Ushauri: Mwenyekiti CCM warudishe Nape na Makonda chamani

Methadone

New Member
Feb 22, 2017
3
0
Mwaka huu Chama chetu kikongwe kinaenda kufanya chaguzi mbalimbali kuanzia ngazi ya tawi mpaka taifa. Ni matarajio yangu wanachama wetu kwa ngazi zote watajitokeza kuomba ridhaa ya kuongoza Chama kwenye kipindi hiki chenye kauli mbiu ya "Hapa Kazi Tu". Hivyo ni matumaini yangu wagombea wote watakuwa na mtazamo na muelekeo wetu wa kuiifikia Tanzania mpya ya Viwanda.

Kilichonigusa mpaka kupandika uzi huu ni pamoja na mambo yanayoendelea sasa. Nakumbuka wiki mbili zilizopita pale Dodoma, ulituahakikishia wana CCM kuwa nafasi ziko nyingi tu. Ila ni rai yangu huyu kijana wetu mpendwa Paul Makonda naomba umludishe chamani tafadhali Mwenyekiti.

Kutokana na misuguano ya kimtazamo iliyopo kati ya wadau mbalimbali juu ya mpendwa wetu huyu. Kwasasa sioni kama atapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa watumishi anaowaongoza pamoja na wadau wa jiji la DSM. Najua Mwenyekiti wewe ndio unamtaka nani ufanyenae kazi na nani umtaki, wewe unajua nani akae wapi na nani asikae. Ila kwa hili mimi natoa kwa ajili tu ya afya kwa jiji letu la DSM.

Mwenyekiti, Paul Makonda amekuzwa ndani ya CCM kimkakati zaidi, rejea jumuiya ya vijana UVCCM. Katika jumuiya hii kijana huyu alikuwa ni kijana wa kupanga mikakati mingi iliyosaidia kuinua hali ya Chama kwa vijana hasa kupitia vyuo vikuu. Kijana huyu alikuwa mstari wa mbele kabisa kupambana kwa wale aliwaita vibaraka wa ufisadi - Mgeja na mwenzake ambao bado kesi yao inaunguruma mahakamani, pia alidiliki kumsema mgombea wa UKAWA wakati akiwa CCM waziwazi. Hivyo kwangu ni mtu ambae anakijua Chama na kama unavyosema mwenyewe kuwa ni mchapa kazi hodari. Pia alisaidia kuzima mijadala mbalimbali ambayo kwa namna moja ikasaidia mapendekezo ya Katiba mpya yabaki na Jamhuri na SMZ.

Hivyo nafikiri kijana huyu ukimludisha chamani bado ataendelea kukufaa zaidi kulivyo alipokuwa sasa kwani nafasi aliyopo imeshaingia shubiri. Huku chamani sisi hatuna shida na Elimu kwani tunachoangalia sisi ni chama kwanza mtu baadae. Mifano huku chamani ipo, rejea Bulembo na Msukuma hawa ni viongozi wetu wa chama lakini wamepewa nafasi bila ya kujali Elimu yao.

Mwenyekiti, kwasababu mpendwa wetu Paul Makonda bado unamuhitaji ni vyema ukamludisha chamani. Nafasi ya Katibu Mwenezi wa Chama chetu ingemfaa sana mpendwa wetu huyu. Kwangu nafasi hii imepwaya sana baada ya kutoka Nape. Paul Makonda kama nilivyosema awali ni kijana wa mikakati ambayo mingine umeshuhudia wewe mwenyewe, kwani Katibu Mwenezi wa sasa bado chamani hakubaliki (mtazamo), kwanza kwa msimamo wake wa Serikali Tatu na pia huyu mtu ni mgeni chamani.

Mwenyekiti nikirejea kwa Komredi Nape, yeye nadhani umeona utendaji wake akimsaidia Katibu Kinana. Yeye amethubutu kuisema Serikali iliyopita na watendaji hadharani kwa kuiona kuwa kuna watu mizigo wakiwemo Mawaziri. Huyu nae amezunguka Tanzania nzima kufufua uhai wa Chama. Amefika kila pembe ya nchi yetu kuona wanachama na kuongea nao, pia walisaidia kutoa maelekezo ya chama kwa viongozi wa Serikali.

Vilevile kumbuka Mwenyekiti, Nape ni mmoja kati ya mtu aliyezuia mafuriko kwa mikono, pia alisema waziwazi kuwa mtu asiyefuata utaratibu wa chama watamkata. Pia sina shaka kama utampatia Ukatibu Mkuu wa Chama atakusaidia sana kwani nae ni mmoja wa watu wanao kijua chama. Mtu huyu pia ni mpambanaji hasa rejea harakati za Uchaguzi 2015.

