Ushauri wa bure kwa PSRS

kyanyangwe

JF-Expert Member
Oct 31, 2018
1,147
2,746
Juzi kati ilibidi nigombane na ndugu yangu baada ya kunipigia ghafla akiniomba nauli ya kwenda kwenye usaili wa psrs huko Dar. Kwa kifupi ndugu yangu huyu alinishtukiza na sikua na kitu mfukoni, hivyo ikabidi niingie madeni kwa kumkopea pesa mahali.

Ushauri wenyewe ni huu:

Nashauri kwamba, kuwe na kipengele kitakachokua kinaonyesha expected date for interview ili watu wajiandae materially na mentally. Nikiwa na maana kwamba tangazo la kazi linapotoka waainishe deadline for interview na tarehe ya lini usaili utafanyika na mahali.

Hii itawasaidia hata wazazi na walezi kuweka akiba kwa ajili ya watoto wao kwa ajili ya hizi saili tofauti na hali ya sasa ya kushtukizana.

Hili linawezekana vizuri tu kwani nimeona taasisi nyingi za kimataifa wanasema kabisa kuwa deadline ya application ni siku flani na expected date for interview ni siku flani pia.

Huu ni ushauri tu wanaweza kuuchukua kama ulivyo au wakaukataa.
 
Huyo dogo interview yake imefanyika lini? na ilikuwa taasisi gani?

Nijibu hayo maswali na mimi nione kama kweli walizingua au Dogo alizingua
 
Ushauri mzuri,ila utumishi mbona huwa wanatoa gape la kama week nzima kwa ajili ya maandalizi?huenda dogo nae amezingua mwenyewe tu.
Nimeuliza hivyo naona hajanijibu.

Interview za juzi Dar, walitoa shortlist tarehe 31, interview zimefanyika tarehe 10.
 
Nyogeza: Kazi za kada zinazo fanana (Bugando, Ocean Road, Mhimbili). Interview za taasisi husika zote zifanywe sehemu 1 na mara moja (mf. Tarehe 1, 2, 3, hadi 4) tena iwe Dodoma siyo Dar.
 
Bugando na ORCI washajifanyia Mwanza na Dar.

Muhimbili ndio wameipanga Dom(inakuwa unafuu kwa watu wote wa pande mbalimbali za nchi)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom