Ushauri wangu kwa Zuberi Zitto Kabwe

NYINYI mawaziri hamfanyi kazi uchumi wa nchi unadorora sababu ya nyinyi kuwazia URAIS, tutamuomba rais awatimue. nauliza kama wapo mawaziri wa namna hiyo ni kosa kuwakosoa. mimi nikiteuliwa na chama changu kugombea urais ntakubali. vilevile napenda kugombea urais. jamani kuna kosa. aaaah kwa kuwa nyie ni watani ,ngoja niwaache. ila mawaziri waligutuka maana jamaa mwiba mkali wengine chamoto walikiona ,wengine wakaula na wako on fire kama mh MWAKYEMBE.
 
Mimi nikiwa mmoja wa watu ambao tumeweka matumaini makubwa kwa chama cha Chadema kuleta mageuzi nchini nina ushauri mdogo sana kwa Zitto kuhusu SIASA zake na misimamo yake ambayo ndiyo sababu na chanzo cha yeye kuwa bangusilo ktk kila tukio la Upinzani..

Mheshimiwa Zitto amekuwa akisimama sana peke yake (independent) kwa fikra kwamba anaweza kuleta mabadiliko kupitia mwamvuli wa CCM. Hutumia sana maneno ya kwamba yuko huru na anafanya kile anbachokiamini yeye kuwa ndio haki na sahihi. Kwa fikra hizo amekuwa mstari wa mbele ktk tunzi za uwekezaji nchini wakati yeye kama mwanasiasa wa Upinzani hakutakiwa kabisa kugusa jambo hilo pasipo kuwepo makubaliano na ushirikiano wa vyama (Bipartisan) ktk kufuata sera (policies) zitakazo tumika..

Siku zote mwanasiasa na hasa mbunge wa chama cha Upinzani unatakiwa kuwa kinyume cha maamuzi ya sera za chama tawala, napengine kutumia nafasi hiyo kuweka shinikizo kwa chama tawala wakubali kufuata sera za Upinzani lakini wewe binafsi huwezi kutumikiwa na sera zile zile ambazo ndizo sababu ilokufanya wewe usimame upande wa pili, fikra hizi ni kuonyesha immaturity ktk ulingo wa siasa!

Nakushauri sana mkuu wangu achana na siasa za CCM inapofikia maswala ya kamati yako ya bunge. Kama mbunge wa Upinznai unachotakiwa ni kutafuta makosa ktk sera zao na kuweka wazi ubadhilifu unaofanyika laa sivyo hakuna sababu ya kuwa na upinzani maana sote tunakubaliana na sera za Chama tawala. Kazi yako ni kupinga sera hizo na sio kujaribu kurekebisha utekelezaji wa miradi ndani ya sera mbovu.. Siasa haijengwi hivyo mkuu wangu.

Huwezi kurekebisha utekelezaji wa sera za CCM kwa kutumia kiti cha upinzani -HAIWEZEKANI isipokuwa utatumiwa muda wote na kuwa the weakest link kwao kumaliza upinzani, maana kinachowezekana kutekelezeka kinatokana na sera zenyewe ambazo wewe kama Mpinzani hukubaliani nazo.

Brother, kitumikie chama chako, simama nyuma ya sera za chama chako na pingana na sera za chama tawala kama mpinzani na sii kutekeleza sera za chama Tawala kwa fikra zile zile zilizotufikisha hapa tulipo. Mtazame mwenzako January Makamba, he is smart kisiasa na siku zote husimama nyuma ya chama chake hata kama hakubaliani na mtu ndani ya chama. Mtazame Lowassa, he is smarter hata kama hakubaliwi na watu wengi nje ya CCM lakini ameendelea kujijenga ndani ya chama kuliko nje kwa sababu huko ndiko alikozaliwa - Hutaki yote haya Unaacha!

