Ushauri: Tiba ya kikohozi na mafua

Kwanza pole.Nashauri umrudishe mama hospitali akaanze upya dawa hizo mara 1.Dozi ya kifua kikuu huwa ni miezi 8.Halafu ni kosa kumsimamisha mgonjwa kutumia dozi ya dw aliyopewa na Dkt wake,hasa huyo wa kifua kikuu,kwani UNAMDHOOFISHA ZAIDI na KK kinaambukiza vibaya.
 
Wana JF habari zenyu bana hope mko poa.
Naomba mnisaidie ndg zangu,

Nina MAMA yangu 69 yrz ANAKOHOA like 2 yrz sasa, mwanzo madaktari walisema ni kikohozi cha kawaida akawa anapewa dawa za kawaida tu. Ila mwanzoni mwaka huu madaktari walisema ni Kifua Kikuu akapewa dozi ya kifua kikuu ila problem ikawa akitumia vile vidonge (kwa mda wa miezi mitatu) anakohoa sana kuzidi siku za nyuma, tukaamua kustopisha dozi.

Tatizo huwa anajisikia kuwashwa kooni then atakohoa, ila anapoanza kukohoa anaweza kohoa mfururizo kama dakika 5 hivi nonstop, baada ya kikohozi kukoma tu huwa anajisikia haja ndogo kila baada ya dakika kwa mda wa saa nzima hivi, mkojo wenyewe huwa mdogo tu mda mwingine, na huo mkojo hawezi kuuzuia (kuicontrol ) na akijichelewesha kwenda toilet basi atajikojolea.

Please mtanisaidiaje wanajamii nimsaidie my dearest mom, thanx, i will appreciate.
Chukuwa kitunguMaji menya kata vipande 4 ,, weka katika Asali fresh funika uzuri u weke pembeni kesho yake itatowa maji ,, kama Syrup basi mpe kijiko kimoja mara tatu au mara 4kwa siku inshaallah itamsaidiya .

Katika kila kiungo kuna hekima na siri yake.

Hewa ambayo tunaivuta sisi wanaadam ni hewa yenye vitu tofauti ndani yake kuna maji, oxygen, nitrogen, mvuke n.k kuna ambavyo ni muhimu ndani ya mwili wa mwanaadam na kuna vitu ambayo havina umuhimu wala havihitajiki katika mwili wa mwanaadam.
Lakini tunapovuta hewa, hewa ile huenda moja kwa moja kupitia katika tundu za pua hushuka katika bomba la koo hadi kwenda kwenye mapafu ya mwanaadam. Hewa hiyo haipiti hivi hivi kila sehemu inakuwa na kazi yake maluum.

Ndio maana ndani ya pua utakuta kitu kama maji maji yale ya lugha inaitwa MUCUS mucus kazi yake ni kukamata taka taka na vumbi ambalo linalopita ndani ya mwili wa mwaadam.

Hivyo maradhi ya kifua huwa yanasababishwa na taka taka au vumbi linalopita katika tundu za pua na kuelekea katika mapafu, hii hutokana ikiwa pua itashindwa kusafishwa kila mara hivyo taka hubakia ndani ya pua na pua hushindwa kupokea taka nyengine.

Zabibu: Glassi moja ya zabibu changanya na kijiko kimoja cha asali tumia kwa muda wa wiki, inasemakana zabibu ni burudisho la mapafu.

Kwa wale wenye kifua kikavu basi Inshallah Lozi iwe dawa yao basi alazae lozi saba katika maji usiku wa kucha asubuhi atoe maganda yake ya uzisage uchanganye na siagi kidodo pamoja na sukari kidogo uwe unakula kijiko kimoja kikubwa kila siku asubuhi na jioni.

Maji ya kitunguu maji changanya na kijiko kimoja asali uweke katika chupa kwa muda wa masaa manne hadi matano, uwe unakunywa mara mbili kwa siku.

Kwa kifua kikavu: Chemsha maziwa glassi moja changanya na manjano acha ichimkie na baadae unywe.
Ikiwa kifua cha kuumia kwa kuanguka basi chukua manjano uchanganye na maji ya moto na umpake pale alipoumia.

Ikiwa ni kifua kinachotokana na hali ya hewa ya ubaridi basi uwe unakunywa juisi ya machungwa iliyozimuliwa kwa maji ya moto kila baada masaa mawili.

Pia jaribu kuacha sigara kama ni mvutaji au kukaa karibu na moshi wa aina yoyote ule, pia vitu vikali, nyama, soda pamoja na chai.
 
Nawashukuru sana ndg zangu, lakini nashindwa kuelewa Lozi na Manjano yakoje? ni matunda? na ntayapata wapi mkuu hapo Dar.
 
Pole sana mkuu! Ninajua tu maji mengi kunywa asubuh ama kufanya mapenz sana eti inasaidia sina uhakika lakini.
 
M2 wangu dawa ya mafua cjui kama ipo cjawahi ickia...lakini ukiwa na mafua mara nyingi unapewa vidonge vya usingizi 2.
 
