Utabiri: Rais ajaye Tanzania (2015) ni Mwanamke

Mwanamke gani huyo wa kuliongoza Taifa hili? Kama huyo anayeongoza mhimili mmoja tu wa Serikali AMETEPETA,huyo atakayepewa nchi itakuwaje?
 
hata emanuel wa emanuel tv alitabili lowasa atakuwa presideee sijui nae ni mwanamke
au watabili wanagongana coz ni waongo
 
Niliwahi kusema kama ukisoma post zangu za nyuma, na narudia na kuthubutu kusema kua watamsimamisha ASHA ROSE MIGIRO, mark my words
 
yule mtabiri wa vifo vya wengine aka-shindwa kutabiri chake?.Ndo alimpa ulinzi usio-onekana kwa macho zaifu.....lol.

alitabiri match ya watan s na y tukataka kuchoma moto kabanda kake ka magomen hizo ke peleka far
 
JUMATATU, JANUARI 07, 2013 04:48 NA KHAMIS MKOTYA

*Sheikh asema atashinda kwa nguvu kubwa
*Awakata maini Lowassa, Membe, Sitta, Dk. Slaa

MWENYEKITI wa Taasisi ya Kiislamu ya Imamu Bukhary, Sheikh Khalifa Khamis, amejitokeza hadharani na kutabiri matukio yatakayojiri mwaka huu kuelekea mwaka 2015.

Sheikh Khalifa ambaye ni mmoja wa wanazuoni wa Kiislamu nchini, alisema mwaka 2013 utatawaliwa na mjadala mkubwa kuhusu mrithi wa Rais wa sasa, Jakaya Kikwete ambaye anamaliza muda wake.

Kiongozi huyo wa kidini alisema, upo mpango unaoandaliwa kwa siri wenye lengo la kuwasambaratisha wanasiasa wanaojipanga kuwania urais, ili kumweka katika soko la siasa mwanamke msomi atakayegombea nafasi hiyo.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, Sheikh Khalifa alisema mwaka 2013, unatazamiwa kuwa wenye matukio makubwa yakiwamo majanga ya moto, mafuriko na vimbunga vitakavyoleta fazaa kwa watu.

Hata hivyo Sheikh Khalifa, alisema utabiri wake huo unatokana na elimu ya kuambiwa, tofauti na ule uliokuwa ukifanywa na marehemu Sheikh Yahaya Hussein, unaotokana na elimu ya nyota.

Kiongozi huyo alisema iwapo hakutatokea sababu za kuahirishwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, ishara zinaonesha kuwa rais ajaye aidha atatokea Kaskazini au Kusini, lakini hatokani na majina ya viongozi wanaotajwa kwa sasa.

Kwa upande wa Kaskazini viongozi wanaotajwa kuwania urais mwaka 2015 ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM) na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), DK. Willbrod Slaa.

Kwa upande wa Kusini anayetajwa kuwania urais ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (Magharibi).

Wengine wanaotajwa kwa mbali ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa zamani wa Hanang' Frederick Sumaye, anayetoka Kanda ya Kaskazini na Zitto Kabwe (Magharibi).

Kiongozi huyo alikwenda mbali zaidi katika utabiri wake na kusema kuwa, upo mpango unaoandaliwa kwa siri na kundi dogo la viongozi serikalini.

Alisema mpango huo wa siri unalengo la kumuandaa na kumuweka kwenye soko la siasa mwanamke msomi na maarufu, kwa lengo la kumjengea uwezo wa kusimama kugombea nafasi hiyo mwaka 2015.

"Ingawa mpango huo unaonyesha utaundiwa mkakati wa hali ya juu, lakini pia utapingwa kwa kutumia nguvu kubwa sana na endapo utafaulu mwanamke huyo anaweza kuwa ndiye rais ajaye," alisema.

Siasa

"Katika medani ya siasa mwaka huu hapa nchini, kutakithiri na kuenea habari nyingi za uzushi, uongo na utesi wenye shabaha ya kuchafua majina ya baadhi ya viongozi waandamizi wa kiserikali na wanasiasa wenye mvuto.

