Utabiri kwa miaka hii miwili 2024 na 2025

Bando la wiki

JF-Expert Member
May 23, 2023
319
884
Kwanza nipende kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kufikia siku hii ya mwisho ya mwaka 2023.
Kutokana na maisha yetu wanadamu kuwa na vipindi tofauti tofauti, nimeona niwaletee utabiri mfupi juu ya mwaka mpya inayokuja ya 2024 na 2025.

Mwaka 2024
Huu mwaka unaonesha utakuwa na utulivu sana hasa kwa nchi yetu ya Tanzania. Wananchi watakuwa na utulivu na mipango mingi ya watu itatimia.
-Ila kunaonesha kutakuwepo na mashimo mawili ambayo ki unajimu yanaonyesha kuna vitu au taasisi au watu wakubwa wataporomoka kutoka kwenye na ukubwa na henzi zao hadi kuwa vitu au taasisi au watu wa kawaida tu.
  • kitu kingine utabiri kuhusu Taifa stars ni kwamba ki roho kuna dude kubwa kama mtu lenye upanga mkali ambalo litaogopesha taifa stars katika mashindano ya AFCON 2024 na hivyo taifa stars itaishia kwenye makundi na kuna uwezekano akatoka pasipo pointi yoyote.
  • kwa utulivu utakaokuwepo 2024, wananchi wanaimizwa kujiwekea akiba hasa chakula maana mwaka 2025 utakuwa mgumu sana.

Mwaka 2025
Huu mwaka utakuwa mgumu sana hasa Tanzania.
  • Nimeona midomo ikiongea kwa fujo sana na kusababisha machafuko kwa baadhi ya maeneo nadhani ni kutokana mwaka huo kuwa ni mwaka wa uchaguzi chini Tanzania.
  • kutakuwa na joto kali sana duniani nadhani ni kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
  • Pia kidunia nimeona mwaka 2025 ni mwaka ambao kuna kitu kama moshi na giza litatapaka duniani nyakati za mchana hii ni kutokana na eitha mlipuko wa volkano kutoka ardhini au matumizi ya mabomu ya nyuklia ambayo yanaweza yakasababisha vumbi zito angani na hivyo karibia ulimwengu mzima ukapata madhara makubwa.

N.B
Mambo hayo yote hasa negative, yanaweza kudhibitiwa yasitokee endapo jamii itadumu katika Maombi na toba.
 
Kwa hiyo unatuambia siku 365 hizi zitakuwa nzuri halafu ghafla tu siku ya 366 na kuendelea hazitakuwa nzuri
 
Back
Top Bottom