Usimchukie mumeo kwa kuwa hajaokoka!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,650
Hata kama huko ibadani wenzio wanakushangaa kwa nini unaenda kusali peke yako, fahamu kuwa suala la imani ni la kibinafsi zaidi na kwenda kwako mbinguni kutategemea na matendo yako.

Kuna mdada amekuwa akimshinikiza mumewe aokoke kama yeye, lakini mume amekuwa hataki kufanya hivyo na kuamua aendelee kuwa ktk imani yake ya awali waliyokuwanayo awali kabla ya mke kuokoka. Sasa mke anajisikia vibaya kuona anaishi na mume ambaye sio mlokole na inaonekana kuna shinikizo toka kwa waumini wenzake kuhusu hilo.

Hali hiyo imeanza kupelekea mume kuona nyumba yake kuwa kama 'jela' kwani mke anaona kama anaishi na shetani, na mume anaona kero muda wote kuimbiwa wimbo wa kuokoka na mkewe.

Hali hiii imemfanya mume kuachelewa kurudi nyumbani ili muda uende akirudi akute usiku umeenda na mke kalala walau amani iwepo na makelele yapungue. Ukiangalia hapo ni kama ndoa inaelekea kuanza kuharibika maana 'akili' za wanaume huwa hazichelewi.

Angalizo: Kina mama ni kweli nyinyi ni wepesi kujifunza na kutenda yale yanayowapa furaha moyoni. Kuweni makini na ndoa zenu, msisumbue waume zenu kisa eti hawajaokoka. "Mwanamke mpumbavu huivunja 'nyumba' yake kwa mikonoye".
 
Sometimes kuokoka is so overrated! Na chakusikitisha ni kua walokole walo wengi hutumia nguvu kumlazimisha mtu... Mtu anakupa nene la Mungu leo na leo hio hio anategemea uanze kuenda ibadani.

Imani hasa ya Dini inajengwa.... taratiiibu mpaka inamuingia mhusika na kujikuta kua nae ataka aandamane na walo okoka. Na that applies to both religion.

BTW "hate the sin, love the sinner" - Mahatma Gandhi
 
Well and aptly put!
 
mwake madam!
 
huyo mke nae sio mzima...
utamchukiaje mtu kwa sababu hajaokoka?
tena mumeo??!!!!!!!!!!!!!!
kwani wokovu ni chuki? kwenye wokovu kuna upendo na amani
unless wachungaji wanatafuta waumini kwa nguvu.....

hata hivyo mwanamk mpumbavu hubomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe, mwache aibomoe....
 
lol....jaman kila m2 atampokea mungu muda na wakat wake, ss hw comes uanze kumlazimisha mwenzio.
siku yake bado ikifika bila purukushani ataokoka 2.
huyo mkewe ni wale walokole waliochanganyikiwa labda loh.
maana kuna walokole wengine wamekuwa keroo kwa wenzao jaman.
imani yangu itaniponya.... INATOSHA.
 
huyo dada bado hajaiva katika mafundisho maana kuna neno linasema kama ndugu ana mme/mke ambaye hajaamini na anakubali kukaa na weye asimwache kwani mtu huyo anaweza kukombolewa kupitia kwako.
ushauri.mwanamke unatakiwa ufanye mabo mazuri na umuombee mumeo yeye mwenyewe ana admire na anaanza kukwambi "Twende kanisani kwenu leo"
 
Nimeipenda sn hii kitu uliyoandika NDYOKO,
Yani kuna mhusika lzm nikirudi hm nimfungulie asome na maoni ya wachangiaji,
Yani km ataelewa kilichoandikwa humu ndoa yake itapona,
Kwan amefikia kuhama chumban kwa ugomvi wa mumewe hajawa tayari kuokoka,
Kuna watu ni mabingwa wa kukomlpikate huu wokovu mpaka unawapelekea kujitia dhambin bila kujua,
Asante sana Ndyoko.
 
Imeandikwa;"Na mwanamke ambae ana mume asieamini,na mume huyo anakubali kukaanae,asimwache mumewe,Kwa maana yule mume hutakaswa katika mkewe.....Kama sivyo watoto wenu wangekua si saf,bali sasa ni watakatifu.1Kor 7:13-14.Mwambie huyo mwanamke afuatilie hayo maandiko!
 
Nimeipenda sn hii kitu uliyoandika NDYOKO,
Yani kuna mhusika lzm nikirudi hm nimfungulie asome na maoni ya wachangiaji,
Yani km ataelewa kilichoandikwa humu ndoa yake itapona,
Kwan amefikia kuhama chumban kwa ugomvi wa mumewe hajawa tayari kuokoka,
Kuna watu ni mabingwa wa kukomlpikate huu wokovu mpaka unawapelekea kujitia dhambin bila kujua,
Asante sana Ndyoko.

