Utabiri wa Shehe Yahya umetimia?!

Hebu sikia mkuu! Kitu chenyewe kinaitwa "Utabiri". Kitu kilichotabiriwa maana yake chaweza kutokea au kinaweza kisitokee. Utabiri is not a certain foreseen event. Utabiri unaacha mwanya wa jambo kutotokea pia. Ndo maana unaitwa utabiri. Shida ya wengi wanataka utabiri uwe na jibu hakika, kamili, lisilo na mashaka. Huu si utabiri tena.

Sikulazimishi uamini hayo yaliyotabiriwa. Unaweza kuyabeza pia. Lakini unapoyabeza uwe na grounds badala ya kusema tu "hakuna kitu hapo". Huwezi kuyabeza tu kwa vile hakutaja jina la mtu, na hakusema tarehe.

Mkuu ina maana gani siyo lazima itokee? Kwa hiyo hata mimi nikitabiri vitu visipo tokea na mimi utaniita mtabiri? Si siyo lazima vitokee? Accuracy ya utabiri ndiyo inayo prove mtu katabiri au laa. Ndiyo maana nikasema mimi personally siamini kwa maana ukitabiri kitu in general chances are something related to it kitatokea. After all this is my personal feeling so sioni sababu ya wewe kujisumbua na mimi nafikiria nini. Mimi simbezi ndiyo maana nikasema mimi siamini so anayetaka kuamini na amini it is a personal choice. Sasa sioni why tubishani juu ya kitu ambacho mimi kama mimi nina uhuru wa kuamua kukiamini au la.
 
Mie natabiri kwamba wiki mbili zijazo kuna baadhi ya wanaJF hawato log in.......tuone kama haitakuwa kweli...
 
Majuzi alitabiri mechi ya yanga na simba mbona mambo yalikuwa tofauti?
Huyu mchawi mwana wa shetani na ibilisi amelaaniwa, anatumiwa na shetani, atakula matunda ya shetani. asipobadilika, na yeye ataaibika na ataenda njia anayowatabiria wenzake. akifika huko ndo atagundua Yesu ni Bwana au la. Mungu na ammalizie mbali.
 
Du! jamani!
 
Jamani hii si lugha ya Mwana wa Mungu. kwa nini unamlaani mzee wa watu? Hata kama hukubaliani na namna zake ilitosha tu kumwombea badala ya kumhukumu na kumkabidhi kwa shetani. Umevuta mpaka.
 
Hebu sikia mkuu! Kitu chenyewe kinaitwa "Utabiri". Kitu kilichotabiriwa maana yake chaweza kutokea au kinaweza kisitokee. Utabiri is not a certain foreseen event. Utabiri unaacha mwanya wa jambo kutotokea pia. Ndo maana unaitwa utabiri. Shida ya wengi wanataka utabiri uwe na jibu hakika, kamili, lisilo na mashaka. Huu si utabiri tena.

Sikulazimishi uamini hayo yaliyotabiriwa. Unaweza kuyabeza pia. Lakini unapoyabeza uwe na grounds badala ya kusema tu "hakuna kitu hapo". Huwezi kuyabeza tu kwa vile hakutaja jina la mtu, na hakusema tarehe.

Babuyao,

Heshima mbele.

Ukweli ni kwamba when you make a prediction it will happen.Anything
contrary to that basi sio prediction...na ndio hayo baadhi ya wachangiaji
wanasema.Sheikh ni msanii tu na anabahatisha karata zake kwa kutoa
'generalities' instead of 'specifics'.

Shukran.
 
alitabiri kifo cha kiongozi na mtu maaraufu nchini kutokea mwezi juni

tayari wafuatao wametutoka:

  1. kaimu mufti mkuu, sheikh suleiman gorogosi
  2. prof haroub othman
kabla yao alitangulia mwana mipasho bi. Nasma khamis kidogo. Kumbe hii sayansi ya nyota inafanya kazi!

dah...
Angekuwa anataja na wajihi japo kwa kiasi kidogo kungetufanya tumuamini maneno yake.
Sasa yeye yuko very general kiasi kwamba utabiri wake unaonekana kama
 
Kutabiri ni neno la kiswahili lililojaza maana nyingi, pengine ubishi upo katika maana zenyewe. Utabiri kwa kiingereza ni either foresee au forecast.

Forecast ndo utabiri unaotumiwa kwenye hali ya hewa hata kwenye masoko, hii ni sayansi. Ingawa kuna utaalam wake forecasting haina maana vile ulivyoforecast lazima iwe. Lakini unatoa best guess kutokana na hali halisi ya mazingira yaliyopo na uzoefu ulio nao kuwa hali ikiwa hivi kesho inaweza kuwa vile. Kuna computer models ambazo zimeshakuwa developed na hizo husaidia kufanya forecasting.

