Ushuhuda wa Dr. H. Mwakyembe

Ame

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
6,194
5,218
Napenda kumshukuru Mungu kwa uaminifu wake katika maisha ya Dr. Mwakyembe. Nami napenda kuungana naye katika kufurahia ushindi wa imani yake na hasa uaminifu wake kwa maelezo yote niliyompatia hapa JF kuwa atoe ushuhuda kwa yale Mungu aliyomtendea ili sifa na utukufu ziwe kwake Mungu katika jina la Yesu bwana na mwokozi wa maisha yetu; ubarikiwe Dr. Mwakyembe na kuanzia pale uliposhuhudia ushuhuda wako hakuna wakuugeuza vinginevyo kwani umemshinda shetani kupitia neno la Mungu katika ufunuo 12:11 And they have defeated him by the blood of the Lamb and by their testimony. And they did not love their lives so much that they were afraid to die....Hukuogopa mtu wala hukujali status yako hata ukasimama kuikiri imani yako...that you did not love your life so much that you were afraid to be condemned, accused or even killed by those who will be condemned by their guilty conscious.....

Yaliyokupata ni promotion katika ulimwengu wa roho kwani sasa kwa hakika utakuwa umemjua Mungu na nguvu zake zaidi kuliko ilivyokuwa mwanzo. Neno la mungu linatuambia kuwa ..John 16:33 "I have told you these things, so that in me you may have peace. In this world you will have trouble. But take heart! I have overcome the world."

Katika maandishi yangu hapa JF niliandika kuwa hiyo hali ya ngozi si kwaajili ya jambo lolote bali ushuhuda kwa wote kuwa yaliyotendwa kweli yalitendwa ili kusiwe na kisingizio kuwa labda walikosea ama haikuingia mwilini na kwakua wengi wameona kwa macho yao na kwakua umediriki kuikiri imani yako hadharani basi acha tuingie hatua ya pili ya muujiza wako kuwa ngozi yako kuanzia siku ile uliposimama kwenye madhabahu ya bwana ilianza kutakata na itakuwa nyororo na laini kama ya mtoto mdogo. Hakuna ambacho ulichokitamani katika maisha yako ambacho utakikosa hasa lile ambalo liliambatana na wewe kupelekea kutaka kuangamizwa. Kwa macho yako utaona maadui zako wakiangamia moja baada ya mwingine wasipodiriki kuungama kwako bila kulazimishwa na mazingira ama nguvu yeyote. Wewe tulia na usubiri kuona uaminifu wa Mungu kwa maana wakati wa Mungu ndiyo ufaao zaidi usiwe na haraka.

Nikatika jina la Yesu naweka huu ushuhuda machoni mwa wa watanzania ili kwa kupitia haya roho nyingi zilizopotea zipate kuponywa...Kupitia ushuhuda huu wa Dr. Mwakyembe kila atakaye mwamini Mungu kwa dogo ama kubwa linalomsumbua katika damu yake apate uponyaji....Sifa na utukufu ni kwa Yesu jina lipitalo majina yote ambalo kwalo wokovu una yeye milele na milele amina.

Mbarikiwe na bwana!
 
Habari za ugonjwa wake na kuhusu ushuhuda wake zipo humu na hasa ndizo zilizoniunganisha mm na yeye japo simfahamu na yeye hanifahamu....

Mimi sielewi kabisa, wewe unazungumza kama mchungaji aliyemuombea Dr Mwakyembe au Mwakyembe mwenyewe?
 
Mkubwa!

Mmmmmhh!
Tuwe humu muda wote tuliokuwepo tusimjue!

Lakini ngoja tuwasubirie wadau jamvini!
Lakini Mi nafikiri hayumo humu!

Hata wewe unaweza kuwa ndiye?kwani nani ajuaye nyuma ya LIVERPOOLFC kuna nani????????? ID ni siri ya mtu na kuna watu wanazo zaidi ya moja...
 
Napita lakini nakuachia maswali Mbona mwakyembe alitibiwa India ...? & Mtoa mada bado sijakuelewa & vipi mwakyembe Yupo hapa jf kwani ..? Tuambie anatumia I'd gani ni pm nimpe pole
 
Ni dua nzuri, lakini kumbuka hata wale waliomfanyia Mwakyembe ubaya huo wako makanisani. Wanasali na kutakaswa... Wanaendesha harambee na kumtolea Mungu sadaka vilevile! Pengine wanafanya hivyo kama ishara ya toba!! Je unaonaje? Pamoja na dua hii ya kutaka hao wabaya waangamie, Mungu ataisikiliza dua ya nani kati ya hao wawili?
 
karibu mnatuchosha na mwakyembe kama angelishwa sumu asingeogopa kusema tangu aliporudi India
 
mwakyembe ameamua kutengeneza cinema ya mabishano ya nani anawajibika kuuambia umma yaliyomsibu.....sijapenda
 
mwakyembe amekuwa anatoa vipande vipande vya movie yake, niliangalia part I alipokuwa mgonjwa nyumbani kwako na part II aliporudi kutoka India, nimesubiri sana part III ya ama kalishwa sumu au hakulishwa sumu bila mafanikio. Hata ikitoka part III sitanunua.
 
Watu huungama kwa mtu ama kwa mungu wa mbinguni?

Mungu huonekana katika watu neno la Mungu linatufundisha kuwa mwanampotevu alikusudia moyoni mwake naye akaamua kurudi ndipo sasa katika maungamo yake alisema nimekosa mbele yako wewe baba yangu na Mungu wangu.....Naye mtoza ushuru alipotembelewa na Yesu alisema tangu leo nitawarudishia wale wote niliowachukulia malizao...kuonyesha toba ya kweli...Toba ya kweli inaambatana na uponyaji wa mwenye kutenda na aliyetendewa ndiyo maana unapaswa kuomba msamaha kwa uliomkosea ili kuwe na uponyaji wa roho zote mbili za mkosaji na mtendwa kosa....Love fears nothing; akitubu alafu aliyekosewa akalipiza kisasi hapo Mungu huingia kati kumtetea mkosaji....
 
Back
Top Bottom