Mwisho, Mwenyekiti naomba tuanze sasakujenga chama kwa kuanza na sisi mikutano yetu ya ndani kwa wanachama wetu kwani vidonda ni vingi, tukikaa sana bila ya kuviponya vitaoza.

Pia rejea hotuba ya Mwenyekiti aliyepita, kuwa tusijisahau sana kuna mtu upande wa pili anajipanga usiku na mchana, tusijekushtuka kumekucha.

Wasalaam

Methadone.
 
Wewe movie ipo katikati hiyoo

It is TOO LATE.....wacha movie iendelee
 
Nape ni kenge kwenye msafara wa mamba, ni mtu wa kuangaliwa kwa umakini dhidi ya anachokifanya. Walioko nje tunamwona Nape kama mpambanaji dhidi ya system. Sijuhi anapambana na nani na kwa masrahi ya nani, hatuelewi ila tunaamini muda ukifika kila kitu huwekwa wazi.

Kupambana si tatizo lakini kupambana dhidi ya wenzio inatia tafrani, mapambano mema ni kuwapambania ulionao katika hari yoyote ile iwayo. Mliokubaliana kwenda wote hamna haja ya kupambana, mnahitaji kushauriana. Na ukitaka kupambana unageuka mkuki, ni sharti ujitenga nao. Kama nia ni kuonekana ni mpambanaji ni vizuri akae upande wa kimapambano ili ifahamike ni adui kuliko kuwa naye halafu akawageuzia mishale kuwachoma
 
Acha movie iendelee na arosto za mateja wakiwa wanaendelea kupambana na Methadone.......!! Hamna namna wala jinsi
 
Nape ni kenge kwenye msafara wa mamba, ni mtu wa kuangaliwa kwa umakini dhidi ya anachokifanya. Walioko nje tunamwona Nape kama mpambanaji dhidi ya system. Sijuhi anapambana na nani na kwa masrahi ya nani, hatuelewi ila tunaamini muda ukifika kila kitu huwekwa wazi.

Kupambana si tatizo lakini kupambana dhidi ya wenzio inatia tafrani, mapambano mema ni kuwapambania ulionao katika hari yoyote ile iwayo. Mliokubaliana kwenda wote hamna haja ya kupambana, mnahitaji kushauriana. Na ukitaka kupambana unageuka mkuki, ni sharti ujitenga nao. Kama nia ni kuonekana ni mpambanaji ni vizuri akae upande wa kimapambano ili ifahamike ni adui kuliko kuwa naye halafu akawageuzia mishale kuwachoma

Leo unamuita Nape kenge? Uyu ndie aliemuweka Magufuli hapo alipo.
 
Makonda ni Mpuuzi sana hajui tulivyopata Shida kutetea Chama.

Wilaya yake ya Kinondoni akiwa DC kwny Uchaguzi wa 2015 alishindwa kupigania hata Jimbo moja yote yalienda Ukawa kuanzia Kwe, Ubungo, Kinondoni na Kibamba na hata Madiwani wengi tulipoteza na Taarifa nyeti zinasema alishiriki kuhujumu Chama kwa Kuhongwa na Ukawa inashangaza yeye hakufukuzwa Chamani Kama kina Sophia Simba kwani hata Matokeo ya Urais Kinondoni Rais wetu Kipenzi alipigwa Mweleka sasa hapo Makonda alikuwa na Msaada gani kwa Chama na Rais Mwenyewe?

Akina Nape na Sisi tulipanda na kushuka kupigania Chama, JPM kazi yake ilikuwa kuja uwanjani Kama Jamhuri Morogoro au Mwanza anakuta Uwanja umetapika hajui Ugumu wala namna ya kukusanya Wasikilizaji. Kuhutubia Mkutano sio kazi hata Wema Sepetu au Lemutuz wanahutubia kazi ni kukusanya wa kuwahutubia.

January Makamba na Nape wamefanya kazi kubwa sana sana lakin Leo hii wanaonekana Takataka mbele ya Makonda.

Mwenykt wetu Rais Magufuli kishasema walioshindwa kusaidia Chama kwny Uchaguzi 2015 mpaka tukakosa Majimbo na Kata kadhaa hataki awaone wanachukua Form, Hatutegemi Paul Makonda achukue form ya kuwania chochote kwny Chama kwny Chaguzi ngazi mbalimbali Mwaka huu kwani alisaidia na alihujumu sana Chama kishindwe.

Iddy Azzan Kama sio uoga wa Kurudishwa Rumande kwa igizo la Madawa ya kulevya Ana Mengi sana Kifuani kumhusu Daudi, Rais ikimpendeza amwite afunguke Mengi!
 
Magufuli hawezi kuwasikia watu kama nyie anamsikiliza bashite wake tu ambaye muda si mrefu he is going to fall in the toilet when bashiteling!!
 
Mkuu Methadone una point!! Makonda arudishwe chamani,ila asipewe nafasi kubwa kwanza bali awekwe mahususi kwa ajili ya kufundwa,kumlinganisha Mh Nape Na makonda kuna kasoro,Nape ametokea jikoni! Amepikwa akaiva,amekipigania chama bila kujijeruhi! Amepigana front line at the moment when the fighting was fierce! Amekivusha chama kipindi kigumu mno kwa kutumia hekima ambayo makonda hajabahatika kuwa nayo,hata sasa roho inamuuma zaidi kwa kuona kuwa mtu wa aina ya makonda anakirudisha chama kwenye hali ile mbaya ya kuchukiwa kwa sababu y Matendo binafsi ya baadhi ya makada wake waliokosa weledi! Kama issue ndogo tu ya clouds imemsukuma makonda kuburuza majeshi yenye silaha nzito(kupambana na watangazaji wa Shilawadu wenye microphone tu)ingekuwaje kama angekuwa na jukumu la kupambana na wanachama milioni sita wa chadema nchi nzima? Vifaru na jet fighters si vingetanda mitaani nchi nzima? Maiti si zingezikwa kwa makatapila? Tuache utani!! Labda kama nia yako ni kuua chama,hivi unategemea Makonda kwa akili zake zile anaweza kufanya kazi na mtu smart kama Kinana?kama Nape nnauye? Si kuhamishia ugomvi wa mbwa chumbani kwako? Siipendi ccm!! Ila wewe utakuwa huipendi kuliko mimi!
 
Makonda ni Mpuuzi sana hajui tulivyopata Shida kutetea Chama.

Wilaya yake ya Kinondoni akiwa DC kwny Uchaguzi wa 2015 alishindwa kupigania hata Jimbo moja yote yalienda Ukawa kuanzia Kwe, Ubungo, Kinondoni na Kibamba na hata Madiwani wengi tulipoteza na Taarifa nyeti zinasema alishiriki kuhujumu Chama kwa Kuhongwa na Ukawa inashangaza yeye hakufukuzwa Chamani Kama kina Sophia Simba kwani hata Matokeo ya Urais Kinondoni Rais wetu Kipenzi alipigwa Mweleka sasa hapo Makonda alikuwa na Msaada gani kwa Chama na Rais Mwenyewe?

Akina Nape na Sisi tulipanda na kushuka kupigania Chama, JPM kazi yake ilikuwa kuja uwanjani Kama Jamhuri Morogoro au Mwanza anakuta Uwanja umetapika hajui Ugumu wala namna ya kukusanya Wasikilizaji. Kuhutubia Mkutano sio kazi hata Wema Sepetu au Lemutuz wanahutubia kazi ni kukusanya wa kuwahutubia.

January Makamba na Nape wamefanya kazi kubwa sana sana lakin Leo hii wanaonekana Takataka mbele ya Makonda.

Mwenykt wetu Rais Magufuli kishasema walioshindwa kusaidia Chama kwny Uchaguzi 2015 mpaka tukakosa Majimbo na Kata kadhaa hataki awaone wanachukua Form, Hatutegemi Paul Makonda achukue form ya kuwania chochote kwny Chama kwny Chaguzi ngazi mbalimbali Mwaka huu kwani alisaidia na alihujumu sana Chama kishindwe.

Iddy Azzan Kama sio uoga wa Kurudishwa Rumande kwa igizo la Madawa ya kulevya Ana Mengi sana Kifuani kumhusu Daudi, Rais ikimpendeza amwite afunguke Mengi!
Pohamba Bravo!! Katu msikubali mpuuzi wa aina ya bashite azike spirit yenu ya kukipigania na kukiweka chama karibu na Watu!! Hajui jasho mlilomwaga kupambana nasi humu mitandaoni!hajui miiba iliyochoma visigino vyenu kuhangaikia chama kilichochakaa kionekane kipya mbele ya wapiga kura! Eti baada ya jitihada zenu zoote ndiyo atokee kichaa mmoja atake kuhodhi matunda ya jasho lenu?kama mbwai iwe mbwai!! Mkataeni hadharani!! Yeye na yeyote aliye nyuma yake!
 
Back
Top Bottom