Ruge Opinion
JF-Expert Member
- Mar 22, 2006
- 1,838
- 701
Shirika la ndege ni zaidi ya kuwa na ndege. ATCL ilinyongwa kabisa pale walipolikabidhi kwa makaburu na South African Airways. Kutokana na njama chafu shirika lilipoteza njia (routes muhimu) lililokuwa nazo pamoja na haki za kutua kwenye viwanja muhimu kama Heathrow, London. Nadhani hata regional routes kama ya Johannesburg ilichukuliwa. Sasa hata shirika likipata ndege mpya litapata shida kupata na kushindana katika routes mpya. Na hiyo ni bila kutaja changamoto zingine kama kukosa karakana, wafanyakazi wazee/wachovu, taswira mbovu/hasi na ushindani katika sekta ya usafiri wa anga kwa sasa (angalia yanayotokea kwa Kenya Airaways, Precision Air na hata Fastjet). Mimi naunga mkono hoja ya kulivunja ATCL na kulipumzisha kwa amani. Kama ni muhimu kuwa na shirika la ndege la taifa kwa sababu za sifa (prestige) tuangalie uwezekano wa kuunga mkono sekta binafsi au ubia katika ya serikali na sekta binafsi (PPP). Kabla serikali haijakurupuka kuzika fedha zaidi katika ATCL inapaswa kujiuliza kwa nini sekta binafsi, amabayo husukumwa zaidi na kutengeneza faida, haijaona fursa katika soko ambalo ATCL inatarajia kulihudumia.Hakika hii ndio siasa ya maendeleo,umebainisha sababu nzuri.Ni kweli linahitaji jina jipya hasa ukizingatia serikali inalipa madeni yote,fikra mpya pia ni muhimu.
Hongera Comrade!