Ushuhuda: Wauzaji wa Trekta Afrika Kusini

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,245
103,948
Hodi huku
Kumekuwa na nyuzi humu zikijadili uimara wa trekhlta zinazouzwa mitandaoni South Afrika. Uimara huo umekuwa ukitiliwa mashaka kulinganisha na bei ya trekta hizo. Ukiingia kwenye mitandao mingi utagundua bei ya trekta zilizotumika muda mfupi zikiuzwa mpaka milioni 15.

Achana na stori za mitandao na simulizi. Mwanenu huwa sikubali kushindwa nilifunga safari mwenyewe mpaka South. Twende taratibu nikupe udondozi wa shuhuda.

TRA na TBS
Kabla ya chochote nikaingia TBS kujua taratibu na gharama za ukaguzi.Nikamuonyesa msela picha kadha wa kadha ili anipe ABC. Kwanza akanipa hongera kichizi,akanitakia kila la kheri niingize chombo nizalishe chakula watu wale washibe. Akaniambia gharama ni laki 3 mpaka laki 4 na kazi inafanywa na NIT. Taratibu ni kwamba kama kutakuwa na hitilafu wataandika ripoti nirekebishe.

Baada ya hapo nikaendesha ndinga mpaka TRA waniambie ushuru ukoje, sio nilete chombo halafu kipigwe mnada. Jamaa akaniambia hakuna kodi kwenye trekta ila kuna ushuru kidogo tu nitalipa kama 0.6% na 1.6% ya bei. Nikampa invoice mbili tatu za wauzaji wa South zenye around 15m mpaka 20m tukaona haizidi laki 5.

Nikaona usinichezee,moja kwa moja nikaenda kupima Covid 19 tayari kwa kusafiri.

South Africa
Kabla sijaondoka nilikuwa na sample ya sellers kama 5 hivi ikiwemo niliopewa link na wadau humu. Watatu nikiwa na invoice zao tayari. Muda mwingi walikuwa wananipiga sound nilipe tu wanitumie mzigo. Sikuwa napepesa macho niliwaambia siwezi kuwa fala,nakuja mwenyewe kuangalia chombo nitafute fundi akague ndio nilipe. Mara oooh invoice ita expiry,nawaambia utaandika nyingine kwani shida iko wapi.

Moja kwa moja nikadondoka Cape Town ambapo ilionekana wauzaji wengi wapo kule. Nikaanza na wa kwanza ambaye mzigo wake ulinivutia sana. Nikampigia simu ku book appointment kesho asubuhi namtimbia. Akaniambia wamefunga wamehamia Pritoria. 🤣🤣 nikamwambia kwa kizungu we ni tapeli? Tumewasiliana kila siku unasema upo Cape Town,adress yenu inasoma Cape Town. Hakujibu.

Nikamcheki wa pili. Huyu adress ilikuwa na geogle location. Nikachukua uber kufika hapo hola kuna malls tu wala hawatambuliki. Kuulizia naambia wewe ni mtu wa 3 leo anaulizia hao jamaa.

Siku ikakata ikabidi nijisalimishe kwa mwanangu mmoja huku bongo aliwahi kuishi South miaka ya 2000s. Akaniunganisha na muhuni mmoja hivi mbongo. Sasa yule ndio akanipeleka kwa wenyewe kabisa.

Uhalisia
Hatimaye nikafika kwa wauzaji halisi wa trekta mpya na used. Kiukweli bei tunazodanganyana humu ni bei za matapeli tu. Lakini uhalisia ni tofauti na hakuna tofauti kuuubwa na bei za kina Chriss Lukosi na wauzaji wengine. Japo kwa mtu mwenye muda wa kutosha anaweza kupata trekta lililotumika mwaka hadi miwili kwa bei ya 30m.

Nikafanikiwa kupata trekta New Holland kali sana TT75 kwa 29m. Ngoma ikiwa kwenye muda wa kusafirisha ungepishana na msimu wa mvua. Kusafirisha kwa meli ambayo ni nafuu inachukua 14 mpaka 21days. Nikaona isiwe tabu hii milioni 2 ikipotea sio issue sana ngoja nikakomae tu huko huko. By the way nimekula bata na pisi mbili huko sio haba

Baada ya kurudi Tz nikapambana tena nikapata Case HP 75 4WD kwa 39.5m kwa mwarabu mmoja hivi.

Nitakuja kuhitimisha baadae,ngoja nitafute vibarua huku Iramba.

sikufahamu kama Singida kuna fursa nyingi aisee. kumenishawishi mpaka nitafute New holland kama trekta ya pili
Mkuu chukua Ford 7610 kwa 35 na 6610 kwa 35M

sikufahamu kama Singida kuna fursa nyingi aisee. kumenishawishi mpaka nitafute New holland kama trekta ya pili

Singida na Songea walishaachana na jembe la mkono kitambo, tofauti na mikoa ya kagera, kigoma, katavi, geita, ambako jembe limetawala japo ni wazalishaji wakubwa then faida utahopata hapo wewe nunua mbolea kipindi haihitajiki sana kwa bei nafuu then weka stock halafu kwenye high season utaiuza mara mbili yake hata uwe na tani elfu ngapi singida zitaisha, kwenye mavuno tafuta vimashine vya kuhamisika vya diesel au petrol vya kupukuchulia mahindi ukomae singida hapo hapo anzia sekenke, sheliu nenda kwa akina mwigulu makunda kule njoo vuruga maluga na Tumuli hadi iguguno huko utoboe misuna wanamaliza kuvuna umepata pesa ya kutosha kwenye kupukuchua mahindi kikubwa uwe na vijana walio faster unapanga tu leo kambi kijiji fulani kesho sehemu nyingine utajiona boya kuchelewa kwenda singida
 
Mkuu chukua Ford 7610 kwa 35 na 6610 kwa 35M

Mkuu nimeshachukua Case tayari ipo kazini. Asante kwa kushea
 
Singida na Songea walishaachana na jembe la mkono kitambo, tofauti na mikoa ya kagera, kigoma, katavi, geita, ambako jembe limetawala japo ni wazalishaji wakubwa then faida utahopata hapo wewe nunua mbolea kipindi haihitajiki sana kwa bei nafuu then weka stock halafu kwenye high season utaiuza mara mbili yake hata uwe na tani elfu ngapi singida zitaisha, kwenye mavuno tafuta vimashine vya kuhamisika vya diesel au petrol vya kupukuchulia mahindi ukomae singida hapo hapo anzia sekenke, sheliu nenda kwa akina mwigulu makunda kule njoo vuruga maluga na Tumuli hadi iguguno huko utoboe misuna wanamaliza kuvuna umepata pesa ya kutosha kwenye kupukuchua mahindi kikubwa uwe na vijana walio faster unapanga tu leo kambi kijiji fulani kesho sehemu nyingine utajiona boya kuchelewa kwenda singida
Safi sana mkuu Arovera kwa kunionyesha machaka
 
Back
Top Bottom