Ushuhuda wa Mjumbe wa Bunge la Katiba

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=1]
IMG_3875.jpg
[/h] BI SALMA SAIDI

Ningependa niandike simulizi za siku chache kabla ya upigaji kura namna ambavyo hali ngumu ilivyotukabili sisi watu saba ambao tuliamua kupiga kura ya hapana tena ya wazi, jinsi Wazanzibari wenzetu walivyotuchukulia kwa mtazamo tofauti kutoka nyumbani Zanzibar baadhi ya vijana walichapisha vipeperushi na kuvisambaza kwenye mitandao ya kijamii wakitutaka turudi nyumbani na kutuita wasaliti.

Kwa upande wa Wazanzibari wenzetu waliokuwepo Dodoma nao walitupa vitisho vya kila namna tu, maana haikuwa kutushawishi tu bali mambo yalizidi na kuzidi mpaka hadi wengine wakitwambia tukipiga kura ya hapana tutakiona cha moto.

Baada ya kuonekana wapo ambao watapiga kura za hapana lugha iliyokuwa ikitumika miongoni mwa wenzetu wa Chama Cha Mapinduzi, wakisema kwamba kuna watu wanataka kuharibu mchakato wa Katiba iliyopendekezwa katika dakika za mwisho, lakini waliapa kwenda na sisi iwapo hatutalegeza misimamo yetu ya kuikataa rasimu hiyo.

Siyo kazi rahisi kama wengi wanavyodhani kama ambavyo haikuwa wepesi kwa Ukawa kurejea bungeni, halikadhalika ugumu ulikuwepo kwa waliokuwepo ndani kutoka nje, ambapo wengine tuliamini kwamba hata maamuzi ya watu kutoka bungeni kwa wakati huo wangetoka watu wachache tena wale ambao wana msimamo madhubuti. Lakini kwa wale waoga wangebaki na kurahisisha mafanikio ya kupatikana theluthi mbili kirahisi, kutokana na hofu iliyokuwa imetanda.

Baadhi ya wajumbe kutoka Zanzibar hasa wale wa kundi la 201, walikuwa wana msimamo wa kuikataa rasimu yote na ndiyo maana kiukweli taarifa za ndani zinasema waliopiga kura za hapana rasimu nzima walikuwa ni wajumbe sita kati ya waliopiga kura za siri, na baadhi yao walikuwa wamekataa baadhi ya ibara tu za rasimu hizo. (Takwimu kamili tunazo).

Naamini kwamba walikuwa wana nia njema ya kuikwamisha rasimu hii kwa kuwa haina maslahi na Zanzibar, hata hao waliokuwa serikalini wakiwemo baadhi ya mawaziri. Lakini walikuwa hawataki kuonekana wabaya na wao ndiyo kikwazo.
Hata hivyo wanaamini katiba hii haina maslahi lakini kwa kuwa wameshurutishwa na misimamo ya chama ambapo baadhi yao wengine waliendekeza hofu zao za kupiga kura ya siri wakiamini kwamba siri zao zitalindwa.

Binafsi nilishaona mapema harakati zilivyokuwa zikiendelea namna gani wajumbe wakitushawishi tupige kura ya siri nikajua hapa kuna namna fulani ya kuibiwa kura zetu na ndipo nikawashauri wenzangu wachache tupigeni kura za wazi ila kwa wale ambao hawakutaka hatukuwa na namna ya kuwabadilisha walikuwa huru na wakapiga kura zao za siri ambazo zilistiriwa na zilisitirika kwa usiri wake. Mimi nasema kusudi haiambiwi pole na walichokipanda ndiyo walichokichuma.

Mimi kwa upande wangu sikuona kama nimefanya makosa kama ambavyo wengi wananichukulia kuwa nimewashawishi wenzangu kuikataa rasimu, lakini najiuliza kwa nini iwe kosa mimi kushawishi kuikataa na isiwe kosa kwa wale wengine ambao walitushawishi kuikubali?.

