Ushirikina unaongezeka kwa kasi kubwa duniani

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,753
699,394
Changamoto za maisha zinazidi kuikumba dunia. Kisiki cha ajira ni mfupa uliowashinda hata mataifa yaliyoendelea sana kiuchumi
Shortcut nyingi za madawa, silaha, vikundi vya kigaidi na umafia wa namna zote vimedhibitiwa kwa kiwango kikubwa. Ni kama sasa dili zile kubwa kubwa zimetoweka na hata kama zipo kwasasa zinahitaji akili kubwa na mtaji mkubwa na watu wachache kuzitekeleza
Huko kwa wenzetu sasa ni mwendo wa makafara kupitia vyama vya giza vilivyobatizwa majina ya freemason, satanism nk

Huku kwetu mmh, hali ndio mbaya kabisa. Walio nacho kidogo wanawindwa na kila mtu
Wanawindwa na vibaka
Wanawindwa na wezi
Wanawindwa na tozo
Wanawindwa na chumaulete
Wanawindwa na wachawi ama kuwaharibia ama kuwafanya watumwa wao kwenye kipato. Kazi unafanya wewe mapato wanachukua wengine

Jaribu kuangalia trend ya watu wanaoanguka kibiashara kwa sasa
Jaribu kuangalia trend ya watu ambao biashara zao zinavyozorota
Angalia watu wanavyofilisika na kuharibu maisha yao kutokana na ulevi ama kufilisiwa na mabenki kutokana na mikopo

Tunaweza kutumia korona kama kigezo cha haya yote lakini nyuma yake kuna msingi mkubwa wa ushirikina unafanya kazi. Imefika mahali huko mtaani hata ukionekana na nguo mpya ni shida. Utawangiwa na kuchawiwa usiku mzima.

Kwa bahati mbaya kabisa hao waganga tunaowaendea kutafuta suluhu ndio hao hao wameendewa na wabaya wetu kutuumiza
Yaani ni sawa na double taxation kwenye tozo na miamala. Ukituma unakatwa, akipokea na kutoa anakatwa! Mganga anachukua kwako kumbe kachukua pia kwa mbaya wako.

Tunaibiwa sana kwakweli halafu tunaumizana sana kwakweli, hatutaki kuona wengine wanapata na kujikwamua kimaisha. Tunasema mioyoni mwetu. BORA TUKOSE WOTE! roho ya kwanini hii! Yaani kati yetu kuna ambao wanaona kushindwa kwao kumesababishwa na wewe. Kukosa kwao wewe ndio sababu.

Changamoto za maisha zinatufanya tuwe na roho mbaya sana tunateketea na kumalizana wenyewe. Ukiniuliza suhusu ninini nitakwambia hata mimi sijui ila tu watu wanarogana sana sasa hivi
 
Ukija kwenye biashara sasankuna matapeli wa ajabu leo utaibiwa kwa njia hii utasema nimejifunza keaho njia watakayokuja kukuibia unabaki dilema huelewi ufanye nini
 
Unadhani haupo tena huko lakini bado ni topic ambazo unazipenda sana. Hujaondoka huko kuondoka kirahisi rahisi katika shughuli uliyoipenda na kuifanya kwa miaka mingi ni DHANA TU.

Mimi sipo tena huko.. Maneno ya Mungu yanasema tazama ya kale yamepita na sasa yamekuwa mapya
 
Ukija kwenye biashara sasankuna matapeli wa ajabu leo utaibiwa kwa njia hii utasema nimejifunza keaho njia watakayokuja kukuibia unabaki dilema huelewi ufanye nini
baby zu naomba tuwasiliane leo jioni tafadhali...MUHIMU
 
Unadhani haupo tena huko lakini bado ni topic ambazo unazipenda sana. Hujaondoka huko kuondoka kirahisi rahisi katika shughuli uliyoipenda na kuifanya kwa miaka mingi ni DHANA TU.
Niombee sana..ulichokisema ni kweli tupu
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Changamoto za maisha zinazidi kuikumba dunia. Kisiki cha ajira ni mfupa uliowashinda hata mataifa yaliyoendelea sana kiuchumi
Shortcut nyingi za madawa, silaha, vikundi vya kigaidi na umafia wa namna zote vimedhibitiwa kwa kiwango kikubwa. Ni kama sasa dili zile kubwa kubwa zimetoweka na hata kama zipo kwasasa zinahitaji akili kubwa na mtaji mkubwa na watu wachache kuzitekeleza
Huko kwa wenzetu sasa ni mwendo wa makafara kupitia vyama vya giza vilivyobatizwa majina ya freemason, satanism nk

Huku kwetu mmh, hali ndio mbaya kabisa. Walio nacho kidogo wanawindwa na kila mtu
Wanawindwa na vibaka
Wanawindwa na wezi
Wanawindwa na tozo
Wanawindwa na chumaulete
Wanawindwa na wachawi ama kuwaharibia ama kuwafanya watumwa wao kwenye kipato. Kazi unafanya wewe mapato wanachukua wengine

Jaribu kuangalia trend ya watu wanaoanguka kibiashara kwa sasa
Jaribu kuangalia trend ya watu ambao biashara zao zinavyozorota
Angalia watu wanavyofilisika na kuharibu maisha yao kutokana na ulevi ama kufilisiwa na mabenki kutokana na mikopo

Tunaweza kutumia korona kama kigezo cha haya yote lakini nyuma yake kuna msingi mkubwa wa ushirikina unafanya kazi. Imefika mahali huko mtaani hata ukionekana na nguo mpya ni shida. Utawangiwa na kuchawiwa usiku mzima.

Kwa bahati mbaya kabisa hao waganga tunaowaendea kutafuta suluhu ndio hao hao wameendewa na wabaya wetu kutuumiza
Yaani ni sawa na double taxation kwenye tozo na miamala. Ukituma unakatwa, akipokea na kutoa anakatwa! Mganga anachukua kwako kumbe kachukua pia kwa mbaya wako.

Tunaibiwa sana kwakweli halafu tunaumizana sana kwakweli, hatutaki kuona wengine wanapata na kujikwamua kimaisha. Tunasema mioyoni mwetu. BORA TUKOSE WOTE! roho ya kwanini hii! Yaani kati yetu kuna ambao wanaona kushindwa kwao kumesababishwa na wewe. Kukosa kwao wewe ndio sababu.

Changamoto za maisha zinatufanya tuwe na roho mbaya sana tunateketea na kumalizana wenyewe. Ukiniuliza suhusu ninini nitakwambia hata mimi sijui ila tu watu wanarogana sana sasa hivi
Wachawi wengine wanajiongelesha wenyewe kisha wanajijibu wenyewe

Screenshot_20210907-172551_Chrome.jpg
 
Mkuu, umenena vema. Ama ni ushirikina au kukosa ubunifu. Mfano, ukifungua biashara, kabla wiki/mwezi haujaisha watu wanaiga, tena eneo hilohilo.
Maofisini kuharibiana kazi imekuwa fasheni, kama vile mshahara watauchukua wao. Hapo hujazungumzia kuvurugiana safari za kikazi ili kukukosesha posho. Madada miji yao imewashinda halafu wanawaonea wivu wifi zao, ugomvi wa kifamilia hauishi.
Jambo la msingi, kuomba baraka za Mwenyezi MUNGU., and NEVER GIVE UP mpaka kieleweke
 
Dunia imegeuka kuwa uwanja wa fujo za kila aina... Imagine hata manabii na mitume nao wanapanga foleni kwa waganga wa kienyeji
 
Back
Top Bottom