Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Naomba kutoa ushauri kwa uongozi wa halmashauri za majiji yote ya Tanzania, na ikiwezekana hata mikoa na wilaya.
Zitungwe sheria kwamba nyumba yeyote iliyoko ndani ya eneo la jiji au mjini, kila baada ya miaka mitano ni lazima ipakwe rangi ya paa (roof paint) ili kupendezesha mji na pia kuendana na mazingira.
Kwa mfano hapa Dar, ukiwa unatua kwa ndege, Dar es Salaam inaonekana chafu sana kwa juu, na tatizo ni mabati ambayo yameathiriwa na kutu.
Halmashauri za majiji na miji zinaweza kuamua utaratibu wa rangi uweje, labda kutegema eneo.
Na sisi watu binafsi tuliojenga mijini, basi ukiwa na nyumba ya bati jitahidi angalau uipake rangi ya bati kama bati zako sio za rangi. Tusingoje kusukumwa na sheria.