"Janga hili litawaangukia zaidi wanasiasa ambao wako katika nafasi nzuri ya kukubalika mbele ya wananchi, kuelekea maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015," alisema.

Mbio za urais 2015

"Pamoja na baadhi ya wanasiasa kujidhatiti katika maandalizi ya kujiweka tayari kugombea nafasi ya juu ya uongozi wa nchi (urais), mjadala utakaotawala mwaka huu 2013 ni kuhusu rais ajaye, baada ya Rais Kikwete kumaliza muda wake.

"Lakini pamoja na jitihada zilizokwishafanyika na zitakazoendelea kufanyika katika kipindi cha mwaka huu, hakuna ishara inayoonesha nyota njema kwa yeyote miongoni mwa majina yanayotajwa hivi sasa kuweza kufikia lengo hilo," alisema.

Vyama vya upinzani

Kuhusu vyama vya kisiasa, alisema hakuna ishara inayoonesha kuibuka kwa vyama vipya vyenye nguvu au kuimarika zaidi vyama vilivyopo, badala yake inaonesha katika kipindi cha mwaka 2013, chama kikuu cha upinzani (CHADEMA) kitaendelea kuimarika.

"Ishara yenye kuonyesha kuendelea kwa ghasia za kisiasa, maandamano na maneno ya kejeli dhidi ya Serikali na viongozi wake, bado imesimama.

"Lakini hata hivyo wazo la kuunganisha nguvu za wananchi pamoja kwa nia ya kuiondoa Serikali madarakani nje ya utaratibu wa Katiba halitafanikiwa," alisema Sheikh Khalifa.

CCM

Kuhusu hali ya kisiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sheikh Khalifa, alisema katika kipindi cha mwaka huu kuna ishara ya kuongezeka kwa mizozo, chuki na makundi yenye uhasama ndani ya chama hicho kikongwe.

"Hali hiyo itakifanya chama hicho kuwa katika uongozi wa makundi, kwani baadhi ya wanachama wake waandamizi watatokwa na staha na adabu kwa viongozi wao wa ngazi za juu na kufikia katika hatua ya kuingia katika magomvi na kutangaza aibu za baadhi yao hadharani.

"Katika kipindi cha mwaka huu, hakuna ishara inayoonesha kuwa makundi hayo yatakuwa na nguvu ya kupindukia na kusababisha chama hicho kusambaratika.

"Bali yanaonesha makundi hayo yatakuwa ndiyo sababu ya chama hicho tawala hatimaye kuja kuongoza Serikali itakayofanana na meza ya mraba, lakini yenye miguu mitatu.

"Ipo ishara inaonesha kuwa, kuna misaada mingi itakayoingizwa nchini kwa anuani ya kuimarisha demokrasia, wakati lengo na madhumuni ni kuundoa utawala wa CCM, chama ambacho wakoloni hawakitaki," alisema.

Hata hivyo kiongozi huyo alimfagilia Rais Jakaya Kikwete nakusema kuwa, mwaka huu atang'ara zaidi katika medani ya kimataifa na kusifika katika eneo la utawala bora na usimamizi mzuri wa misaada ya wahisani.

 
JUMATATU, JANUARI 07, 2013 04:48 NA KHAMIS MKOTYA

*Sheikh asema atashinda kwa nguvu kubwa
*Awakata maini Lowassa, Membe, Sitta, Dk. Slaa

MWENYEKITI wa Taasisi ya Kiislamu ya Imamu Bukhary, Sheikh Khalifa Khamis, amejitokeza hadharani na kutabiri matukio yatakayojiri mwaka huu kuelekea mwaka 2015.

ivi sheikh yahya aliacha mrithi?
 
Mtabiri maarufu ametabiri kuwa Rais ajae Tanzania atakuwa ni mwanamke. Utabiri huo utakuwa umewakata maini Mh Laigwanani na Mh wa Mambo ya nje.

