Usinipite mwokozi, Unisikie

James Hadley Chase

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
1,576
2,664
"Usinipite mwokozi, Unisikie,
Unapozuru wengine, usinipite.
"Yesu, Yesu! Unisikie,
Unapozuru wengine, usinipite.."
______________________________________
Ni wimbo ulioandikwa mwaka 1868 na mwanamama Fanny Crosby, aliyezaliwa katika kijiji cha Brewster huko New York, Marekani.

Wimbo huu umetiwa sauti 'melody' na William H. Doane mnamo mwaka 1870. Ni wimbo namba 10 katika kitabu cha Tenzi za Rohoni

Maudhui ya wimbo huu yametokana na kisa cha kwenye biblia kinachomuhusu 'ombaomba kipofu' ambaye mara baada ya kusikia umati wa watu ukipita aliuliza “Kuna nini?” Wakamwambia, “Yesu wa Nazareti anapita.”

Ndipo akapaza sauti akisema, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!” Wale watu waliotangulia wakamkemea wakimwambia anyamaze; lakini yeye akazidi kupaza sauti: “Mwana wa Daudi, nihurumie!”

Yesu alisimama, akaamuru wamlete mbele yake. Yule kipofu alipofika karibu, Yesu akamwuliza, “Unataka nikufanyie nini?” Naye akamjibu, “Bwana, naomba nipate kuona.” Yesu akamwambia, “Ona! Imani yako imekuponya.”

Fanny Crosby ni kipofu. Alipata upofu angali mtoto mchanga. Licha ya upofu wake, alipata kuandika nyimbo zaidi ya 8000 zikiwemo 1000 zisizo za dini.

Alilelewa katika misingi ya dini. Akiwa na miaka 10, alibarikiwa uwezo wa kukariri sura 4 za biblia kila siku. Akiwa na umri wa miaka 15, alikuwa amekariri 'torati' (vitabu vitano vya mwanzo katika biblia) pia alikuwa amekariri vitabu vyote vya injili (mathayo, luka, marko na Yohana). Vilevile alikuwa amekariri kitabu cha wimbo uliobora, Methali, na baadhi ya zaburi.

Crosby alifariki mwaka 1915 akiwa na umri wa miaka 94.

©KichwaKikuu
 
Nimeimba sana huu wimbo nikiwa mdogo sababu nimekulia kwa mjomba wangu ambae ni mchungaji hadi sasa. Ilikua kila siku jioni kabla ya kulala lazima watoto tuimbe tenzi za rohoni.

Miaka mingi imepita toka niachane na masuala ya dini lakini bado huu wimbo naweza kuuimba hadi mwisho.

Mwisho, dini ni utapeli kama utapeli mwingine. Mungu wa kwenye biblia ama quran hayupo.
 
Nimeimba sana huu wimbo nikiwa mdogo sababu nimekulia kwa mjomba wangu ambae ni mchungaji hadi sasa. Ilikua kila siku jioni kabla ya kulala lazima watoto tuimbe tenzi za rohoni.

Miaka mingi imepita toka niachane na masuala ya dini lakini bado huu wimbo naweza kuuimba hadi mwisho.

Mwisho, dini ni utapeli kama utapeli mwingine. Mungu wa kwenye biblia ama quran hayupo.
Evil Genius!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom