Tuambie kwanza: wewe una Phd katika fani gani na unafundisha shule qani?Kwa miaka ya sasa ni rahisi sana kuona mwalimu ana Masters/PhD lakini yupo tu anafundisha huko shuleni, ila mabosi wake wote wana Shahada. Huyu mwalimu mwenye Masters/PhD anaambulia kuhujumiwa tu na mabosi hao ili kumkatisha tamaa.
Mfano, anaweza akawa amepata mchongo mahali pengine kutokana na sifa alizonazo akaandika barua, lakini still maboss wake wakagoma kumpitishia barua zake kwa madai Walimu hawatoshi😀 na mengine mengi.
Hivyo basi, tunaomba wizara husika itoe mwongozo ambao utapunguza hujuma za kupata vyeo na nafasi mbalimbali za hawa walimu wenye Masters/PhD.
Hata ikiwezekana wafanyiwe interview kupata hizo nafasi za uongozi ili hujuma zipungue/ziishe kabisa.