immaturity haipo kwa wanasiasa tu hata katika mwandishi anaweza akawa hivyo kutokana na asipoelewa sifa na wajibu wa kazi yake.mwandishi maneno yako ni mazur ila hakua mature enough katika tafakuri na changanuzi zako.mfano.mwanasiasa wa upande wa upinzani haina maana kama kila kitu kinacholetwa na chama tawala kupitia ilani ya chama hicho akipinge.anatakiwa akipinge iwapo patakua na kasoro na kama hapana kasoro wanatakiwa wakubaliane nacho na hiyo ndo sahihi.mfano.jalia ilani ya ccm ni kuinua kiwango cha elimu nchini.hatua wanazochukua ni nyingi ikiwemo ya kusambaza vitabu mashuleni.jee iwapo vitabu hvyo vinafka kweli shule.jee ktk hali hyo chadema lazme wapinge kupelekwa vitabu shuleni?
 
"Vijana na watanzania wengi walikupenda, si kwa sababu wewe ni mwerevu kuliko wao, bali kwa sababu uliusimamia ukweli. Ni dhahiri kwamba vijana waliojiunga na Chadema kwa kukufuata wewe, hawakukufuata wewe kama wewe, bali waliufuata ukweli uliousimamia na walioutafuta kwa muda mrefu. Endapo utauacha ukweli huo, vijana wote watakukataa mara".

ZZK kaka yangu kwaheri katika uwanja wa siasa!nitakumis xana!CCM Watakutumiaje ilhali wanajua wewe ni mnafiki?utatupwa kama kondomu ndugu yangu!umeshaahidiwa vyeo na kutusaliti tulio wengi!MOLA ATAKUTENDEA HAKI YAKO KAMA ULILOTENDA NA UNALOTENDA KWA WA TANZANIA WALIOVUNJIKA MOYO NA KUKOSA MATUMAINI KWA MIAKA MINGI NI SAHIHI!
 
Zitto ana kazi kweli, CDM hawamuamini kabisa na CCM hawamuamini kabisa. Ni popo, si mnyama si ndege!!!
 
Chadema kama kinavyojipambanua kama chama cha democrasia na maendeleo ni lazima kipitie katika msuguano wa mawazo ili kijitengeneze na kipate mwelekeo. Lazima kuwe na uhuru wa mawazo kila mtu aongee kwa uwazi bila kutishwa aongee kile anachohisi ni sahihi na chenye faida kwa chama bila kuitwa msaliti au pandikizi. Chadema hakitaweza kuendelea kama hakutakuwa mawazo mgongano ndani ya chama. Mawazo haya lazima yashindanishwe kwa hoja za kimsingi zitakazo kinyanyua chama, watu wawe huru kutoa mawazo yao juu ya mwelekeo wa chama.


Watu wawe huru kuchukua fomu kugombea uenyekiti, ukatibu mkuu na tiketi ya uraisi bila kutishwa kuitwa pandikizi au msaliti. Kila mtu awe na uhuru huo ndio demokrasia yenyewe kila mtu ashindanishwe na mwenzake atakayeshinda kwa hoja ndio apite na awe kiongozi. Chadema lazima kipitie mitafaruku ya kimtizamo ni hatua muhimu. Habari ya zidumu fikra za mwenyekiti na katibu mkuu ziishe.

Vijana wa Taifa hili mnauwezo wa kubadilisha vyama vyetu na nchi yetu kama mtakuwa tayari kubadilisha mitazamo hii iliyomea kwa viongozi wetu kwa muda mrefu kama kweli tunataka kujenga Taifa la kidemokrasia. Ni ukweli kwamba Demokrasia katika nchi kwa upana wake huanza katika Vyama. Vyama vyetu vinapokuwa vya kidemocrasia na wanachama wake wanapokuwa huru kutoa mitazamo yao bila kutishwa na kuitwa mapandikizi, kunapokuwa na uchaguzi huru kila mtu akiwa na nafasi ya kugombea nafasi yeyote katika chama bila kubughuziwa, tutakuwa na nafasi kubwa ya kujenga demokrasia yetu katika Taifa letu na katika vyama na hii iwe nuru yetu.

