Ushauri: Meya wa Kinondoni atoke CUF

njundelekajo

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
310
227
NASHAURI,MEYA WA KINONDONI ATOKE CUF.

Tarehe 16/9/2016 baraza la madiwani manispaa ya kinondoni lilivunjwa rasmi kutokana na takwa la kisheria.(sheria ya serikali za mitaa namba 8 ya mwaka 1982).Sheria hii inazuia wilaya mbili kua chini ya almashauri moja.Hivyo Ubungo na Kinondoni zinapaswa sasa kua lamshauri mbili chini ya wilaya moja ya kinondoni.

Mabadiliko haya yametoa nafasi pia ya kufanyika upya kwa uchaguzi wa nafasi ya umeya kwa kwa mansipaa zote mbili, mpya ya ubungo na ile ya zamani "iliyomegwa" kutoka kinondoni.

kwa maoni yangu chadema HATUPASWI KUTOA MAMEYA KWENYE MANISPAA ZOTE MBILI na chama ambacho kipo ndani ya UKAWA chenye kustahili "kuachiwa" manispaa mojawapo ni chama cha CIVIC UNITED FRONT(CUF), ifuatayo ni orodha ya sababu ya kwa nini CUF na kwa nini tuache manispaa mojawapo:-

1.Kwenye makubaliano ya mgawanyo wa UKAWA, majimbo ya uchaguzi wa mwaka 2015 upande wa Tanzania bara CHADEMA ilichukua 54% ya majimbo yote na CUF 39% , kwa upande wa Zanzibar iliachiwa CUF kwa zaidi ya karibia 100% KWAKUA CUF ILISUSIA UCHAGUZI WA MARUDIO haikuwezekana kupatikana kwa "compasation" kama ilivyotaraijwa hivyo CUF haikufukia malengo yake kupitia mgawanyo ule.

2.Ni lazima ukawa uimarike hata kwa kupoteza,CUF ndicho chama kinachoonekana "kupoteza" zaidi ili kuulinda UKAWA.Hata vurugu za wakati huu kumkataa mwenyekiti wao aliyejiudhuru Prof Lipumba ni munedelezo wa hayo..kumkubali lipumba ni kuua UKAWA hivyo basi ni wakati wa CHADEMA SASA KUUPOTEZA UMEYA KWA MOJA YA MANISPAA KWA KUTOTOA MGOMBEA NAFASI YA UMEYA japo ina madiwani wengi huko kuliko CUF.

3.Kuuondoa picha inayojaribu kujengwa kwamba UKAWA ni CHADEMA na CHADEMA ni UKAWA ni vyema CHADEMA ikashiriki "kuua"mtazamo huu kwa kukubali kutoa makamu meya ,kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza mojawapo ya manispaa kwa UKAWA kama C.C.M wakiamua kuikuza HOJA hii ikiwa CHADEMA watatoa wagombea manispaa zote mbili.

4.CUF ndicho chama pekee ndani ya UKAWA ukiacha Chadema chenye madiwani kwenye almashauri zote mbili.Hivyo kina sifa ya kutoa mgombea wa umeya kama ambavyo Chadema ilivyo.

5.Pamoja na kwamba inaonekana CHADEMA ina madiwani wengi,lakini ushindi wa nafasi za umeya kwa manispaa za Dar-es-Salaam ulichangiwa sana na "uaminifu" wa madiwani wachache wa CUF .Ikumbukwe CUF ilipoteza jimbo la Segerea kwa katika mazingira ya kutoaminiana (mgombea wa CUF alipata 33% wa chadema 21% na wa C.C.M 41%) kwa kiwango cha uelewa hasa wa watu wa Dar-es-Salaam kuhusu UKAWA ni ngumu kuamini mgombea wa CHADEMA lipata 21% bila kufanya kampeni.

N.B Manispaa ambayo CHADEMA inapaswa kuiachia CUF ni manispaa ya KINIONDONI kwakua Boniface Jacob aliyekua meya kwenye manispaa ya kinondoni anatarajiwa kugombea nafasi hiyo kwenye manispaa ya UBUNGO hivyo ni vyema akaachwa kuendelea ama demokrasia ndani ya chama ikiamua vinginevyo.

NGUZO NOEL.R.
 
Chadema hawawezi kukubali... Wameshampitisha Eng. Muro kuwania Umeya Kinondoni...

CUF walikubali kuingizwa mkende... Sasa chama kinaelekea kufa....
 
Back
Top Bottom