Ushauri wangu kwa Zuberi Zitto Kabwe

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,772
8,958
Mimi nikiwa mmoja wa watu ambao tumeweka matumaini makubwa kwa chama cha Chadema kuleta mageuzi nchini nina ushauri mdogo sana kwa Zitto kuhusu SIASA zake na misimamo yake ambayo ndiyo sababu na chanzo cha yeye kuwa bangusilo ktk kila tukio la Upinzani..

Mheshimiwa Zitto amekuwa akisimama sana peke yake (independent) kwa fikra kwamba anaweza kuleta mabadiliko kupitia mwamvuli wa CCM. Hutumia sana maneno ya kwamba yuko huru na anafanya kile anbachokiamini yeye kuwa ndio haki na sahihi. Kwa fikra hizo amekuwa mstari wa mbele ktk tunzi za uwekezaji nchini wakati yeye kama mwanasiasa wa Upinzani hakutakiwa kabisa kugusa jambo hilo pasipo kuwepo makubaliano na ushirikiano wa vyama (Bipartisan) ktk kufuata sera (policies) zitakazo tumika..

Siku zote mwanasiasa na hasa mbunge wa chama cha Upinzani unatakiwa kuwa kinyume cha maamuzi ya sera za chama tawala, napengine kutumia nafasi hiyo kuweka shinikizo kwa chama tawala wakubali kufuata sera za Upinzani lakini wewe binafsi huwezi kutumikiwa na sera zile zile ambazo ndizo sababu ilokufanya wewe usimame upande wa pili, fikra hizi ni kuonyesha immaturity ktk ulingo wa siasa!

Nakushauri sana mkuu wangu achana na siasa za CCM inapofikia maswala ya kamati yako ya bunge. Kama mbunge wa Upinznai unachotakiwa ni kutafuta makosa ktk sera zao na kuweka wazi ubadhilifu unaofanyika laa sivyo hakuna sababu ya kuwa na upinzani maana sote tunakubaliana na sera za Chama tawala. Kazi yako ni kupinga sera hizo na sio kujaribu kurekebisha utekelezaji wa miradi ndani ya sera mbovu.. Siasa haijengwi hivyo mkuu wangu.

Huwezi kurekebisha utekelezaji wa sera za CCM kwa kutumia kiti cha upinzani -HAIWEZEKANI isipokuwa utatumiwa muda wote na kuwa the weakest link kwao kumaliza upinzani, maana kinachowezekana kutekelezeka kinatokana na sera zenyewe ambazo wewe kama Mpinzani hukubaliani nazo.

Brother, kitumikie chama chako, simama nyuma ya sera za chama chako na pingana na sera za chama tawala kama mpinzani na sii kutekeleza sera za chama Tawala kwa fikra zile zile zilizotufikisha hapa tulipo. Mtazame mwenzako January Makamba, he is smart kisiasa na siku zote husimama nyuma ya chama chake hata kama hakubaliani na mtu ndani ya chama. Mtazame Lowassa, he is smarter hata kama hakubaliwi na watu wengi nje ya CCM lakini ameendelea kujijenga ndani ya chama kuliko nje kwa sababu huko ndiko alikozaliwa - Hutaki yote haya Unaacha!
 
Mandala nakubaliana na wewe. Zitto zingatia huo ushauri, vinginevyo heshima na hadhi yako vinaanza kuporomoka
 
Mimi nikiwa mmoja wa watu ambao tumeweka matumaini makubwa kwa chama cha Chadema kuleta mageuzi nchini nina ushauri mdogo sana kwa Zitto kuhusu SIASA zake na misimamo yake ambayo ndiyo sababu na chanzo cha yeye kuwa bangusilo ktk kila tukio la Upinzani....

simjibii mwanasiasa Zitto Kabwe, bali najaribu kuelezea jinsi ninavyoona!
Tatatizo liko hivi (nafikiri) Zitto anataka kuendelea mbele katika siasa lakini tatizo anatoka familia ya kimaskini kama watz wengi tulivvyo, na ukweli ni kwamba kama huna pesa hakuna mafanikio katika siasa, huo ndio ukweli wenyewe! Sasa swali linakuja atapata wapi pesa? Kuna mawili aidha mtu au kikundi cha watu kimpe ili afanikishe azma yake ya kisiasa au yeye mwenyewe atafute, lakini atafute wapi kwao sio matajiri?

Kwa hiyo njia pekee na raisi iliyobaki kuzunguka huko huko serikalini kwa watu wa CCm kufanya nao dili na mwishowe kupata pesa ambayo sasa anaweza kuitumia kukamilisha mipango yake ya kisiasa, lakini hiyo haiji bure ina bei pia na bei yake ndio kama hiyo anayoilipa sasa , na huu ni mwanzo mengi yatakuja kwa maana piga ua garagaza anahitaji PESA kama anataka kutimiza azma ya kusonga mbele kisiasa!
 
