Utajiri wako na hali nzuri ya maisha unayojisifu nayo si lolote kama jamii inayokuhusu ni masikini na fukara

Morning_star

JF-Expert Member
Apr 21, 2018
4,167
11,490
Fikiria huko sehemu na jamaa zako mkila bata alafu jamaa fulani amnong'oneze mwenzake "unamuona huyo jamaa! kwao ni masikini wa kutupwa". Au umekaa sehemu za ushuani kama "masaki" ukiwa na marafiki na wewe unaishi mbagara japo umejenga mjengo wa maana mbagara (ghorofa) alafu wakati mnatambulishana mtu aseme jamaa yetu katoka mbagara ndiko anakoishi!

Huwe na uhakika pamoja na mwonekano na ghorofa lako watu watakuona masikini umedandia party za watu! Ulishawahi kujiuliza umeenda "Ulaya" japo kwenu ni maisha bora unakaa "Oysterbay" na baba yako ana hela ni mkurugenzi katika kampuni kubwa nchini mwako, mko mnakula bata na foreigners kutoka nchi mbalimbali duniani alafu mnaanza kutambulishana nchi mlizotoka alafu unatambulishwa umetoka Tanzania na wengi wana "google" kutaka kujua "Tanzania" na kukuta ni mojawapo ya nchi masikini duniani kutoka Africa?

Muda huo utaanza kunyanyapaliwa hata kama unajiona tajiri. Ulishawahi kujiuliza viongozi wa kiafrika wakienda ulaya wanavyowachulia? Kama hujui rejea msiba wa malikia wa Uingereza! Marais wa kiafrika walipakizwa wote kwenye basi! Rais kutoka mataifa tajiri kama USA, Canada, France, walipewa usafiri binafsi! Katika uwakilishi wa kimataifa, wakati nchi moja inakuwa na kura ya "veto" kama USA, Canada, France, UK, n.k.

Upande wa Africa yenye nchi zaidi ya 52 hatuna hata kura moja au kwa kutufikiria tunawakilishwa na mfumo fulani ambao hauna ushawishi wa kukubali au kukataa hakuwezi kubadili chochote! Sasa nije hapa nchini! Wako mashemeji zangu siku hizi ukiwakuta wamekaa wanavyousifia mkoa wao eti ni kama ulaya! Hivi hapa Tz kuna mji/mkoa wa kulinganisha na ulaya?

Bado nyie woote ni masikini na mafukara! kujikomboa kwenu ni mpaka hapo mikoa yote itakapokombolewa! Endelea kuiba na kudumaza uchumi wa mikoa mingine na nyie mtaendelea kuwa kapu lilelile la masikini na mafukara!
 
Back
Top Bottom