Usisubiri mzazi akuombe ndio umpe, sio busara

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
11,169
15,851
Wakuu kuwasaidia wazazi wetu tusisubiri simu ya haloo baba tunashida huku,alafu wewe ndo unatuma alfu kumi,sio busara. Ukipata chochote tuma japo 10% ya ulichopata sio mpaka wakuombe,nao watu wale wanaonaga jau kuomba kila mara.

Usisubiri upate laki ndo utume alfu 30, wewe umepata kidogo tuma kidogo watajua kuwa dogo anatujali, huongeza baraka sana. Wakati mwingine hasa baba zetu wanaona shida kuomba pesa kwa dogo kila time badala yake wanakufa na tai shingoni huku dogo akisubiri kupogiwa simu kuombwa.

Kama ambavyo utotoni ulikuwa hupeleki maombi ya kula mchana na jioni,wewe ulikula bila kuomba kwa sababu wazee walikuthamini.

Kumthamini mtu zaidi ni kumpa kabla hajakuomba.
 
Ujumbe murua

Daah! yaani tangu niingie JF pengine huenda huu ndo ukawa uzi nilioupenda zaidi kuliko zote...

Mola akujaalie kila la heri na akubariki sana uwe ni miongoni mwa walioheshimika kabisa

Aamin
 
Japo nimetuma siku siyo nyingi ila kwa kuipa heshima Uzi wako Leo natuma tena...Mwenyezi MUNGU awape maisha marefu wazazi wangu ili wafurahie matunda ya mtoto wao hapa Duniani.
Sahihi mkuu,

Kumsaidia mzazi ni wajibu,na mtu mwerevu haombwi katika kutimiza wajibu wake.

Ndio maana hata baba huwa hasubiri kuombwa huduma pale nyumbani,ukiona baba anasubiri kuombwa huduma basi kuna shida
 
Back
Top Bottom