Ushauri Kwa Wabunge: Kabla ya Kupitisha Bajeti ya Wizara, Waziri Husika Aje na Majibu ya Hoja ya CAG kwenye Wizara Yake

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,049
49,731
Bunge ndio chombo pekee ambacho kina mamlaka ya kuisimamia na kuiwajibisha Serikali.

Badala ya kupiga makelele ya jumla jumla yasiyo ya Kimkakati,hakikisheni mnafanya hivyo.

Rais alishasema wahusika wapishe au majibu yaletwe kabla ya Bunge kuanza na hapa muanze na Tamisemi Jumanne ijayo.

Mh.Spika hakikisha Kila Waziri anaekuja kusoma Hotuba ya Bajeti yake aje na majibu ya hoja za Ufisadi kwenye Wizara husika la sivyo Bajeti isipotishwe na Waziri husika achukukiwe hatua ikiwamo kufukuzwa..

Hakuna Wizara hata Moja ambayo Haina hoja za CAG,hatuwezi kuwa tunapayuka bila kwenda Kimkakati..
 
Hakuna lolote, mwisho wa siku bajeti itapitishwa pamoja na kwamba hao wabunge watajidai "kuwabana" hao mawaziri.

Hilo bunge ni la watu wasiojitambua, ni kama wanasesere wa Rais, badala wao wamuagize Rais afanye jambo, wao ndio wanageuka watoto kuagizwa na Rais.

Ndio maana nawashangaa wale wanaolazimisha tuamini ripoti ya CAG kwanza lazima ipelekwe bungeni kujadiliwa, ndio hatua dhidi ya wezi zichukuliwe...

Hayo ni maandishi tu kwenye makaratasi mnayoyaita "sheria", lakini kiuhalisia hali ya mambo field haiko hivyo.

Rais ndie kalibeba bunge mgongoni mwake, hivyo anastahili lawama zote, huu ndio ukweli, tusidanganyane kwa uongo mwingine wowote, anapoamua kukaa kimya, basi na ajue yeye ndie anayetuangamiza.
Screenshot_20230407-052209_Gallery.jpg
 
Unaionaje Ccm?
Unachosema Hakipo Ccm Ni Ile Ile Hapo Wenyewe Wanasema Tonge La Mwisho Ndiyo La Kukomba Mboga Zote Kwenye Bakuri Uelekeo 2025 Kuchota Kura Kubaki Kwenye Maeneo Yetu
 
Bunge ndio chombo pekee ambacho kina mamlaka ya kuisimamia na kuiwajibisha Serikali.

Badala ya kupiga makelele ya jumla jumla yasiyo ya Kimkakati,hakikisheni mnafanya hivyo.

Rais alishasema wahusika wapishe au majibu yaletwe kabla ya Bunge kuanza na hapa muanze na Tamisemi Jumanne ijayo.

Mh.Spika hakikisha Kila Waziri anaekuja kusoma Hotuba ya Bajeti yake aje na majibu ya hoja za Ufisadi kwenye Wizara husika la sivyo Bajeti isipotishwe na Waziri husika achukukiwe hatua ikiwamo kufukuzwa..

Hakuna Wizara hata Moja ambayo Haina hoja za CAG,hatuwezi kuwa tunapayuka bila kwenda Kimkakati..
Spika akisimamia haya, atakuwa amejijengea heshima kubwa sana
 
Back
Top Bottom