Cartoon ya The Simpsons na utabiri wa 2024

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,861
Tunatoka mwaka 2023, tunaingia mwaka 2024. Huu ni mwaka ambao hao watawala wa dunia hii wanakwenda kufanya mambo makubwa sana, wanasema haijawahi kutokea. Kutakuwa na matukio makubwa ya vifo, hasa kwa viongozi wakubwa, kutakuwa na mambo mengi mabaya kuliko miaka mingine.

Nilikuwa naangalia katuni ya Simpsons, wameweka mambo mengi sana ambayo yanakwenda kutokea mwaka huo. Kwa kawaida hawa watu wakitaka kufanya mambo yao huwa hawafanyi kwa siri, ni lazima wakupe taarifa, ila taarifa zao huwa zinakuwa na mafumbo mengi mno.

Ishu za Balenciaga, Google, Youtube kumilikiwa na mawakala wa shetani hata katuni hizo zimeonyesha, ila huwezi kugundua mpaka uambiwe, manake zinakuwa zimejaa mafumbo mengi.

Kwenye katuni yenye maunabii yao basi ni hiyo. Niwakumbushe tu kwamba hiyo katuni imeanza kutengenezwa na jamaa ambaye ni Freemason, na kwa sababu dunia ipo kiganjani mwao na wao ndiyo wanaopanga matukio, wanaelezea kila kitu kinachokwenda kutokea.

Walitoa utabiri wa kuzama wa Submersible Titan kale kakifaa ka watalii walioenda kutizama meli ya Titanic chini ya bahari wakapotea, Walitoa utabiri wa kifo cha Kobe Bryant kwa helkopta, wakaja wakatoa ya Trump kuwa rais wa Marekani, wakaonyesha mpaka hiyo ya earth firmanent jinsi inavyokuwa inailinda dunia na hakuna mtu kutoka humo, yaani walionyesha kila kitu, video nitazitafuta nizione.

Hawa majamaa wanatoa meseji zao kwa mafumbo makubwa, wanamuiga Mungu kwa namna alivyoongea kimafumbo kwenye vitabu vya dini. Taarifa zote wanazotoa huwa na mafumbo.

Hata ukiangalia muvi, wanaweka sana symbol zao lakini huwezi kuziona kwa haraka, huwa zinapita tu, ile inaonyesha kwamba hata Hollywood ni mali yao pia.

Mwaka 2024 washikaji wanausubiri sana kwa sababu wana maunabii yao mengi waliyaweka na mwaka huo yanakwenda kutokea. Utakuwa ni mwaka wa matukio makubwa, utakuwa ni mwaka ambao inawezekana hujawahi kuhushudia kwenye maisha yako, ni mwaka ambao wameuwekea viporo vingi sana, na inawezekana kuna mengi yatakwenda kukushangaza.

Sitaki kuyataja hayo maunabii yao ya mwaka huu wa 2024 kwa sababu moja tu, bado hamjajua wapi pa kushikilia. Kwa vitabu vya Mungu ama vitabu vya wanasayansi!!!!

1703506141826.jpg
 
The so called wazungu wako mbele ya muda,japo wakati fulani wanapenyeza agenda zao kupitia hizi movie nk..hicho wanachojifanya kukitabiri ni mipango yao tu madhubuti ya kuindesha dunia,hayatokei kwa bahati mbaya yako scripted.
 
Back
Top Bottom