Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,900
- 944
USIKU KAMA MCHANA!, RUHORO AGAWA TV BUNGE LA KAHAWA - NGARA
Mbunge wa Jimbo la Ngara Mh. Ndaisaba George Ruhoro anapenda kuujulisha umma na Wananchi wa Jimbo la Ngara kuwa anaendelea na Zoezi la ugawaji wa Television (TV) kwenye vijiwe/mabunge ya kahawa yaliyopo Wilayani Ngara.
Lengo kubwa ni kuwawezesha Wananchi kupata taarifa za Mambo mbali mbali yanayoendelea Duniani na Nchini, pamoja na kuwafanya waone kazi kubwa inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan .
Kwa sasa Mbunge wetu amegawa TV Kwenye Kijiwe cha Kahawa Ngara mjini na muda si mrefu atagawa Rulenge, Junction na Benaco.
TV itafanya watu wengi kuvijua vijiwe vya kahawa, Kuhudhuria vikao vya kujadili mambo mbali mbali ya Maendeleo na kubwa kuliko yote, kuwafanya Watanzania kuanza kunywa Kahawa ambayo wanaizalisha wenyewe na hivyo kutengeneza soko la Ndani la wanywaji wa Kahawa.
Mbunge wa Wanangara hapoi, hategemei kupoa, kasi ni ileile. Watu wanaseme “ KEEP" BOMBING ”