Usikate tamaa baada ya kushindwa mara moja

Tony Laurent

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
4,726
5,442
Thomas Edison ndiye alivumbua balbu za umeme tunazotumia leo. Lakini kabla hajafikia hayo mafanikio ya kuifanya balbu itoe mwanga, alifanya majaribio zaidi ya 2000 (elfu mbili). Siku moja mwandishi wa habari alimuuliza jinsi alivyokuwa anajisikia baada ya kushindwa maranyingi kiasi kile; Naye alijibu,

" I never failed once, Invented the light bulb. It just happened to be a 2000 step process"

Hivyo unaweza kuona kwamba mafanikio hayaji mara moja tu, wakati mwingine inaweza kuchukua muda mrefu sana mpaka uje kufikia mafanikio uliyokuwa unatarajia katika maisha yako. Ukishindwa mara ya kwanza jaribu tena na tena mpaka uone mafanikio. Kukata tamaa ni miongoni mwa mambo mabaya kabisa kuyafanya katika maisha.
 
Back
Top Bottom