Chiomaizwe
Member
- Apr 9, 2015
- 24
- 41
Wana jamvi habari za siku tele,
Mimi nimekuwa naingia hapa jamvini kama guest baada ya kuelezwa na rafiki yangu juu ya uwepo wa hili jamvi. Nimekuwa msomaji wa mada mbali mbali ambazo kwa namna moja zimenifunza mengi sana.
Leo hii nimeamua kujiunga ili nilete swala langu japo mnishauri manake nimekuwa nalo kwa mdua sasa na sijaweza kuomba ushauri kwa mtu yeyote yule.Nianze hivi hii ni habari ya kweli na kama ukiona nimekuudhi naomba uniwie radhi lakni sina budi tu kuisema manake muda mwingine mwiba wa kujidunga mwenyewe unahusika.
Mimi ni mwanamke mwenye miaka 39 sasa, nikiwa na watoto wawili na ndoa ya kikristo. Kwa bahati njema sana Mungu alitupa watoto wazuri na wenye afya katika kipindi ambacho sote mie na mume wangu tukiwa chuoni tunasoma. Yeye alikuwa anasoma digree ya 2 na mie nilikuwa nasoma ya kwanza katika fani tofauti.
Maisha yetu japo yalikuwa ya kimaskin lakin tuliishi kwa raha amani na upendo furaha na heshima na yakawa yana afya za rohoni na mwilini pia. Kiukweli mume wangu ni miongoni mwa wanume ambao ni wazuri wana upendo wa kweli, anajali na mtu anayependa zaid familia kuliko kitu kingine chochote.
Mimi kama mama nilijitahd sana kuwa na heshima na kutimiza wajibu wangu kama mama na hata kusaidia katika kuijenga familia kiuchumi.Miaka 5 iliyopita mume wangu alipata safari ya kwenda masomoni na ukweli nilijitahdi sana kuhakikisha kila kilichotakiwa alikipata ili aende nikiamini kwamba anaenda kwaajili ya manufaa ya famili. Wakati anaondoka nilikuwa ni mjamzito hivyo nilimwambia aende tu mie sina neno.
Kwa bahati nzuri mtoto alizaliwa baada ya mwezi toka asafiri na ukweli alifurahi sana. Alipopata likizo alikuja akamkuta tayari mtoto ni mkubwa na alikuwa kama na miezi 11 hivi. Siku chache kabla ya yeye kurudi tena ulaya tulipata ajali mbaya sana ya gari na familia nzima ilihusika, ingawa majeruhi tulikuwa mimi na mtoto huyu mdogo.
Nililazimika kumruhusu mume wangu kurudi shule kwasababu ticket yake ilikuwa hawez kuiahirisha kwa siku nyingi zaid, na nilijitahd sana japo mgonjwa kuhudumia wanangu akiwemo huyu mdogo ambaye alikwua amevunjia mguu.Hata hivyo maisha yalikwua mazuri na tuliishi kwa mapenzi sana, na kila alipopata likizo alikuja nyumban kutuona.
Sasa tatizo lilianza mwaka juzi kuna hela amabzo alinipa kwaajili ya kujengea mie nikazitumia hazikuwa nyingi sana ila pia zingeweza kufanya jambo kwenye ujenzi hata kama ni dogo, fedha zile sikuzitumia ivyo ila nilizitumia kwa kumtibu mtoto mguu na matumiz ya nyumban, alipokuja akakuta sikuzitumia nilimuelewesha akaelewa maisha yakaendelea.
Sikujua kama mume huyu ameweka kinyongo ila alipoondoka sasa toka mwaka 2013 hadi leo hajawah kuwasiliana na mimi wala watoto. Mara ya kwanza nilijua ni utan lkn nikashangaa miezi iankatika simsikii mara akanibock skype, tweeter na kila kitu, mara nikipiga hapokei simu yangu, mara email zangu kablock nikaishiwa nguvu kabisa.
Nikaona isiwe tabu wala sina sababu ya kuanza kuitisha vikao vya ukoo kujadili haya nikaamua sasa kuwa siriazi na watoto wangu wasome, wavae, na waishi maisha mazuri. Mungu bariki nikapata kazi kwenye kampuni moja ya utafiti na ushimbaj wa gesi.
Maisha yakaanza kuenda vizuri zaid kwa upande wangu. Ila mume nikawa bado sina mawasiliano naye. Mwaka ukakatika sijampata kwenye mawasiliano mama yake anaongea naye na dada zake lkn mie mkewe hapana niaksema siwez kununiana na wakwe zangu mie kisa yeye nikaachana na hayo mambo.
