Usinunue vitu online kwa kutipia TIGO MASTERCARD!

Juakali jr

JF-Expert Member
Aug 8, 2019
694
1,682
NItakupa sababu mbili muhimu kwanini usitumie kadi yako ya TIGO mastercard kununua vitu online.

1. Hii kadi wameunganisha mojamoja na akaunti ya Tigopesa, hamna control ambayo mteja unakua nayo kudhibiti kiwango cha juu ya muamala pale ambapo akaunti yako inakiasi cha kutosha kufanya muamala zaidi ya mmoja.

2. Accountability, support ya Tigopesa ipo very poor, haijibu kwa wakati na haitaki kubeba majukumu ya kutatua matatizo pale yatakapotokea. Ili uwezekuelewa vizuri ngoja nikupe mapito yangu ya hivi karibuni.

Kisa: Mwezi uliyopita nilinunua application kupita MICROSOFT Store kwa kiasi cha $15, inaonekana kulikua na tatizo kwenye mfumo wa malipo na kupelekea muamala ya $15 kufanyika mara nne, tena ingewezekana kufanyika mara nyingi zaidi kama nisingewahi kuizuia kadi.

Sasa Microsoft wanasema kati ya miamala minne ni mmoja tu ambao umewafikia, nawakashauri ni wasiliane na benki yangu kuhusu miamala mitatu ambayo haikufanikiwa na wakanipa reference namba 3.

Sasa nimewasiliana na hawa ndugu zangu Tigo kwa njia ya simu kisa kwenda kwenye moja ya duka lao, wanakazana kuwa miamala yote minne ilienda ("Posted"), wamegoma kusoma barua pepe niliyotumiwa kutoka Microsoft, wamegoma mimi kuwaunganisha ("CC") katika barua pepe ambayo nimetumiwa na Microsoft. Pia wamenipa printout ya hizo transaction lakini wamegoma kutumia makaratasi ambayo yapo branded, yani kwa lugha nyepesi wameprint tables kwenye makaratasi ya kawaida ambapo hamna details ambazo zinasema kilichoprintiwa kimetoka wapi. Sasa wanategemea mimi nishare haya makaratasi na hawa wajamaa, dah.

Kwa ufupi hili ni funzo nimelipata, na imani na wewe utakua umejifunza kitu kipya.

N.B: Kunamdau anaweza sema ningeamisha hela kwenda namba kabla sijafanya huo muamala.
1. Hii sio practical kwa sababu itahitaji niwe na namba zaidi ya moja, pia kila unapoamisha kuna makato yasiyo na kichwa wala mguu.
2. Baada ya kuamisha unaweza kupokea muamala kutoka kwa mtu na kuifanya accounti yako kuwa na hela za ziada.
3. Kama ni subscription, huu ujinga unaweza kufanyika usiku wakati umelala, na kujikuta unaamka asubuhi message za Tigo pesa zinaongozana.

Umepokea TSH milioni XX kutoka kwa ZZZZZ
Malipo yamefanikwa, umelipa TTT kwenda GGG salio lako jipya .....
Malipo yamefanikwa, umelipa TTT kwenda GGG salio lako jipya .....
Malipo yamefanikwa, umelipa TTT kwenda GGG salio lako jipya .....
Malipo yamefanikwa, umelipa TTT kwenda GGG salio lako jipya 0


Asante
 
Pole sana kwa madhila haya, makampuni yetu huwa hawathamini kabisa thamani ya shilingi ya "mteja"!!

Hii ni kwa sababu hata Watanzania wenyewe hatujui haki zetu na ikitokea umezijua haki zako unapodai wataibuka watu kukuponda kana kwamba unachofanya si sawa!! Inaumiza sana

Kwanini wasikuprintie kwenye headed paper, means hizi kesi ni nyingi kwao na wamegundua njia hiyo kukwepa jukumu la kuwajibika!! Watakataa siyo karatasi yao ukitaka kuwawajibisha
 
Pole sana kwa madhila haya, makampuni yetu huwa hawathamini kabisa thamani ya shilingi ya "mteja"!!

Hii ni kwa sababu hata Watanzania wenyewe hatujui haki zetu na ikitokea umezijua haki zako unapodai wataibuka watu kukuponda kana kwamba unachofanya si sawa!! Inaumiza sana

Kwanini wasikuprintie kwenye headed paper, means hizi kesi ni nyingi kwao na wamegundua njia hiyo kukwepa jukumu la kuwajibika!! Watakataa siyo karatasi yao ukitaka kuwawajibisha
Hakika mkuu, hii imenishangaza sana.
Sijajua ni taasisi ipi inahusika kwenye kusimamia haya maswala, ila pia sidhani kama hiyo taasisi husika itakua interested pia.
 
Mpesa MasterCard wako vizuri, bora kutumia hiyo

Kumbe ipo tofauti na MPesa Visa card. Wao iyo virtual card unaiwekea hela then ndio unafanya malipo. Nadhani iyo inafanya maokoto kuwa salama zaidi.
Kwa kawaida huwa natumia ya hawa watu, sijawahi kukutana na hii kitu iliyonipata kwa hawa ndugu zangu.
Kiherehere cha kujaribu service mpya kimenifunza kitu kipya.
 
Back
Top Bottom