Wapo ambao kutokana na uzalendo wao walitutaka tutoke kwa maana ya kususia Bunge, lakini mimi binafsi nilikataa kwa kuwa niliamini kuwa nina maamuzi yangu binafsi na siko tayari kuchukua ushauri kutoka popote kwa kuwa niliamini sijatumwa na chama cha siasa, wala kikundi cha dini wala taasisi yoyote zaidi ya Jumuiya yangu ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA) ambao kimsingi walinishauri tokea kuanza kwa mchakato huo wa Bunge nibaki ndani na nitetee nikiwa ndani kwa hivyo nisingeweza kwenda kinyume.

Binafsi nilikuwa naamini naweza kuizuwia theluthi mbili nikiwa ndani ya Bunge na hamu yangu ilikuwa niweke rekodi ili vijukuu vyangu vije kusoma kuwa Salma Said alipiga kura ya HAPANA kwa rasimu hii ya katiba, kimsingi sikuwa nakubaliana nayo tokea kuanza kwa majadiliano ambayo yaliondosha sura ya kwanza na sura ya sita ambazo ndiyo hasa kiini na roho ya katiba hii.

Mimi nimetoka Zanzibar kwa ajili ya kusimamia maslahi ya Zanzibar na kiapo changu moyoni kilibeba dhana hiyo kwa hivyo sikutaka kujizonga, kwani niliamini ndani ya moyo wangu nje ya maslahi ya Zanzibar katiba hii ni mwiba mchungu kwangu na ndiyo maana natoa ‘challenges’ ili watu wafuatilie ‘hansards’ (kumbukumbu rasmi za mijadala ya Bunge).

Huko wataona kama kuna mchango wangu katika kamati kwa kuwa nilikuwa nikiamini kuwa siri yangu moyoni ni siri ya kura yangu ya hapana, baada ya majadiliano ya ndani ya kamati mwisho wa mchakato mzima kule bungeni, na siyo kwenye kamati niliamini ndani ya kamati hakuna nitakachopendekeza kitakachozingatiwa na hayo ambayo wenzangu wakiyasema hayakuwa yakizingatiwa, kwahivyo niliamini sina sababu ya kuongea chochote ila niwe na siri ya maamuzi yangu moyoni.

Wajumbe Waliopiga kura ya Hapana
1.Adil Mohammed Ali (Walemavu)
2.Alley Soud Nassor (Taasisi za Elimu)
3.Ali Omar Juma (Vyama vya siasa)
4.Jamila Abeid Saleh (Vyama vya siasa)
5.Salma Hamoud Said (Taasisi zisizo za kiseri kali)
6.Mwanaidi Othman Tahir (Vyama vya siasa)
7.Fatma Mohammed Hassan (Taasisi za dini)

Wakati mchakato ukiendelea wajumbe saba waliamua kuondoka Dodoma kutokana na dharau, matusi machafu na ya nguoni, vitisho walivyokuwa wakivipata kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa CCM, hawakujifanya tu kuwa wao ndiyo wengi bali walijifanya wao ni wenye nguvu, wao ndiyo wenye maamuzi ya wenzao kwa kisingizio cha kuwa na dola eti, wao ni wenye uwezo wa kufanya chochote katika katiba hii kutokana na kauli zao walizokuwa wakituambia.

Lakini pia ningependa niandike namna gani Wazanzibari walivyotumika kufanyiana uadui wenyewe kwa wenyewe, kuonyeshana ubabe, dharau, matusi ya nguoni na kebehi na vijembe kutokana na kuwa na mitazamo tofauti wakati wenziwao wa Tanzania Bara wakikaa pamoja.

“Hii Katiba itapita mtake msitake, hii katiba nyinyi hata mkipiga hapana nyote mliopo ndani ya ukumbi huu, mjue tu kwamba tutaipitisha mnacheza na wana CCM nyie hii ndiyo chama dume hiki ndiyo chama chenye uwezo, hiki ndiyo chama tawala …” ni maneno ya mmoja wa viongozi wa ngazi za juu wa CCM upande wa Zanzibar.

