PMWAKA
Senior Member
- Aug 29, 2019
- 191
- 206
Should we thank GOD/ ALLAH
?!
Mungu vinywa vyetu vimejawa na maneno ya Shukrani.
Tunashukuru kwa ajili ya 2020, umekua nasi January mpaka December.
Asante kwa yale ambayo umekwisha kuyafanya, asante kwa yale ambayo bado hujayafanya, asante kwa yale ambayo umefanya kwa sehemu tuu, Tunaomba tunda la uvumilivu likajae kwa wingi ndani yetu na kutuandaa kupokea yale uliyokusudia kwa mwaka ujao.,
Nyakati za usiku tukiwa hatujitambui, hukulala wala kusinzia, ulitulinda na ulitupa nafasi nyingine ya kuona siku mpya.
Tukiwa barabarani, ulituepusha na ajali, katika biashara zetu hatukupungukiwa bali Bwana ulitusaidia tukapata kwa sehemu.
Katika huduma zenu, tumeona Neema yako ikituongoza na kutusaidia kujua tunachopaswa kufanya kwa wakati na majira fulani.
Mbingu hazijawahi kunyamaza na kuacha kutusikia, tumeshuhudia ukitushika mkono na kutuvusha, tumeshuhudia ukituganga mioyo kwenye nyakati ngumu, tumeshuhudia ukituzungushia watu wanaotusababisha tuone bado ipo sababu ya kukuamini.
Katika utafutaji wetu, kuna nyakati tulikosa kabisa lakini wewe Baba hukutuacha tulale njaa, bado ulionyesha vile ulivyo mwaminifu na wa haki.
Tukiwa masomoni, kuna nyakati ada zilisumbua, tukahisi hatutamaliza masomo, lkn Bwana uaminifu wako hatuwezi kuelezea, hata sasa umetusaidia, tumeuona mkono wako.
Kuna nyakati upatikanaji wa kodi ulikua mgumu, lakini tunakushukuru hatukuwahi kulala nje, tukapigwa na jua wala mvua.
Kuna nyakati tulipoteza nuru katika nyuso zetu, lakini hukuacha kututia moyo na kutushika mkono, kuna nyakati hatukuona sabb za kuishi kwasbb ya yale tunayoyapitia lakini wewe Mungu hukuacha kusema nasi kwa namna fulani.
Yapo tuliyoyaomba, tunaona yamechelewa kibinadamu, lkn tunajua ipo siku yatatimia na tutajawa na kelele za shangwe.
Tuliomba mtaji, ukatupatia, tuliomba afya njema, ukatupatia, umetuhurumia, umetutetea, umetupenda kwa uvumilivu.
TUSEME NINI Mungu, zaidi ya KUKUSHUKURU..
Pokea sifa hizi Mfalme wa wafalme..
Tunakurudishia sifa, heshima, utukufu na adhama, UNASTAHILI MFALME...!