Huu sasa ni wamaka wa 3 sijamtia machoni ingawa kuna kipindi alikuja Tz akapokelewa na dada yake akakaa siku alizokaa na kurudi huko ulaya kwake mie hata sikuumiza kichwa nikasema watoto wangu ni bora zaid kuliko huyo aliyeko huko so niakjipa moyo maisha yakaendelea.Niliamuaga kawa na mchepuko ili nipate liwazo lakin pia vikanishinda manake sikupata ambaye tuko compatible nikaona nitulize akili kazini na kwenye malezi ya watoto manake hawa ndio watakao nitoa baadae.
Mwaka 2012 mwezi dec nilipata nafasi ya kwenda SA kwenye makao makuu ya kampuni ninayofanyia kazi, kulikuwa na mkutano wa wadau wakuu wa uchimbaj wa mafuta nagesi dunian nilikutana na watu wengi sana akiwemo Bwana mmoja DB ambaye ni mhadisi wa petroleum. Kama kawaida kwenye mikutano kunakupeana contacts basi na mie nikawa nimepata za watu wengi tuu.
Mwaka 2014 june kukafanyika mkutano mwingine Ghana nilipokwenda nikakutana na almost watu wengi niliokutana nao huko SA akiwemo DB hivyo network ikazidi kukomaa katika kazi. Mwaka huu mwezi jana pakafanyika kongamano la gesi la mafuta lililoandaliwa na ubalozi wa Canada hapa nchini mie nikawa naiwakilisha kampuni nikakutana tena na watu almost wale wale hivyo kibiashara nikawa nina watu wengi zaid kwenye huu upande ambao nawajua sana na tumezoeana.
Jambo la ajabu sna Bwana DB alikuwa ni mtu wangu wa karibu kikazi na yeye huyu tulikuwa tunawasiliana hasa pale ninapokwama kikazi kuomba ushauri nk na amekuwa akinimentor sana kwenye huu upande. japo kuwa tulikwa karibu lakin hatukuwah kupata muda wa kuongea maswala yetu ya kijamii kwa muda wote toka nimfahamu. Alipokuja hapa Tanzania sasa kwa mara ya kwanza akaniomba tutoke dina mie na yeye nikamkubalia.
Kweli kwenye dina tuliongea sasa mambo ya kijamii zaid kuliko ya kazi ndipo aliponieleza mkasa wa maisha wote, na kwamba mkewe ni marehemu, na anayemtoto wa kuasili muafrica wa Ghana, jamaa alifunguka sana na mie nikamwambia ukweli juu ya maisha yangu kwamba niko kwenye hali ya sintofahamu ya ndoa yangu.
Basi katika kuongea akaniambia kwamba anapenda basi kama nitaridhia anioe na yuko tayari kuwa na mimi na awe baba mlezi wa watoto wangu. Sikumjibu kwa haraka manake mie sijielewi na naogopa sana kutoa ahadi za uongo. Ila nilimkaribisha nyumban kwangu siku moja kabla hajasafiri kurudi kwao akawaona wanangu na akala chakula cha jion kisha akaondoka kurudi hotelin kwake.
Toka ameondoka DB amekuwa akinitumia salam anachat na mie kila mara kwenye messenger nk, pia amekuwa akiwasalimu watoto na kuonyesha nia ya dhati kabisa ya kua na mimi. Mie bado sijampa jibu manake sijui hatima yangu, ingawa kutoka kwa dada wa mume wangu nimeambiwa mume wangu kaoa binti huko anaish nae. Nilishtuka sana lakin nikasema maisha ndivyo yalivyo sina ujanja zaid.
Leo asubuhi nimefika tu ofisini DB akanipigia anataka kuja Tanzania kuniona na hapa amenipa email adress ya kampuni anayofanyia kazi niwatumie email kuwaomba wamruhusu aje kuniona na niseme kwamba namuhitaj kwa haraka sana. Nimejikuta napata kigugumizi nimjibuje wapendwa wangu.
Ugumu kwangu unakuja hapa, bado nampenda sana mume wangu ingawa amekosea. Pili kuanza maisha na mtu mwingine mgeni kabisa katika uzee huu najionea kama nitapata shida kwenye kuishi.Kitu ambacho nakiamini kutoka kwake ameniambia yuko tayari kulea watoto wangu, yeye anachotaka ni kupendwa, kujaliwa na kuheshimiwa tu katika maisha yake yaliyobaki. Yeye ana umri wa miaka 48.