Nipo kwenye ndoa kwa miaka miwili sana na tuna mtoto mmoja mdogo. Tangu mwanzo wa ndoa yetu mume wangu amekuwa kama boss vile. Nilipata mimba mara tu baada ya kuolewa na mimba ilikuwa inanichosha sana maana ni mfanyakazi wa kuajiriwa.
Mume wangu mara nyingi alikuwa anatoka kazini kabla yangu na nikirudi namkuta amepumzika na mimi ndio naanza na mambo ya jikoni, tatizo ikifika tu saa moja na chakula hakijawa tayari anaanza kulalamika na kusema hajazoea kuchelewa kula, analalaamaa wee wakati nimefika nyumbani saa 12 kasoro na hakuwa tayari kusaidia lolote. Nikimuomba anisaidie anakuwa mkali na kusema yani unataka mimi niingie jikoni? kwa ukali! Ukichelewa tu kufua nguo zikawa nyingi kwenye tenga basi ni maneno meengi, mimba ikisumbua nikiwa sijisikii vizuri anasema najifanyisha kuumwa basi ikawa taabu tu.
Nikawa najitahidi sana kufanya majukumu yangu kama mke na kweli mambo ya chumbani yalikuwa si haba, ila kutokana na malalamishi yake na kutokuwa tayari kunisaidia taratibu nikawa nakosa hamu naye maana kila ninachofanya yeye alikuwa anatafuta kasoro. Tukiwa tunaenda mahali nikichelewa kujiandaa basi ni kugombezwa na kulalamikiwa. Mara nyingine ukiweka chakula mezani anakiangalia na kusema kwa ukali kuwa kwanini umepika chakula hiki tena mbele za watu tunaoishi nao wakati ukimuuliza nikupikie nini anasema chochote.
Siku nyingine nikiwa nataka kusoma kwanza kabla ya kulala namwambia nitaenda kulala baada ya masaa mawili nasoma kwanza mambo fulani basi anakuwa mkali kuwa mimi simuheshimu. Nimejitahidi kupuuzia maneno na matendo yake ili niweze kuwa na hisia kama mwanzo ila imeshindikana. Akisafiri najisikia huru sana maana akiwepo hata kuangalia tamthilia tu inakuw atabu. Najiona kama chombo tu cha kumfurahisha.
Moyo umekuwa mzito sana, nimebadilika na kuwa mwenye huzuni mara zote, na mwenye hasira zisizo na sababu hasa kwa dada wa kazi hadi naogopa sasa. Mume wangu nahisi amegundua hilo na anajaribu kujirudi ila kwa kweli moyo umekuw mzito sana, sex siku hizi imekuwa kutimiza wajibu na sijisikii tena furaha maana kila mara maneno yake ya kuumiza na vitendo vyake vinazunguka kny akili yangu. Niishie hapa maana siwezi andika vyote.
Nahitaji ushauri wenu wana jamii, natamani kusahau haya yote na kuanza upya.