Kijana huyu mnafiki sijapata kuona......kweheri zitto ulitaka kuwafanya watz mambumbu eeee sasa misifa yako utaona mwisho wako pia
 
Mkandara asante sana.

All the well wishers knows that Zitto is a prodigal son. Now what he need most is not to trade fire with fire. He simply need to pause and consider his ways.

Mh. Zitto. ambitions are all too natural traits for us all, none here is telling you anything to the contra. Neither do Mkandara or me or anyone really intends herein to lecture you brother.

What some of us perceives (may be wrongly) is when you foster your ambitions as the political absolutes. When you define things in a ruthless contrast to what CHADEMA manifests. Those two things really put you in direct jeopardy position.

It's obviously a sorry state to be in, so the quick it ends the better.
 
Mkandara nakubaliana na wewe kabisa Zitto saa hizi anyamaze kabisa na aachane na siasa za kutetea Chama Tawala, hata km anatafuta pesa za kugombea nafasi za juu katika Chama chake au Urais, pesa chafu zitammaliza, hadi ataenda kugombea binafsi na huko hakuna wapiga kura wala wapambe, Pia aachane na Magazeti kabisa sio yote mazuri angefuatila Gazeti la Jamhuri au Majira ndio angeamini hawako nae
 
Mkandara nakubaliana na wewe kabisa Zitto saa hizi anyamaze kabisa na aachane na siasa za kutetea Chama Tawala, hata km anatafuta pesa za kugombea nafasi za juu katika Chama chake au Urais, pesa chafu zitammaliza, hadi ataenda kugombea binafsi na huko hakuna wapiga kura wala wapambe, Pia aachane na Magazeti kabisa sio yote mazuri angefuatila Gazeti la Jamhuri au Majira ndio angeamini hawako nae
Mkuu wangu binafsi yangu sidhani kabisa kwamba Zitto anasukumwa na tamaa ya Pesa - Hapana.. sio kweli kwa sababu namjua Zitto japo sii kwa saana hivyo. Sii mla rushwa tena nadhani anapiga vita rushwa kuliko watu wengi sana hata ndani ya chama chake mwenyewe hupenda kuhoji matumizi ya chama..Ni mtu safi sana inabidi uwe naye karibu ndio utamjua..

Tatizo la Zitto ni imani yake kwa kuelewa kwamba nchi yetu tajiri sana na hakuna sababu ya watu wake kuwa maskini na kwa ambiton yake anafikiri yeye ataweza kufanya mabadiliko. Lakini njia za mageuzi hayo ndizo zinazo mponza kwa kujishirikisha na sera za CCM iwe ktk makaa ya mawe Mchuchuma, bomba la gas, kesi ya Mhando na Maswi na uwekezaji mwingine nchini. Hii sio kazi yake kama Mpinzani, kazi yake ni kuonyesha sera mbovu zinatumika na ndio maana matumizi mabaya yanafanyika. tatizo lolote ktk uwekezaji wa Tanesco au wizara angeliwakilisha kama hoja ya chama chake au upinzani..

Kila napomsoma Zitto huwa kama vile Chadema ndio ipo madarakani, yaani yeye husisitiza hili ama lile litawezekana kufanyika under his watch..Litafanikiwa vipo kwa kutumia sera za CCM. Na ndio maana mimi husema Zitto sio mwanasiasa bali mtekelezaji mzuri na kazi hiyo ataiweza tu kuifanya kama Chadema wataingia madarakani maana sera zake zinaendana na makusudio yake. Nimesema sana kuhusu UONGOZI, kiongozi bora mwanasiasa lazima awe spiritual, awe innovator ktk what he preach, na sii Pedegee, a good Managing Director au CEO ktk muundo wa Utekelezaji wa sera mbovu iwe economic development, ajira ama client retention.
- Ni hayo tu...
 
Zitto baada ya hili swaga la rushwa kupita, natabili atarudi kwa kasi sana ktk kuiwajibisha hii serikali ya ccm, baada ya kesho kutoa tamko kwa waandishi wa habari tutarajie yule Zitto wa Buzwagi 1997-1999
 
Last edited by a moderator:
Kama ana masikio na asikie lakini kama atajidai mjuaji na kuendelea kusimamia anachokiamini siku zote basi apuuze thn matokeo yake atayaona
 
zzk alijiona kifikra kua tayari ni mtawala aliye makini wa serikali na chama kilichopo badala ya mpinzani makini mwenye nia ya kuja kushika dola ya nchi hii na kuondoakana na madudu yote ya CCM
 
Back
Top Bottom