Namuomba Zito kabwe aendelee na harakati zake za kukiweka chama sawa ili kiwe cha kidemocrasia zaidi. Hii itasadia vijana wanaokuja kupata nafasi ya kushiriki uongozi wa juu katika chama. Ni lazima uhuru huu upiganiwe. Msikubali kulishwa maneno lazima mfikiri.

Chama cha demokrasia na maendeleo ni lazima kiwe reformed hii sio tu kwa manufaa ya Chadema bali pia kwa manufaa ya nchi kwakuwa ni lazima tuwe na vyama imara ili tupate serikali iliyobora na ya kidemocrasia. Hili ni jambo la msingi kabisa kuwa na vyama ambavyo misingi yake imesindikwa imara. Vyenye utulivu na mshikamano ambavyo vimejengwa katika misingi ya uzalendo kwa Taifa. Ni lazima tujenge harmonic relationship kati ya chama na chama pamoja na serikali. Kupingana kwetu na kuwe kwa hoja na sio propaganda zisizo na manufaa. Hili Taifa linahitaji kusonga mbele na jukumu hili ni letu. Tunahitaji viongozi wenye busara kushika hatamu katika Taifa na katika vyama vyetu.

Chadema ni lazima kiwe na wanachama wanaofikiria sio wanaofuata mkumbo au mashabiki ili kijibadili na kusonga mbele. Mimi nafikiri Zitto kabwe malengo yake sio kukivunja Chadema bali kuki reform. Tujenge utamaduni wa kusikilizana na kutafakari kile mtu anachoongea pasipo kukurupuka bali kutafakari kwa kina kwanza.

Kwahiyo wanachedema punguzeni hasira na mmsikilize mtazamo wake. Mtakapo msikiliza mpambanue na kumjibu lakini ninachoona kwamba huyu jamaa ni reformer. Pengine anaweza kuleta mwelekeo katika chadema akipewa nafasi. Demokrasia ni lazima ijengwe katika Taifa hili na misingi yake iwekwe imara.

Tuna umuhimu mkubwa wa kutengeneza viosonary leaders katika Taifa hili na kuruhusu watu wenye mawazo mapya kuingia katika system ili kuleta mapinduzi.

Chadema ni lazima ibadili mtazamo wake na uendeshaji wa siasa zake. Ili tusijejenga chuki katika Taifa hili. Mtu kuwa CCM sio adui na wala mtu kuwa Chadema sio adui. Ni lazima tuangalie mazingira upya ya siasa zetu. CCM wanapaswa kujua kwamba nchi hii sio mali yao chama chchote kile kina haki ya kuliongoza Taifa hili kikipewa idhini na wananchi. Kitendo chochote cha kutaka kuzima demokrasia, kutumia nguvu ya polisi kuzima harakati za watu kutumia vyama vyao kuweza kuingia madarakani kutumikia Taifa lao ni uhaini. Kuingiza vibaraka kutaka kuwaharibu harmony and order katika vyama ni uhaini na ni ukiukwaji wa katiba wa uhuru wa vyama kwanini mnataka mbaki peke yenu? Vyama vyote vya nchi hii vina haki kuongoza nchi. CCM kwa kuendelea kufanya hivi mtaharibu nchi.


Ni lazima tuendeshe siasa zetu katika misingi ya kuheshimiana. Tuweke akilini misingi bora ya vyama vyetu vya siasa ndio vinavyopelekea serikali bora. Ni lazima tuondoe hili suala la kuingia kwenye siasa kwa manufaa binafsi. Kila mtu apewe nafasi ya kuongoza kama ni kipaji chake na ana uwezo ni lazima tujenge mazingira ambayo kila mtu ataweza kushiriki katika uongozi wa kisiasa bila uoga. Bila kuogopa matusi ambayo yatamvunjia heshima yake. Kwahiyo tunahitaji Taifa hili lisonge mbele lakini bila vyama imara itakuwa ndoto. Juhudi zetu ni lazima iwe kujenga vyama hivi katika misingi ya kidemokrasia. Ili kila mtu awe na uwanja mpana wa kushiriki katika uongozi wa nchi yake bila kuogopa.

