Wasanii wa Pwani ya Mombasa Kenya wana uwezo kuliko wasanii wa Tanzania, tatizo hawana platform

incredible terminator

JF-Expert Member
Aug 1, 2016
2,229
3,525
Kenya mombasan ina Vijana wanaojua sana Mziki, Kiufupi wanajua kuandika, wanajua kupangilia production wanajua kupangilia melodies na vocal tatzo sijui kwanini hawavumi kama wasanii wa Nairobi Kenya ambao ndio wana majina makubwa ambayo hawayatendei haki.

Wasanii wa Nairobi kusema kweli hawajui kuimba zaidi ya kuropoka na kuruka ruka tu hawasa Swaga, wala hawana panchline hawatumii akili kubwa kuandika nyimbo zaidi ya kuchanganya kikalenjini, kiluya, kikisii, pamoja na kikikuyu kiswahili na broken English na kutafuna mirungi (moghokaa) Kwenye video zao,

Japo wapo wachache akina NYANSHISKI, BIEN wa SAUTISOUL,
WILLY PAUL, NADIA MOKAMI, Ambo kwa namna moja wanajitahidi lakini Bado hawafiki hata Robo ya Vichwa vya Mombasani tatzo hawana Majina na ukubwa unaonedana na kazi zao.

Mombasa kuna producer Anajiita TK2, PRODUVISHIZZO, Huyu mwamba kwa bongo tufanye heshima yake ni kama tukichanganya vichwa vya akina ABBA, SHEDCLOVEOR, BOB MANECK , JIMMY ,MOCOGENIUS na NAZDAAH Wote ndio wanafikia mikono ya huyu mwamba mmoja nahawa ndio mafundi wa BEAT TZ zisizokuwa na makelele na ma sample kibao ya Hip hop za kimarekani.

Mombasani Kuna vijana akina

Otile brown
Chikuzee
Masauti,
Dogo Richie,
Klech Africanaa
Fund Echo,
Karntonah,
Dadysele,
Susumila

Hawa jamaa ni moto wa kuotea mbali lakini hawajulikani labda Otile Brown kidogo yuko mainstream kiasi chake.
Ila hao wengine hawana majina makubwa,

Nakuwekea hapa Piano mbili tu za huyo ECHO alafuz zitaftie mfanano wake hapa Tz na dogo hajulikani..

Klech Africanaa
 
Attachments

  • Kelechi Africana - MY ONE.mp3
    2.1 MB
Mkuu nimeziskiliza vizuri,kwanza kuhusu uandishi ni wazi watu wa Mombasa wanawazidi wa Nairobi sababu wao wanajua kiswahili vzuri maana ukumbuke hao ni watanzania kabisa ila ni mambo ya mipaka tu na wakiloloni,ila kuhusu kuwafikia watanzania hapana Bado sana tena sana,huyo Otile brown tu hamuwezi hata da prince .
 
Shizzo huyo wa enzi za Sugua Gaga. Ni producer wa singeli na Mnanda kwa huku bongo wapo kibao kitaa hasa kwetu uswazi.
Yaani producer wa mnanda analipwa beat ya harusi na rusha roho wala haiendi redioni.
kenya bado kimuziki, tanzania tatizo radios na promoters hawajaenda shule.
 
Mkuu nimeziskiliza vizuri,kwanza kuhusu uandishi ni wazi watu wa Mombasa wanawazidi wa Nairobi sababu wao wanajua kiswahili vzuri maana ukumbuke hao ni watanzania kabisa ila ni mambo ya mipaka tu na wakiloloni,ila kuhusu kuwafikia watanzania hapana Bado sana tena sana,huyo Otile brown tu hamuwezi hata da prince .
Majamaa ni mafundi sana ngoja nikuwekee pini zingine za Echo
 
Sikiliza hii ya echo na kelech huku ni wapi kisha rudi namajibu
 
Haya Bhn mdg mdg nipo nasikiliza Nyimbo zako? Vijana wenu sio wabaya lkn utambue mziki wa Tanzania ni Level nyngne.

Sema Siku hiz watu hawatumii Nguvu sn wanatafuta Pesa (Music unabase kwenye Beat kuliko Content maana Mashabik ndy wanautaka huo music lkn sio kwamba hawajui kuandika mashairi)
 
Ukiskiliza nyimbo za hao vijana zimekidhi vigezo vyote
 
Wabongo wako juu sana kimuziki East Africa tunawaburuza wote.

Ila huyo chalii masaut ana goma lake "dawa ya baridi" alinyoosha ikanyooka, kudos.
 
Masauti yuko vizuri ndiye anaweza kucompete na wabongo, ila sijui kakwama wapi sikuhizi simsikii
 
Labda masauti tu hapo wengine peleka huko kalenjin
Mkuu labda mnamjua masauti tu ila mtu kama dogo richie, kelech Africanaa pamoja na Echo wapo vzuri sana tatzo ndo hawajulikani ndio maana hamuwazungumzii jaribuni kuwapa maskio mtakuja kunishukuru
 
Wabongo wako juu sana kimuziki East Africa tunawaburuza wote.

Ila huyo chalii masaut ana goma lake "dawa ya baridi" alinyoosha ikanyooka, kudos.
Kwa kuwa unajua msauti alivyoimba na Winie ila hao niliowataja hapo kila mtu ni fund mno
 
Back
Top Bottom