Asikudanganye mtu, mafua hayana dawa. Hupona yenyewe na kadri kinga zako zinavyokuwa na uwezo mkubwa wa kupambana na vimelea vya magonjwa mwilini na kasi ya kupona haraka nayo huwa kwa kiwango cha juu. Kutuliza mafua makali tumia dawa za kutuliza maumivu kama pcm nk.
 
Dawa Ya Mafuwa Na Kichwa. Chukuwa Mafuta Zeti Zaituni (Olive oil)Fresh Tia Kidogo Katika Puwa Pakapaka Ndani Ya Puwa Yako Kabla Ya Kulala.

Kitunguu swaumu tangu kale kimekuwa kikijulikana kama 'dawa ya kushangaza' na kutumiwa na watu wengi katika kutibu mafua na influenza. Miongoni mwa faida za kitunguu swaumu ni kuzuia kupatwa na magonjwa mbalimbali na maambukizo ya virusi. Hivyo

kitunguu swaumu hujulikana kama antibiotiki ya asilia. Uchunguzi umeonyesha kwamba kula kitunguu swaumu kunapunguza kushadidi ugonjwa wa influenza na hata kuzuia kupatwa na ugonjwa huo. Vilevile kula kila mara kitunguu swaumu, huzuia

kupatwa na magonjwa ya moyo, kwani kitunguu swaumu huzuia damu isigande kwenye mishipa ya damu.

Halikadhalika kitunguu swaumu ambacho pia ni kiungo muhimu cha chakula kina potassium, na hivyo watu wenye ugonjwa wa

shinikizo la damu wanashauriwa kula vyakula vilivyopikwa kwa kitunguu swaumu.

Si vibaya kujua kuwa katika uchunguzi uliochapishwa mwaka 2001, imeelezwa kwamba, kitunguu swaumu kina athari kubwa na

nzuri pale kinapochanganywa na baadhi ya dawa nyinginezo katika kutibu Ukimwi au HIV.

Haya shime jamani… kuanzia leo vyakula visikose kuungwa na kitunguu thomu, iwapo unaogopa kupatwa na influenza kama mimi!

220px-Italian_garlic_PDO.JPG
 
pia unaweza tumia ephedrine nasal drops/spray,kunywa maji mengi kama mtaalamu alivyoshauri,acha kuvuta sigara wakati una mafua kwani inaongezea tatizo.
 
pia unaweza tumia ephedrine nasal drops/spray,kunywa maji mengi kama mtaalamu alivyoshauri,acha kuvuta sigara wakati una mafua kwani inaongezea tatizo.

mimi binafsi hii dawa huwa inanisaidia sana hasa kwa yale mafua yanayotiririka kwa huyakata kabisa ktk muda mfupi.na kama mafua yako yanatokana na allergy kama za vumbi,pafyum basi tumia dawa za allergy kama vile cetirizine,loratadine,desloratadine au piriton.hapo ni kwa mafua ya kawaida yaani common cold.lkn kama ni flu huo ni mziki mwingine na unahitaji uvumilivu kidogo kwani haitibiki kirahisi na mwisho wa siku huambatana na kikohozi kikali.
 
Ni kweli mafua (common colds) hayana dawa maana yanasababishwa na viruses.

Dawa nyingi zilizotajwa hapo juu ni just "symptomatic treatments", yaani zinapunguza dalili bila kugusa virus.

Konyagi au valuer au pombe yeyote kali inaweza kupunguza idadi ya virus maana inawaua, kwa hiyo kupunguza makali ya dalili
 
Huenda mafua yako yanatokana na allergy ndo maana yanakupa tabu kiasi hicho. Nakushauri kanunue dawa ya allergic flue inayoitwa syntrine (tablet).
 
Kwa mafua yanayosababishwa na allergy km vumbi,baridi.
Tiba yake ni kutumia dawa za kuondoa allergy km piriton,prednisolone,ephedrine, coldril etc.


Kwa mafua ambayo yanatokana na virus hayana tiba ya moja kwa moja,kinachotibiwa ni complications zake km homa /maumivu ya kichwa [utatumia antibiotics + antipains],kuyakata mafua yenyewe utatumia antiallergics kama hapo juu.

KUNYWA MAJI MENGI/ VINYWAJI BARIDI NI MUHIMU SANA KAMA TIBA YA ZIADA.

WATU WANAAMINI KUWA MAFUA HAYANA DAWA KWA SABABU: >>HAKUNA TIBA YA KUONDOA VIRUS COMPLETELY,LEO UTAMALIZA DOSE KESHO UKIWA EXPOSED UNAYADAKA.

>>HAKUNA DAWA YA KUWAUA VIRUS WA MAFUA.TIBA INATOLEWA KWA DALILI ZINAZOJITOKEZA. FINE ENOUGH VIRUS HAO HUPOTEA BAADA YA MUDA.
 
Nenda phamacy, zipo nyingi tu. Kila dawa inaponya tofauti kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Maumivu yakizidi kamuone daktari.
 
Back
Top Bottom