Ukweli mtupu kuhusu Wizara ya Fedha baada ya kusikiliza bajeti ya Wizara hiyo

Deodravis

New Member
Jul 27, 2022
2
0
BAADA YA KUSIKILIZA BAJETI YA WIZARA YA FEDHA LEO NIMEGUNDUA MAMBO MATANO MAKUBWA.

Na wengi huenda huwa tunaitupia bure mawe wizara hii.

Kivipi?

JITAHIDI USOME UZI HUU MPAKA MWISHO.

Kati ya wizara ambazo zinapigwa mawe nchini basi wizara ya fedha inaongoza. Kwa sababu ndio wanasimamia sera za kodi, Wanakusanya mapato, Ndio wakopaji, Ndio walipa madeni, hivyo lawama dhidi yao haziepukiki.

Lakini.

Nilikua na hamu ya kusikia makadirio ya bajeti ya wizara hii kwa hamu ili nijiridhishe na hiki nachoenda kukizungumza na hatimae leo nimejiridhisha na kwa bahati nzuri nilikuepo mjengoni kabisa.

NIMEGUNDUA KUWA

1. WIZARA HII INA MAJUKUMU MAKUBWA MNO KULIKO HATA RASILIMALI WATU ZILIZOPO WIZARANI.

Kusimamia bajeti, Kuandaa bajeti, Kukusanya kodi na kutafuta wahisani (mikopo na misaada) namaanisha kutafuta mapato ya kutosha matumizi yote ya serikali na maendeleo kisha ukiringanisha na
Idadi ya rasilimali watu waliopo wizarani aisee majukumu haya ni makubwa sana zaidi ya idadi yao.

2. MITAANI TUNAIBEBESHA LAWAMA NYINGINE AMBAZO HAZIWAHUSU MOJA KWA MOJA.

Kwa mujibu wa makadirio haya maana yake wizara hii haisimamii miradi yoyote isipokuwa ile ya kikodi.
Nasema hawahusiki moja kwa moja kwasababu wao hutoa tu fedha ila miradi inasimamiwa na wizara husika. So kutupia lawama za Reli, Ujenzi fulani, miradi ya nishati nk moja kwa moja kwa @mofURT ni kuwaonea sana

3. WIZARA HII MIANYA YA UPIGAJI KWAO NI MIDOGO SANA.

Ndio namaanisha ni midogo mno. Ukiniuliza kwanini nitakwambia.

i. Mfumo wa sasa wa ukusanyaji kodi TRA ni wa kimtandao. So ukilipa kodi moja kwa moja inaenda account ya serikali kupitia mifumo ya GePG n.k

ii. Mikopo ikiingia inaingia kwenye account ya serikali na siyo za wizara ya fedha. Na data base inaonwa na serikali kuu.

SASA NIAMBIE KWA HALI HIYO MIANYA YA UPIGAJI SI NI FINYU SANA. So ili wapige inabidi watumie nguvu kubwa tofauti na wizara nyingine ambazo
Hupokea fedha toka wizara ya fedha ili wakatekeleze miradi yao kupitia wakandarasi walioingia mikataba nao.

4. WIZARA HII INAANDAMWA NA CHANGAMOTO ZA WATU KUTOKUWA NA ELIMU

Watanzania wengi hawana elimu ya kikodi na hawajui majukumu ya hizi wizara zetu. Kuanzia elimu ya kikodi na hizi za kimajukumu basi watu hawa ni rahisi kutoelewa mipango mikakati ya wizara na sio hii tu.

Na kuishia tu kulaumu kila kitu. Na ndio maana Leo wakati Mhe. Nusrat Anje Mb Viti maalumu Chadema akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ametoa maoni kuwa Wizara iwekeze katika kutoa elimu ili kila mtanzania ajue kuwa kulipa kodi ni wajibu wake. Ingawa ni jukumu pia la wizara.

Kuweka mazingira bora kwa walipa kodi. Hivyo kama kila mtanzania atakua na uelewa juu ya haya mambo basi wizara hii tutaielewa sana.

5. JUHUDI KUBWA ZA WIZARA HII ZA KUKUZA UCHUMI ZINARUDISHWA NYUMA NA UBADHIRIFU NA URASIMU KATIKA UTEKELEZAJI.

Ukitazama taswira ya bajeti hii. Na utagundua kuwa muelekeo wa uchumi wa nchi uko katika mstakabali sahihi. Ingawa tunasubiri pia bajeti kuu kuona muelekeo wa jumla.

Lakini hali kama hii na mstakabali huu bila kupepesa macho unarudishwa nyuma na ubadhirifu unaofanywa kwenye miradi. Hali inayotoa feedback mbaya wa walipa kodi kuona kuwa kodi wanayolipa inaishia kweye mikono ya watu wachache. Na inashawishi ukwepaji wa kodi pia.

NATAKA KUSEMA NINI?

Licha ya kuwepo elimu kuanzia ndani ya bunge. Nikikumbuka alichokisema naibu spika leo wakati anahairisha bunge kwa kuwapongeza wabunge kwa kutoa hoja sahihi dhidi ya wizara. Hii inaonesha kuwa tayari elimu ya majukumu ya hizi wizara ipo ndani ya bunge.
HIVYO BASI.

Katika nchi hii huru hatuzuiwi kukosoa na kutoa maoni lakini ni vema kufanya utafiti juu ya vitu tunavyovikosoa na kukosoa kwa watu sahihi na kwa namna sahihi. .

Nihitimishe kwa kutoa pongezi kwa Wizara ya fedha @mofURT inayoongozwa na Dkt Mwigulu Nchemba. PhD kwa kazi waliyoifanya katika kuandaa bajeti waliyoiwasirisha leo na wanayoendelea kuiandaa kuelekea bajeti kuu na kwa kuahidi kuyafanyia kazi Maoni yaliyotolewa leo.

MWISHO WA UZI.

IMG_20230607_140654.jpg
IMG_20230607_140810.jpg
 
Back
Top Bottom