Hiki anachofanya Shekhe Yahya si forecasting. Ni foreseeing. Foreseeing ndo walizokuwa wanafanya watu kama kina nabii Yusuf walipotabiri miaka ya njaa na miaka ya chakula kingi. Hii haina sayansi bali ni maono. Ndo walichokuwa wakifanya manabii enzi hizo.

Sasa wataalam uchwara wa enzi hizo walijaribu kutafuta mbinu mbadala za kuwasaidia kufanya wawe wanatabiri kama manabii. Hii ndo astrology. Kusema kweli wenyewe wanaoifuata elimu hii wanakuambia ni sayansi na wanazo principles zao. Lakini peer review nyingi zilizofanyika zimethibitisha kuwa sayansi iliyoko huko si lolote si chochote bali ni ushirikina fulani tuu. Unahitaji kuamini zaidi kuliko kutumia mbinu za kisayansi zinazojulikana. Kwa hiyo wataalam wenyewe wa sayansi wanaiita PSEUDO SCIENCE au sayansi feki.

wafuasi wa sayansi hii feki hupenda kuwaaminisha watu kuwa hii ni sayansi kabisa na ukweli wanatoa mifano hiyo ya kwenye biblia (ya mamajusi wa mashariki walivyotumia utaalam huo kutabiri kuzaliwa nabii Issa au Yesu) kutetea uhalisi wa sayansi inayotumika. Na hupenda watu waamini kuwa wanachokisema ni foreseeing sawa na ile ya manabii. Lakini mbinu za kawaida za kisayansi zimeshindwa kuthibitisha ukweli wa madai hayo na kwa hiyo wanasayansi wenyewe hawaiamini.

Astrology ni mchanganyiko wa sayansi feki na ushirikina pamoja na imani za kale. Haina uhusiano na forecasting ya hali ya hewa. Na haina uhusiano na foreseeing ya manabii. Wenyewe wanataka watu waamini kuwa ni sawa na foreseeing.
 
Hii ni moja ya sanaa ambayo ina amsha hisia zetu wanadamu ili maisha yaendelee kila kukicha, Hivyo tumpongeze tu kwa ku plei his party wakati huu wa uhai wake kwa kufanya utabiri. Wengine wanaamini na ni part ya maisha yao. Tukumbuke maisha ni mchanganyiko wa activities. Wengine huwekeana madau kabla ya mechi, vitu kama hivyo.
 
Alitabiri kifo cha kiongozi na mtu maaraufu nchini kutokea mwezi Juni

Tayari wafuatao wametutoka:

  1. Kaimu Mufti Mkuu, Sheikh Suleiman Gorogosi
  2. Prof Haroub Othman
Kabla yao alitangulia Mwana mipasho Bi. Nasma Khamis Kidogo. Kumbe hii sayansi ya Nyota inafanya kazi!

Hivi huyu mzee anafanyaje kuweza kuyaona haya? To be honest, si kila mtu anaweza kutabiri at this level of specificity and consistency. Hivi kuna mtabiri mwingine kijana hapa nchini anaweza kumkaribia (maana naona yeye ameanza kuchoka)?
 
Wataalamu wa mambo "yanayoonekana na yasiyoonekana" wanaigawa reality katika sehemu 3:
a. Mbingu au makao ya mwenyezi Mungu (supernatural world)
b. Ulimwengu tunaoishi (natural world) ambao tunaufahamu kwa njia ya milango 5 ya fahamu
c. Ulimwengu wa katikati (praetaenatural world). Huu ni ulimwengu wa roho, wa malaika wema na wabaya. Binadamu anaweza kuuingia ulimwengu huu kwa njia ya nguvu za Mungu (mf. utabiri wa manabii : Mungu anamshirikisha mwanadamu elimu yake kama atakavyo).
Binadamu pia anaweza kuuingia ulimwengu wa roho kwa njia ya pepo (majini - nguvu za giza).Pepo anaweza kumchukua mtu kiroho tu au kiroho na kimwili na kumpeleka mahali pengine (translocation) na kumfahamisha mambo ambayo wanadamu hawawezi kwa nguvu zao za kawaida kuyafahamu. Jambo hilo linaitwa Astral projection
Kwa sababu hiyo mtu anawezeshwa kuyafahamu mambo ya wakati ujao, mambo ambayo kimsingi ni haki yake Mungu peke yake kuyafahamu. Ni kama kumwibia Mungu maarifa, na kujifanya Mungu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom