Utajiri wa Ridhwani wamweka pabaya Kikwete

Status
Not open for further replies.
Wapendwa tkt JF salam zenu wote/nyote/sote.
Nashukuru kupata nafasi hii kuwasiliana na ndugu zangu wanamijadala.
napenda kuwasilisha madda hii hapa, je, huyu mtt wa n je ni n? unadhani km kweli wanavyosema ameweza kuagiza magari 100 semi traillers unadhani nikwasababu ameweza kujijasiliamali mapema au unadhani kuna mkono mkubwa wa mafisi maji? je, unadhani EL anamzidi nani kwa ufisaid? je nikweli kuwa akipewa urais 2015 anaweza kutuacha nakutumia vibaya madaraka yk nakuendelezza mafisadi? je unadhani kweli wapo km akina Sumaye au Warioba wnaofaa kuwa marais?
napenda kusema kwani nilikwisha sema EL anatufaa sn.


Riziwani ni kijana muungwana, safi, muadilifu si kama wanasiasa wanavyotaka tuamini. Ni kichekesho viongozi wa kisiasa kutafuta umaarufu kupitia kwa kijana mdogo huyu. Mwanamume mwenye taarifa ya ukweli aipeleke PCCB, Polisi na aweke ushahidi wazi. Tuache kumchafua kijana kwa sababu tu mzazi wake ni Mkuu wa nchi. Tuhuma bila ushahidi ni udikteta wa hali ya juu.

Inasikitisha watanzania hatudai uthibitisho kutoka kwa wanaoropoka majukwaani bila ushahidi. Watanzania ni wepesi kutuhumu bila ushahidi. Hizi ni tuhuma kama za HOTELI LAKAIRO zilizotolewa wakati wa uchaguzi uliopita. Tulidanganywa kuwa alikuwa Mwanza wakati ilikuwa ni uongo mtupu. Viongozi waandamizi wanapotoa tuhuma nzito bila ushahidi ni hatari kwa demokrasia. Hivi kwa nini tuhuma nzito zinatolewa katika mikutano ya kisiasa badala ya kupelekwa katika vyombo vya sheria? Siku moja watanzania watagundua uongo unaopikwa katika majukwa ya kisiasa na wanasiasa.
 
Riziwani ni kijana muungwana, safi, muadilifu si kama wanasiasa wanavyotaka tuamini. Ni kichekesho viongozi wa kisiasa kutafuta umaarufu kupitia kwa kijana mdogo huyu. Mwanamume mwenye taarifa ya ukweli aipeleke PCCB, Polisi na aweke ushahidi wazi. Tuache kumchafua kijana kwa sababu tu mzazi wake ni Mkuu wa nchi. Tuhuma bila ushahidi ni udikteta wa hali ya juu.

Inasikitisha watanzania hatudai uthibitisho kutoka kwa wanaoropoka majukwaani bila ushahidi. Watanzania ni wepesi kutuhumu bila ushahidi. Hizi ni tuhuma kama za HOTELI LAKAIRO zilizotolewa wakati wa uchaguzi uliopita. Tulidanganywa kuwa alikuwa Mwanza wakati ilikuwa ni uongo mtupu. Viongozi waandamizi wanapotoa tuhuma nzito bila ushahidi ni hatari kwa demokrasia. Hivi kwa nini tuhuma nzito zinatolewa katika mikutano ya kisiasa badala ya kupelekwa katika vyombo vya sheria? Siku moja watanzania watagundua uongo unaopikwa katika majukwa ya kisiasa na wanasiasa.
Umesoma post ya Horseshoe Arch hapo juu?
 
Dear Chamkoroma,
Nafikiri wewe unajaribu uwezo wa wana JF kupambanua mambo.
1. RZ1 kwanza ni nani? ana nini cha kufanya na watanzania? yeye majukumu yake ni kwa familia yake tu, likiwemo lile la msingi la kumkapenia baba yake 2010. Suala la kuwa yeye ni fisadi, hata hapa tukisema halitusaidii kwa vile hakuna hatua zitazochukuliwa kwake na pia ushahidi upo wake. Ni mtoto but a billionnaire now, just imagine ni watanzania wangapi, maarufu, wasomi, waliofanya kazi sehemu kubwa hawajawahi kuwa mabilionea hadi leo? mtoto katoka shule juzi, leo ni bilionea, hata kama vya kurithi, badooooooo, it is too much
2. EL anajifahamu mwenyewe
3. Watanzania na wana JF tuna mambo mengi ya kujadili na sio maisha binafsi ya watu. Kuongelea uchaguzi 2015 wakati kilosa watu wanakufa na mafuriko itatusaidia nini sisi?
4. UMETUMWA kucheki STATUS ya RZ1 kwa wana JF
 
Utajiri wa Ridhiwani wamweka pabaya JK
• Adaiwa kuwa bilionea kwa mgongo wa Ikulu

Na Mwandishi wetu

RAIS Jakaya Kikwete anakabiliwa na kashfa nzito kutokana na utajiri wa mtoto wake, Ridhiwani. Sasa anatuhumiwa kuitumia Ikulu kumtajirisha mwanawe, ambaye anasemekana ni bilionea.