Huwa sielewi iweje wokovu ukufanye uone dunia nzima ni wadhambi, uliye sahihi ni wewe tu kwa ajili ya wokovu wako. Mi ndo maana mtu akishaniambia mlokole natafuta namna nzuri ya kumuepuka maana najua akili mwake haoni tofauti kati yangu na kitimoto au mdudu mwingine yeyote mbaya!

Duniani kuna vituko sana, hawa wachungaji hawa wanaipeleka dunia mchomo kabisa! Na hili liko sana kwa kina mama, sijui kwanini! Ni wepesi kweli kugeuka utadhani kinyonga na rangi zake!
 
Wee Ndyoko wee!Nani kakuambia kiti moto a.k.a mkuu wa meza ni mdudu mbaya?
 
Na ukisema nawe, ingawa sio mlokole, umpe neno atakavyokuangalia kwa dharau utadhani yeye ndo YESU halisi.
 
Wee Ndyoko wee!Nani kakuambia kiti moto a.k.a mkuu wa meza ni mdudu mbaya?

Niko chini ya miguu yako, nisameheee sikujua kuwa nimegusa maslahi binafsi ktk hilo mkuu!
 
Kweli Mungu ni katuumba tofaouti,.....maaake hata mimi namchukia tena sana mwanamke aliyeokoka,...by the way_ hata mimi ni mkristo
 
Huwa sielewi iweje wokovu ukufanye uone dunia nzima ni wadhambi, uliye sahihi ni wewe tu kwa ajili ya wokovu wako. Mi ndo maana mtu akishaniambia mlokole natafuta namna nzuri ya kumuepuka maana najua akili mwake haoni tofauti kati yangu na kitimoto au mdudu mwingine yeyote mbaya!

Duniani kuna vituko sana, hawa wachungaji hawa wanaipeleka dunia mchomo kabisa! Na hili liko sana kwa kina mama, sijui kwanini! Ni wepesi kweli kugeuka utadhani kinyonga na rangi zake!
Na aina ya makanisa na wachungaji wao nayo inachangia kupotosha watu,
Yani utadhani wao wanasalimiana na yesu kwa kushikana mikono naye!
Japo huyu mhusika ni mbishi kwa hili simwachi nitamlainisha mpaka akubali kusoma na ubishi wake wote,
Yani imefika mahali mmewe anakunywa pombe na kurudi usiku sana wakati wala alikuwa hanywi,akirudi mapema mkewe akianza ibada yake hapo mzuka unampanda mpaka anatoka nje akikemea bila hata kujijua na hapo mpaka apoe ni masaa alafu kila anachokemea ni kuhusu dhambi za mmewe na mambo chungu nzima,
Leo nimezamiria kumsalimia kwa salam ya bwana asifiwe mtumishi wa mungu ndio tuanze maongezi.
 
Imani za kudandia kama daladala, upotofu mtupu. Kibaya zaidi, analazimisha kuwapotosha na wengine. Hizi biashara zingine loooh!
 
Na aina ya makanisa na wachungaji wao nayo inachangia kupotosha watu,
Yani utadhani wao wanasalimiana na yesu kwa kushikana mikono naye!
Japo huyu mhusika ni mbishi kwa hili simwachi nitamlainisha mpaka akubali kusoma na ubishi wake wote,
Yani imefika mahali mmewe anakunywa pombe na kurudi usiku sana wakati wala alikuwa hanywi,akirudi mapema mkewe akianza ibada yake hapo mzuka unampanda mpaka anatoka nje akikemea bila hata kujijua na hapo mpaka apoe ni masaa alafu kila anachokemea ni kuhusu dhambi za mmewe na mambo chungu nzima,
Leo nimezamiria kumsalimia kwa salam ya bwana asifiwe mtumishi wa mungu ndio tuanze maongezi.

Usishangae ukatolewa baruti nawe pia. Unajua wengine kwenye huu ulokole ni kama wameegesha tu, wanasilkiliza mtu anavyomuabisha mumewe...........mara sijui mzinzi, mlevi na mengine mengi.......masikini kesho waumini wanamuona huyo mume aliyetolewa ushuhuda wa dhambi, yaani aibu tupu sema tu mume anakuwa hajui alivyoongelewa na mkewe huko kanisani. Kifupi ni kuaibishana tupu!

Slowly this is becoming a social problem in the country!
 
Back
Top Bottom