Kauli kama hizo pia zikitolewa na kiongozi mwingine wa kitaifa wa moja ya jumuiya za CCM, akishirikiana na wana-CCM wenzake waliondoka katika nafasi zao bungeni, na kuja pale tulipokaa sisi na kuunga mkono kauli ya mwenzao wakitudhihaki kwa uamuzi wetu wa kupiga kura ya hapana kwa kutuita ni watu wajinga na ni watu tunaotumiwa na watu ambao tunaongozwa na kuburuzwa. “ Hamtaki hata haki ya kuishi, hata mtu kuishi hataki basi kila kitu hapana hapana tu,” ni moja ya kauli yao.

“Wajinga wana mji wao tutawaonyesha, hawa wanaosema hapana ni watu wenye kutumiwa na wakoloni, wanatumiwa na waarabu na wengine hapa wala siyo kwao kwao ni Oman, lakini hii katiba itapita mtake msitake hizo kura zenu za hapana ni bure tu,” alisema mbunge wa CCM ambaye akiwa na wenzake walihama kwenye viti vyao na kuja tulipokaa sisi.

Mbunge wa CCM kutoka Zanzibar akiwa na wenzake walioniomba nipige kura ya NDIYO, mmoja wao aliniuliza iwapo hatujaona jambo zuri hata moja katika rasimu iliyopendekezwa hata tupige kura ya HAPANA, lakini jibu letu lilikuwa rahisi, “je, nyinyi mliopiga NDIYO, basi hakuna baya hata moja ambalo limewachukiza hata muamue kupiga NDIYO rasimu nzima?.

Kwa ufupi baadhi ya wana CCM walitoka sehemu zao walizokaa na kuja katika sehemu zetu kuja kutufanyia fujo kwa maneno ya dharau na kebehi, huku wakitumia lugha za udhalilishaji ili kuturudisha nyuma na kutaka tupoteze muelekeo ili tukubali kwa kupiga kura za NDIYO ili katiba iliyopendekezwa ipite bila ya matatizo.

Kutokana na katiba iliyopendekezwa kuonekana imelalia sana upande wa Zanzibar, wapo baadhi ya wawakilishi na wabunge wa CCM waliokuwa wakisema potelea mbali wapoteze majimbo yao lakini nisiipoteze Zanzibar, na walikuwa na hamasa ya kutaka kuvikataa baadhi ya vifungu vya rasimu wakisema chama chao kiliwapa muongozo wa kuikataa sura ya kwanza na ya sita tu, lakini hakijatoa muongozo katika sura na ibara nyengine.

“Sisi hatukupewa muongozo wa hizi sura nyIngine tuliopewa muongozo ni sura ya kwanza na sura ya sita, kwa hivyo kwa kuwa rasimu hii haina maslahi ya Zanzibar hatuwezi kuvikubali baadhi ya ibara lazima tuvikatae, ingawa tunajua kwamba tutapoteza nafasi zetu tunapoteza majimbo yetu lakini potelea mbali vizazi vyetu vitakuja kuona kwamba hatujachangia kuizamisha Zanzibar,” Walisema wajumbe hao wa CCM.

Siku ya upigaji kura baadhi ya wajumbe walifurahi kutokana na kauli ya William Lukuvi ya kuwa kila mmoja ana msimamo wake wa kupiga kura amma ya wazi au ya siri, hivyo wengi wao iliwapa fursa ya kuamua watakavyo.
“Lukuvi tayari ameshasema kuwa tutapiga kura tutakavyo mtu asiamuliwe kila mmoja achague, akitaka kupiga kura ya wazi au ya siri na nikisema Lukuvi basi ujue huo ni msimamo wa PM (Pinda) mimi kura yangu nitapiga ya siri, si tumeshaambiwa tupige kura tutakavyo,” aliniambia mjumbe mmoja kutoka CCM.