Kwa nyakati mbalimbali, ukwasi wa mtoto huyo wa rais uliibuliwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila.

Katika moja ya mikutano yake ya hadhara hivi karibuni mkoani Tabora, Dk. Slaa alisema Ridhiwani amemaliza shule miaka michache iliyopita, lakini hivi sasa ni tajiri bilionea na kwamba ameupata utajiri huo katika mazingira ya kutatanisha.

Jana Mtikila alizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Travertine, akidai Ridhiwani amegeuka bilionea kwa muda mfupi “kwa mgongo wa baba yake.”

Akibainisha zaidi uwezo wa kifedha wa kijana huyo, Mtikila alisema hivi karibuni mtoto huyo ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM), aliingiza magari makubwa ya mizigo aina ya “semi trailer” zaidi ya 100 na kudai kuwa yanafanya kazi ya kusomba mizigo DRC na mengine ameyauza.

Alidai pia mtoto huyo wa rais anamiliki makampuni ya ujenzi wa barabara na maeneo mengi ya ardhi kwa lengo la kujenga maghorofa ya kupangisha.
“Huyu ni mtoto mdogo, kamaliza shule juzi, pesa za utajiri wote huu kazipata wapi?” alihoji Mtikila.

Hata hivyo, wiki iliyopita, Ridhiwani alikaririwa na moja ya vyombo vya habari akisema kuwa yuko tayari kutoa ushirikiano kwa Dk. Slaa kuonyesha kila anachomiliki.

Kutokana na tuhuma hizo, Mtikila alimtaka Rais Kikwete naye ajivue gamba kwa kuonyesha mfano, vinginevyo ni uendawazimu kujivua gamba bila mkuu huyo wa nchi kujiuzulu urais na uenyekiti wa CCM.

Huku akionekana kuwatetea Edward Lowassa (Monduli), Andrew Chenge (Bariadi Magharibi) na Rostam Aziz (Igunga), Mtikila alisema Kikwete anawachezea wana CCM na Watanzania kwamba ana nia ya kuwatimua makada hao kwa madai kuwa ni mafisadi wakati yeye ni mshirika wao.

“Kikwete aanze kutoka yeye ndipo awanyoshee vidole hawa Mapacha Watatu alioshirikiana nao kwenye ufisadi wa EPA, Richmond na Dowans, vinginevyo anawadanganya Watanzania. Aanze yeye,” alisema Mtikila.

Alisema anashangazwa na Kikwete kuibuka na dhana ya kujivua gamba kwa kuwatosa marafiki zake watatu wakati chama hicho kina mafisadi lukuki.

Mchungaji Mtikila pia aliorodhesha miradi ya ufisadi aliyomhusisha nayo Kikwete na watendaji wengine serikalini kuwa ni pamoja na IPTL, uuzaji wa iliyokuwa Benki ya NBC, Meremeta, Richmond, Dowans, EPA na nyingine, kwamba zinawahusu watendaji wengi na si mapacha watatu pekee.

”Kikwete aliunda tume kubaini waliochota fedha za EPA na kutakiwa warudishe, lakini hadi sasa hatujui kina nani wamehusika, na kiasi gani cha fedha kilichorudishwa. Kama rais hahusiki na ufisadi huu, usiri wa nini?” alihoji Mtikila.

Alisisitiza kuwa hana maana kuwa Lowassa, Rostam na Chenge ni wasafi, bali anataka orodha ya kuwatimua mafisadi wa CCM iwe kubwa, akiwamo Rais Kikwete kwani ndilo gamba kubwa kuliko yote.

Kuhusu hatima ya CCM na kile alichokiita usanii wa kujivua gamba, Mchungaji Mtikila alisema chama hicho kina ugonjwa wa ‘Nambulila’ ambao mgonjwa hufa na kuzikwa akijiona.

“Wapangwa wana ugonjwa unaitwa Nambulila. Ni ugonjwa unaotokana na tego la mke. Mtu akitembea na mke wa mtu anaupata na anapokufa, anawaona watu wanavyomlilia, wanavyomuingiza kwenye kaburi, lakini hana uwezo wa kusema, hivyo anazikwa akiwa hai, akiona kila kitu. Ndivyo ilivyo CCM, inakufa ikijiona. Hii ndiyo Nambulila,” alisema Mtikila.

Alisema usanii wa kujivua gamba hauwezi kuinusuru CCM kwani ni dhana ya uendawazimu yenye lengo la kuwaghilibu Watanzania.

Sambamba na hilo, Mtikila aliwataja mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye, Joseph Warioba na Cleopa Msuya, kuwa ni miongoni mwa watu wachache wasafi ndani ya CCM.

Alipobanwa kueleza usafi wa Sumaye wakati miaka sita iliyopita alipata kumtaja kwamba ni fisadi namba moja, Mtikila alikiri kutoa kauli hiyo na kuongeza kwamba baada ya kufuatilia walibaini kashfa dhidi yake zilikuwa za uongo na zilipikwa ili kumrahisishia Kikwete njia ya kuwa rais.

“Kweli niliwahi kumtaja kama fisadi namba moja, tulipofuatilia tulibaini kwamba haikuwa sahihi na ndiyo maana leo namtaja kama mmoja ya viongozi wachache wasafi,” alisema.

Aliwataka wana CCM kutobeza ushauri wa viongozi hao wachache wasafi na kutolea mfano wa Warioba na Sumaye walivyoshambuliwa na UVCCM walipotoa mawazo yao.
 
Nimefuatilia thread nzima kwa umakini sana. Hao wanaotuhumiwa kutumia vibaya mali ya umma ni viongozi. Hivyo basi wanawajibika kujibu tuhuma zozote zile zitakazotolewa dhidi yao. Majibu hayo yasiporidhisha, mali yote ya hiyo ya umma irudishwe kwa wananchi, na hatua za kisheria zichukuliwe ipaswavyo. Kuna haja ya kuodhoresha tuhuma zote zinazosemwa, ili hiyo siku ya siku ikija, watu wawajibike. Ni imani yangu kuwa siku hiyo inakuja.
 
kWANI HAMKUJUA HAYA CCM MLIPOIPA TENA KIPINDI CHA KUONGOZA? TANGU KAHAMA MINING CORPORATION IMEANZA KUCHIMBA MADINI, NDEGE ZAKE HURUKA NA KUPELEKA MADINI ZINAKO KUJUA ZENYEWE, AIDHA, MAGARI MAKUBWA YA KUBEBA UDONGO UNAOSEMEKANA UNA MADINI, ULIKUWA UKISOMBWA KUTOKA KAHAMA SHINYANGA NA KUPELEKWA BANDARI YA TANGA ILI USAFIRISHWE NJE ZAIDI YA MIAKA 10 SASA? KAMA HAYO YANAFANYIKA, RIZI ATASHINDWAJE KUNUNUA HAYO MAGARI 100?
 
Ben;1918188]Every moment in life is a moment of history. Every present action immediately becomes past and roles played today will be remembered tomorrow with pride or shame, satisfaction or regret[/COLOR]. Yet some moments are clearly more momentous than others, and represent far greater opportunities and dangers. These are often moments of crisis, a word which in its Japanese form is written with two characters, the one representing danger, the other opportunity.

When looting from our coffers and culture of impunity becomes the order of the day,Tanzania reflects the truculent African tragedy.Let us unite against this social-economic vice embraced and celebrated by the Ruling elites at the expense of Poor Tanzanians.Let us Unite,let us Restore the Dignity of our people.Let us dare![/QUOTE]


Mkuu ukitumia maneno ya mtu mwingine ni vema ukaweka kwenye quote au lasivyo ni plagiarism (Hapo kwenye Red- by SANUSI LAMIDO SANUSI) na wala hujamcredit mtu aliyeyasema hayo maneno. Mbaya zaidi unacopy na ku-paste bila kujua mtoa mada alikuwa anaongelea nini na yanausiana vipi na mada iliyopo jamvini.

http://www.nairaland.com/nigeria/topic-281035.0.html
 
utajiri haukupeleki mbinguni wee ****,jenga heshima kwa watanzania wenzio tutakuheshimu,hela utazipeleka wapi,mbona watoto wa nyerere hawashutumiwi
 
Imerushwa kwenye taarifa ya habari saa 1 usiku huu ktk Channel 10. Mwenye ushahidi haya jamaaaaaaaani.......
 
hALAFU amesema anamiliki akaunti 3, crdb, Stanbic, na baclays, japo hajasema kuwa zina shiing ngapi!
Na anasema ana heka 1.5 za shamba, na si zaidi ya hapo!.ha ha haaaa!, mtoto kaguswa pabaya huyu, sasa atadhalilika!
Nadhani baba yake amemlazimisha ajitetee, vinginevyo anavuliwa gamba kwa maji ya moto!
 
Hana account visiwa vya Jersey huyu, hizi huwa hawazitaji. Ngoja tusubiri tuone, najua ushahidi upo labda aje aukanushe. Dr wa Ukweli huwa hakurupuki.
 
Anapaswa kujua kuwa juhudi alizokuwa anafanya za kubadilisha baadhi ya majina yake kwenye kumjiliki Ginneries mbalimbali sio siri , zitawasilishwa nyaraka atapata aibu sana huyu kijana mwenzangu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom