Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,760
- 41,624
Kuna kelele nyingi za wanafiki kwako Mh. Membe. Lililo jema ni kwamba unaufahamu sana unafiki wao.
Manabii wa kweli wa Mungu, tangu historia, na tangu kale, wanafahamika kwa kusimama na kuusemea ukweli. Hawakujali nini kitawapata kwa kuwa wakweli. Walismama imara hata dhidi ya wafalme wenye nguvu na wenye mamlaka ya kutisha.
Tuwaulize viongozi wetu wa dini, wakati watu wakishambuliwa kwa risasi, wakiuawa, wakitekwa, wakiporwa mali zao, wakibambikiziwa kesi na kutupwa magerezani kwa uonevu, wao waliokuwa wapi? Walisimama upande upi? Walinena nini juu ya uovu ule?
Mungu aendelee kusimama na viongozi wa dini waliokemea na wanaoendelea kukemea uovu, wanaoutumikia ukweli, kwa sababu Mungu wetu ni Mungu wa ukweli, ni Mungu wa haki.
Ushauri wangu kwako Membe, ili usiendelee kusumbuliwa na watu wanafiki wanaojifanya wana hekima leo, lakini walijifanya vipofu na mabubu wakati uovu unatendeka, toa tamko kuwa iwe ni ofisini kwako, nyumbani kwako au mahali pengine popote, hutaki kutembelewa na mtu yeyote mnafiki ambaye anakuja eti kumwombea msamaha Musiba.
Ikikupendeza ruhusu tu kujadiliana na watu wenye hekima, watu ambao maisha yao yamejawa na kusimama katika ukweli bila ya kujali watawala watanena nini.
Lakini ufahamu kuwa ule uchafuzi wa haiba za watu, uhamasishaji wa watu kuuawa na kufungwa ulikuwa ni mradi uliohusisha watu wengi, mbele wakiwa wamemsimamisha Musiba, wao wakiwa nyuma yake. Hao waliokuwa nyuma yake, wengi wao ndio watakuja sasa na kujifanya washauri wa kukutaka umsamehe Musiba. Na wengine kwa vile hawawezi kukyfikia, wanawatumia viongozi wa dini wanaoamini wanaweza kuwatumia.
Ukweli ni kwamba watu hawa hawaombi umsamehe Musiba kama mtu tu, bali umsamehe mwenzao ambaye walimweka mbele na wao wakiwa nyuma yake. Hawa wanataka kujitoa kwenye mazingira ya kulaumiwa na Musiba ambaye anawaona wamemsaliti kwa kutomsaidia nyakati hizi. Ukimwachia huyu mhalifu, hawa wahalifu wenzake watakwenda na kumwambia kuwa tumefanya kazi, tumekusaidia mpaka umekuwa huru sasa. Mbinu yao kubwa waliyoibuni kwa sasa ni kuwatumia viongozi wa dini ambao wwanawafahamu kuwa kwa namna fulani walikuwa nao katika katika hali ile ya kuulinda uovu.
Waliokuwa na Musiba, wamsaidie Musiba kulipia uovu wake, maana wao ni sehemu yake katika uovu wake. Na baadhi ya watu ambao sio waovu, na hawakuwahi kuwa waovu, wawe na hekima siyo kukubali maombi ya watu hovyo hovyo, hata wakaharibiwa heshima zao kutokana na kutumika na hao waovu wa kundi la Musiba.
Mpaka sasa si Musiba binafsi ndiye anayewaona viongozi wa dini kumwombea msamaha Musiba, bali ni watu wale wenzake na Musiba ndio wanaoenda kwa hao viongozi wa dini.
Mh. Membe, ujaliwe hekima katika hili.