Mwisho nchi yetu ni jamhuri. Mamlaka yote hutoka kwa umma. Viongozi kikatiba wanawajibika kusimamia mali za umma na kuhakikisha nchi inaendelea. Wapo kwenye uongozi kwa faida ya umma. Vitendo vyovyote vya kifisadi ni USALITI DHIDI YA UMMA. Wananchi wana haki ya kuwa na hasira na serikali iliyowageuka na kama wakipata nguvu wana haki ya kuiondoa kwasababu imewekwa pale kwa faida ya umma. Kuleta maendeleo kwa watu.

Watanzania ni lazima tutengeneze serikali ambayo itatuvaa ambayo itaendana na sisi na kuwa na harmonius relationship kati ya wanaoongozwa na wanaoongoza. Hili ni muhimu sana kwa Taifa letu. Serikali ya watu iliyoundwa na watu kwa manufaa ya watu ni lazima iwepo na imee mioyoni mwa watu. Tujenge Taifa la haki na la watu wanaoheshimiana hii tumaini hili lazima limee mioyoni mwetu ya kwamba sisi ni wamoja na mwisho wetu ni mmmoja na ya kwamba kama tukiamua kwa mioyo yetu yote kulijenga Taifa hili iwe sehemu nzuri ya kuishi hatutashindwa. Watanzania wana nguvu hii ya kulijenga Taifa lao na kulipenda. Watoto wataifa hili lazima wajengwe katika utaifa na katika Uzalendo.

Vyama vyetu ni lazima visiwe kusanyiko la genge la watu wenye malengo binafsi na uchu bali kusanyiko la wenye malengo mema kwa Taifa. Watu wenye busara na hekima wanaoweza kujiongoza na kuongoza watu. Basi na mwangaza uangaze Taifa hili hata yule asiyeona sawasawa aweze kuona ya kwamba kuna matumaini kama tukibali fikra zetu na kuruhusu watu wetu bora kuongoza Taifa. Watu hao wapo hawapendi kushushiwa heshima na mazingira yaliyopo ya kisiasa. Ukweli ni kwamba mwelekeo wetu kama Taifa uko gizani. Unaweza kuzungumzia uchumi lakini uchumi hauwezi kuwa endelevu pasipo order and harmony. Lazima tuwe waangalifu sana nchi yetu sasa hivi ina migawanyiko. Tuombe mungu kiongozi ajaye aweze kuunganisha watu wetu na kuleta tumaini kwa watu wote.h
 
Nashindwa kukuelewa kwa kutambulisha au kumtwisha mtu kwa jina (Zitto) kuwa aendelee kupigania demokrasia kwenye chama ili hali Chadema kwa jina, itikadi, muundo na mikakati vinapigania democrasia.
 
immaturity haipo kwa wanasiasa tu hata katika mwandishi anaweza akawa hivyo kutokana na asipoelewa sifa na wajibu wa kazi yake.mwandishi maneno yako ni mazur ila hakua mature enough katika tafakuri na changanuzi zako.mfano.mwanasiasa wa upande wa upinzani haina maana kama kila kitu kinacholetwa na chama tawala kupitia ilani ya chama hicho akipinge.anatakiwa akipinge iwapo patakua na kasoro na kama hapana kasoro wanatakiwa wakubaliane nacho na hiyo ndo sahihi.mfano.jalia ilani ya ccm ni kuinua kiwango cha elimu nchini.hatua wanazochukua ni nyingi ikiwemo ya kusambaza vitabu mashuleni.jee iwapo vitabu hvyo vinafka kweli shule.jee ktk hali hyo chadema lazme wapinge kupelekwa vitabu shuleni?
immaturity ni pale mwandishi anapojibu hoja pasipo kuelewa anajibu hoja inayohusu nini...

Katika ushauri wangu nimezungumzia SERA lakini naona umeamua kujibu jkwa kuziungumzia ILANI ya chama, pengine yawezekana huelewi tofauti baina ya ILANI na SERA hivyo nakusamehe kwa leo na pengine tena itakuwezesha kukua kifikra ktk kusoma vizuri na kuelewa hoja za watu..
 
Back
Top Bottom