Ushiriki wa wanaume afya ya uzazi waleta mafanikio

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
Na Rachel Mrisho, Rukwa USHIRIKI wa wanaume katika afya ya uzazi umesaidia kupunguza idadi ya mimba shuleni katika Wilaya ya Nkasi iliyopo mkoani Rukwa.

Chachu ya mafanikio hayo imetokana na kuanzishwa kwa Mradi wa Ushiriki wa Wanaume katika Afya ya Uzazi (TMEP) unaoendeshwa na Chama cha Elimu ya Afya ya Uzazi cha Sweden (RFSU) na Shirika lisilo la kiserikali Mkoani Rukwa (RODI).

Ofisa Elimu wa Wilaya ya Nkasi, George Mwahinda, alisema mradi huo ambao pia unawalenga vijana waliopo shuleni kutambua dhana ya ushiriki wao katika afya ya uzazi umewawezesha wanafunzi kujitambua na kuchukua hatua za kujikinga wasipate mimba au kuwapa mimba wenzao.

Kwa upande wa shule za msingi kabla ya kuanza mradi huu tulikuwa tunapokea kesi tano hadi saba za watoto kupata mimba kuanzia mwaka jana hadi mwaka huu hakuna kesi hata iliyoripotiwa.

Kama unavyofahamu tatizo la mimba shuleni ni changamoto kubwa tunajivunia kuona hakuna taarifa ya mimba shuleni watoto wetu wameelimika kwa mfano hivi sasa wasichana na wavulana wamekuwa huru kwenda vituo vya afya kuomba kinga za kuzuia mimba tofauti na hapo awali ambapo walikuwa wanaona aibu.

Ni vyema mradi huu ukaendelea nchi nzima kwa kuwa utasaidia kupunguza tatizo la mimba shuleni ambalo kila siku Serikali inatafuta njia ya kukabiliana nalo na hii itawezekana tu endapo itawekeza rasilimali na kushirikiana kwa karibu na TMEP katika kufikisha ujumbe, alisema Mwahinda.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nkasi, Emmanuel Kushoka, alisema Serikali katika mipango yake imekuwa na wazo la kuwashirikisha wanaume katika huduma hiyo ambayo imejengeka kuwa maalumu kwa akina mama peke yao.

Kumekuwapo na mabadiliko baada ya TMEP kutoa elimu ya afya na ujinsia, wanaume wengi wamebadili mtazamo na kwa kiasi kikubwa mradi huu umesaidia kubadili mila na desturi zisizofaa ambazo zinawasababisha wanaume kutoshiriki katika huduma hiyo muhimu.

Naye, Ofisa Sera na Uraghabishi wa RFSU, Arthur Mtafya, alisema Wilaya ya Sumbawanga na Nkasi ni kiini cha mabadiliko na kuna haja jamii kuiga mfano huo.

Kutokana na mafanikio haya tunaona kuna haja Serikali kuingiza elimu ya afya ya uzazi na jinsia katika mitaala ya shule na hatimaye ile dhana ya kwamba elimu hiyo ni ushawishi wa ngono, iondolewe ili mafanikio ya kutokomeza mimba shuleni yaweze kufikiwa, alisema Mtafya.

Toa Maoni yako kwa habari hii
 
Back
Top Bottom