Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 178,275
- 1,077,680
Kitabu hiki ni kizuri. Mimi binafsi kilinisaidia katika interview yangu ya tatu baada ya kuwa nimeboronga katika interview zangu mbili za kwanza. Ndiyo nilikuwa nimemaliza chuo na kazi ya kwanza ndiyo hasa niliitaka lakini nilikutana na vijana wenzangu kutoka Kenya na Nigeria nikajua tu waziwazi kuwa hapa sitoboi maana wenzangu walikuwa wamejiandaa kweli kweli. Baada ya kusoma kitabu hiki nilipata picha halisi ya ninachotakiwa kufanya katika interview yangu ya tatu na nilikwenda kwa kujiamini sana maana nilikuwa nimejua mambo ya msingi. Mifano ya majibu ya maswali ya kawaida yanayoulizwa katika interview nyingi yaliyomo kwenye kitabu hiki pia yalinisaidia sana. Na nilipata hiyo kazi!
Najua ukiritimba uliopo katika ajira hapa kwetu. Kuna mambo ya kujuana (nepotism), rushwa (za kila aina) na connection. Pamoja na yote haya naamini utafaidika na yaliyomo katika kitabu hiki katika ujumla wake. Na watakaofaidika zaidi ni wale watakaoomba kazi katika mashirika ya kimataifa ambako pengine mambo ya kujuana, rushwa na connection hayana nafasi kubwa sana kama huku kwingine. Usiende huko tu kichwa kichwa. Soma kitabu hiki kwa uangalifu. Zingatia yale mambo ya msingi. Jiamini na mengine mwachie Mungu!
Nitaongezea na vingine viwili au vitatu hivi vyenye mitazamo tofauti tofauti huko mbele ya safari. Kila la heri kwa vijana mnaotafuta kazi. Kama kitabu hiki kitamsaidia japo kijana mmoja kwa namna moja au nyingine kupata kazi basi, lengo langu litakuwa limekamilika. Endeleeni kupambana kwa kadri inavyowekana na kamwe msikate tamaa. Ndivyo maisha yalivyo!