge chuki na kushindwa kumlea vizuri mwanao aisee.............lakini kuna kaukweli flani ; kuna jmaa yangua kaowa mtu amabaye ana mtoto; huyo mtoto ni pasua kichwa ajabu
 
Ukweli upo kiasi,but let us kupotezea.
 
hacha kudanganya umma! km ana tabia za wajomba zake bt kafanana na baba!??
 
Hii nadharia ngoja niifanyie utafiti, wiki ijayo nakuja na uzi......................
 
Mhhh hi siyo njia sahihi ya kupima uhalisia wa mtoto wako. Fanya DNA test kama una wasi wasi. Ujeuri wa mtoto unachangiwa na mambo mengi sana na wala hauna uhusiano kabisa wa kama ni wako au laa. Na kwa taarifa yako mtoto asiye wako na huwa na mapenzi na ukaribu zaidi na wewe kuliko hata yule wa kwako orijino
 
Haya bana,utaja nambia one day!nijuavyo mimi mtoto asiye wako si kwamba atakupenda sana wewe ila wewe ndo utampenda kuliko hata yule wa damu yako halisia.
 
taratibu atakua na atabadilika kabisa na kuwa mtoto unaye muhitaji wewe, japo mwanzoni inaonekana mlimdekeza sana
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom