UTAFITI: Umaarufu wa wasanii wanaishabikia CCM umengua ghafla!!

Losambo

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
2,612
864
Tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oct - 2015, wasanii mbali mbali walijitokeza kuunga aidha UKAWA au CCM. Ni ukweli usiopingia CCM imekusanya kundi kubwa la wasanii kama akina Wema Sepetu, Diaomond Platinumz, Ali Kiba, Peter Msechu, JB, na wengine wengi kama Original Komed.

Katika hao wapo waliokuwa wanajihusisha na kampeni zaidi mtandao, kwa maana ya live politics na wapo ambao walikuwa wanasoma alama za nyakati yaani ni kama wapo hawapo.

Katika group ambao walikuwa wanafanya kampeni kwenye mitandao kama INSTAGRAM, FB, Twitter kwa ujumla umaarufu wao umeshuka tofauti na awali. Katika kuthibitisha hili, unaweza kukuta post zao zinaweza kuwa na likes kama 500 hivi licha ya masaa mengi kupita jambo ambalo halikuwa kawaida. Mfano ni Blogger Mange Kimambi, Wema Sepetu, Diamond Platinumz na wengine wengi katika post zao kisiasa wemekuwa wakipata likes chache na maoni hasi kuwa wamepotea.

Hali ni tofauti kabisa kwa wasanii waliojitokeza UKAWA kama akina Aunt Ezekiel, Shamsa Ford na wenzake, clips na picha zao Instagram, Facebook, Whatsupp zimekuwa lulu. Watu wanaonyesha kuzipokea kwa shangwe kwa kupata malikes ya kutosha licha na comments za kuwatia moyo.

Huo ni uthibitisho tosha kwamba tusiishi kwa mazoea, wasanii wanatakiwa wasome alama za nyakati na hata ni maslahi basi usijiingize katika live politics kwa maana zinaua umaarufu na kukushusha labda kama uwe UMEAMUA SIASA KUWA KAZI YAKO.

Na mwisho hii, ni kama utabiri wa upande ambao unakubalika sana ambao unaweza kuwa mshindi.

Nawasilisha
 
upepo wa mabadiliko utavuma na kuwavurumisha huko.....
 
Wajiandae kuuza madira & kupiga wenzao majungu watakao wafunika baada ya Lowassa kuchukua nchi.
 
Ni kweli kabisa mkuu

Yaani kama Wema na Mangi watu wanawatukana sana, hali iliyopelekea Diamond kutulia kupiga kampeni maan watu walikuwa wanamwambia, mbambie Kinana na Nape wakupigie kura. Usicheze na siasa.
 
Mwanangu yaani umeongea ukweli hata wale watoto wa Yamoto band wamepungua mvuto siasa inatakiwa usome alama za nyakati...nimeona saiv Jacqueline Wolpher ameoneza mafollower kwa 40% kwenye instagram account yake.
 
Kuna ukweli flani hivi wao wanafikiri influence yao inaweza kuchange hali halisi. Post zao comments chache na likes bora wangekua wanaongea Facts wao ni uongo dhahiri usio na mashiko
 
Tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oct - 2015, wasanii mbali mbali walijitokeza kuunga aidha UKAWA au CCM. Ni ukweli usiopingia CCM imekusanya kundi kubwa la wasanii kama akina Wema Sepetu, Diaomond Platinumz, Ali Kiba, Peter Msechu, JB, na wengine wengi kama Original Komed.

Katika hao wapo waliokuwa wanajihusisha na kampeni zaidi mtandao, kwa maana ya live politics na wapo ambao walikuwa wanasoma alama za nyakati yaani ni kama wapo hawapo.

Katika group ambao walikuwa wanafanya kampeni kwenye mitandao kama INSTAGRAM, FB, Twitter kwa ujumla umaarufu wao umeshuka tofauti na awali. Katika kuthibitisha hili, unaweza kukuta post zao zinaweza kuwa na likes kama 500 hivi licha ya masaa mengi kupita jambo ambalo halikuwa kawaida. Mfano ni Blogger Mange Kimambi, Wema Sepetu, Diamond Platinumz na wengine wengi katika post zao kisiasa wemekuwa wakipata likes chache na maoni hasi kuwa wamepotea.

Hali ni tofauti kabisa kwa wasanii waliojitokeza UKAWA kama akina Aunt Ezekiel, Shamsa Ford na wenzake, clips na picha zao Instagram, Facebook, Whatsupp zimekuwa lulu. Watu wanaonyesha kuzipokea kwa shangwe kwa kupata malikes ya kutosha licha na comments za kuwatia moyo.

Huo ni uthibitisho tosha kwamba tusiishi kwa mazoea, wasanii wanatakiwa wasome alama za nyakati na hata ni maslahi basi usijiingize katika live politics kwa maana zinaua umaarufu na kukushusha labda kama uwe UMEAMUA SIASA KUWA KAZI YAKO.

Na mwisho hii, ni kama utabiri wa upande ambao unakubalika sana ambao unaweza kuwa mshindi.

Nawasilisha

Viva roma viva lowasaaa.
 
Sio kila mtu anaakili fupi kama zako, tupo tunaojieleea na ni wengi zaidi yenu...

Ndio maana propaganda za kuunfollow wasanii zimefeli Diamond kkaliprove hilo baada ya kuwafikisha milioni jana...

Jamani ladynaa...unakimbizwa??
Dismond tena?
 
Back
Top Bottom