Lakini mwisho alipiga kura ya wazi na kusema hapana na baada ya kura saba za hapana zilivyoanza kujipanga, kura ya mwisho ya hapana namna ilivyopatikana katika tundu ya sindano kwa mikiki, vitisho, dharau, khofu, kulazimishwa na kutekwa nyara na matusi ya nguoni, lakini pamoja na yote hayo kura saba zilipiga hapana na ndiyo mwisho wa mchezo.




Ni kauli ya mjumbe aliyeshiriki mchakato wote wa Katiba ndani Bunge Maalumu, ikiwemo kuipigia kura rasimu.


Wiki iliyopita shuhuda wa simulizi hii Mwandishi Salma Said, alianza kuelezea yale yaliyojitokeza wakati wa upigaji kura ndani ya lililokuwa Bunge Maalumu la Katiba, ambapo aliishia pale walipoelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) William Lukuvi, kupiga kura watakavyo.



Lakini muda mfupi baada ya mjumbe huyo kueleza kauli hiyo kiliitishwa kikao na kubadilishwa uamuzi huo na ikaamuliwa kura iwe moja tu na ni ya wazi, hivyo baadhi ya wajumbe hasa kutoka Zanzibar na wale wenye kudai Tanganyika wakashindwa kuonyesha misimamo yao hadharani na wakalazimika kupiga kura zao kwa wazi na kukubaliana na maelezo waliopewa.



“Daaah mambo yameshabadilika hivi sasa tunatakiwa tupige kura ya wazi, lakini hii najua ni mbinu ya makusudi ya kututega lakini aaaah,” alisema mjumbe mmoja kati yao ambao walikuwa wana nia ya kukataa baadhi ya ibara.

“Mheshimiwa Salma hii katiba inataka kupitishwa lakini, kwa ufupi haina maslahi na Zanzibar hata kidogo na afadhali ile katiba ya 77 kuliko hii, maana katiba hii itakwenda kuiathiri katiba yetu ya Zanzibar kwa kiasi kikubwa, ikataeni kwani tunaamini nyinyi ndiyo wakombozi wetu sisi tupo nyuma yenu Inshallah maana unajua tena sisi mazingira yetu,” alisema mjumbe mmoja ambaye ni Waziri.



Binafsi namheshimu sana mheshimiwa huyu kutokana na taaluma yake ambayo, sina shaka hata chembe na uzalendo wake na ndiyo maana alithubutu akanikabili na kunieleza wakati wenzake wakiniona kama ni adui wao, ingawa baadhi wanamlaumu kwa nini na yeye asichukue uamuzi mgumu? Wengi hawajamfahamu lakini mimi nimemfahamu sana kutokana na uamuzi wake huo.



Natamani nivute kumbumbuku pale dakika chache kabla ya kura ya hapana siku ya kwanza ambayo alianza kupiga Adil Mohammed Ali akiongozwa na Aley Soud na kufuatiwa na Ali Omar, kisha kuja Fatma Mohammed na kisha Jamila Abeid na baadaye mimi na hatimaye kura ya mwisho ambayo ikitarajiwa kupigwa na Mwanaidi Othman, lakini muda mfupi aliondoka na kwenda chooni akitujulisha kwa simu ya mkononi kwamba “Siwezi kupiga kura ya wazi nitapiga kura ya siri” na kisha aliondoka katika sehemu ambayo alikuwa amekaa na kwenda kukaa kwenye kiti, akiwekwa katikati upande mmoja akiwa ameketi Mwana na upande mwengine akiwa ameketi Mahmoud Thabit Kombo.



Lakini mwisho alipiga kura ya wazi na kusema hapana na baada ya kura saba za hapana zilivyoanza kujipanga, kura ya mwisho ya hapana namna ilivyopatikana katika tundu ya sindano kwa mikiki, vitisho, dharau, khofu, kulazimishwa na kutekwa nyara na matusi ya nguoni, lakini pamoja na yote hayo kura saba zilipiga hapana na ndiyo mwisho wa mchezo.



Siku moja baada ya kupiga kura ya hapana kila mmoja wetu alikabiliwa na vitisho na matusi mbalimbali, lakini kila mmoja alisimama imara hadi dakika za mwisho hakuna aliyetetereka na kubadilisha msimamo wake, zaidi ya watu 14 walikuwa na msimamo wa kuikataa rasimu yote lakini kutokana na khofu wakaanza kupungua na kuamua kupiga kura za siri.



Kulikuwa na vikundi vidogo vidogo vikitujadili sisi ambao tumekubali kupiga kura ya wazi na ya hapana kuwa eti sisi siyo wazalendo na nikitangazwa mimi kuwa ndiyo ‘Public Enemy Number One’, lakini hilo katu halikunitia hofu wala kuvunjika moyo kwa kuwa nilijua mambo kama hayo yatanikuta na nilijitayarisha kuyapokea na kuyakabili kwa hali yoyote.



Ingawa wajumbe wengi waliotoka Zanzibar walikuwa wana msimamo kama wetu wa kupiga kura ya hapana kuanzia sura ya kwanza hadi sura ya 19 na ibara zake zote, lakini hawakuwa na uwezo wa kutetea uamuzi wao huo kwa kupiga kura ya wazi kutokana na ushawishi, vitisho na hofu za kuogopa kupoteza kazi zao, nafasi zao na wapo ambao walikuwa wakiona muhali kupiga kura ya wazi kwa sababu tu wamekuwa na maelewano ya karibu na baadhi yao katika kipindi chote cha bunge na baadhi ya wale watu ambao wana mitazamo tofauti.



“Mimi nipo pamoja na nyie lakini kwa kweli nikiri kwamba siwezi kupiga kura ya wazi kwa sababu tumeshakaa na hawa watu na wananiamini sana kwamba mimi ni mwenzao, sasa nikipiga kura ya wazi nitawavunja moyo sana, lakini niamini kwamba mimi sijapokea pesa na hata kama nimepokea nitapiga kura ya hapana,” alisema mmoja wa wajumbe walopiga kura ya siri.
 
nyie wa Zanzibar unafiq na njaa zenu ndio zimewaponza.
Tutaendelea kiwatawala Mpaka utimilifu wa dahali
 
Mh! Katiba na Demokrasia ya kukiuks haki za binadamu.Ningemshauri binti Salma kwenda mahakamani na kuipinga Katiba hii sababu ya kuwa na ushahidi wa hivyo vitisho.
 
Wazanzibar wanalalamika mpk wanatia aibu! Wameamua kuikubali katiba wenyewe wanaanza kulalama! Watanganyika tumechoka na kelele zenu! Mtu mzma unakubali kuiangamiza nchi yako tena waziwazi wananchi wako wanaona eti kisa pesa hadi vizaz vyenu vitawalaani! Acha muendelee kunyonywa na watanganyika hadi miaka mingne50!
 
Hizi ni hekaya za abunwasi. Anajikosha kwa nani sasa na ili iweje, kwa nini hakuyasema hayo kabla hajapiga kura
 
kilichokufanya ubak ndan ni tamaa2 ya fedha na jihesabu kama mtulioshindwa maana kama uko kwenu wasom mnaojua sheria mmeibiwa kura uku kwa mbumbumbu tutaweza kuzuia uchafu hu usipite?
 
Woga wako ndio umeiangamiza nafsi yako na kuitwa msaliti wahedi. Kwa nini ukuwa kama ag@Salma
 
Ningependa ataje na majina kabisa ili tuwajue maharamia kwa majina
 
Ninyi saba,historia ya Zanzibar itawaandika vizuri. Msihofu kwa sababu katiba yao haitapita. Wazanzibari wataikataa. Ni suala la wakati tu.
 
Back
Top Bottom