Source: Magazeti ya leo kama vile Majira na Jambo Leo
Watanzania wazalendo tuyapige vita haya magazeti maana yanazidi kuhatarisha muungano wetu, mbona ni Laigwanan na mzee wa mambo ya nje tuu? Kwani wenzetu wamegoma?
 
Taifa la waabudu uchawi na unajimu wa kichawi

we dont deal with psychiatric people. Eti mtu msomi! Amepewa wizara nyeti ya ardhi mmeona ilivyomshinda? This is our most valuable ministry tulobakiwa nayo maana zingine zinamilikiwa na wawekezaji tena wazungu. Naye anabariki uuzaji wa ardhi tena kwa wazungu! Kwa mikataba ile ile ya miaka 99! Loh! Ningekuwa nashabikia ccm tibaijuka no. Bora hata mwakyembe na magufuli wanaoogopwa japo na wafanyakazi walio chini yao.
 
kumbe shekhe ponda nawao wameanza machaguo ya mungu wao itabidi tutafute din mbadara.kama gambia coz hata wanaofufua watatoa utabiri wakipewa chenj ya rada
 
Asharose Migiro ndiyo chaguo la JK na US...alienda kupikwa UN kama wale wa Liberia na malawi. huu ni mpango mkakati wa Economic Hit Men (EHM) unaoratibiwa na CIA...
 
ivi sheikh yahya aliacha mrithi?[/QUOT

Hao ni DUGU moja,yule NYOTA huyu KUAMBIWA (NDOTO a.k.a MAJINI),wafuga wanyama hewa mnashida......!,mwenzie alitisha mpinzani wa DHAIFU atakufa matokeo yake akafa yeye SASA kaibuka mwingine,mmmmh! nchi ya KISHIRIKINA maendeleo kuja ni jambo adimu sana mara sheikh(marehemu) katoa ulinzi usio onekana kwa macho,mara kikombe loliondo kwa BABU.
- Tuachanani na hawa MASHIRIKINA wanaturudisha nyuma kwa sababu za kijinga tu.naviongozi wetu nao ndo hao hao walala makaburini.tuondoe hizi takataka.
Tulisha ingia aibu ya karne pale kituo cha CNN kilipo fanya utafiti juu ya Ushirikina Vs Tekinokogia Kwa ukanda wa Afrika Mashariki,MAJIBU yake NI AIBU kwa TAIFA letu,KENYA waliongoza kwa technology wakati TANZANIA iliongoza kwa ushirikina(73% ya raia wote ni washirikina),wakati huo huo tukienda kwenye maendeleo kwa ujumla TANZANIA ya mwisho-
USHAURI:
TUPO JUU KISHIRIKINA ila TUPO CHINI KIMAENDELEO means kufuga majini HAKUTUSAIDIA ni bora TWENDENI SHULE tuajaribu sayansi/Elimu.TUWAKATAE WAFUGA MAJINI na tabiri zao+Watengeneza VIKOMBE na ulaghai wao.-
 
nchi hii bwana ina vichekesho sana ...Yaani atakuwa kama alivyo spika makinda au ..hahaaaaa ...bado sana

Mimi nahisi siyo taifa ndo lenye vichekesho ni hii post ambayo haina habari kamili na uhakika
 
Mtabiri maarufu ametabiri kuwa Rais ajae Tanzania atakuwa ni mwanamke. Utabiri huo utakuwa umewakata maini Mh Laigwanani na Mh wa Mambo ya nje.

Source: Magazeti ya leo.

Badala ya kutaja sifa za Rais ajaye watu wanataja majina! Au uanamke nayo ni sifa ya Kikatiba ya kuwa Rais jamani? Wengine wamethubutu kutaja hata maeneo, kwamba Rais wa safari hii atatokea eneo fulani! Kwa kweli nchi haina mwelekeo kwa sasa!
 
Haka ka nchi kanavituko kweli,ni ajabu yaani kwa karne hii bado watu wanaamini haya madudu!!kazi kweli kweli.
 
Back
Top Bottom