Ushauri kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
18,511
68,141
Salaam.

Nimepata wazo la kumshauri Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Mheshimiwa Tundu Lissu juu ya taarifa zake anazotoa kuwalenga baadhi ya viongozi wa serikali ya CCM, hasa awapo kwenye majukwaa ya siasa.

Jambo lililonisukuma zaidi kutoa ushauri huu, ni baada ya Lissu, jana akiwa kwenye mkutano wa siasa, kutoa madai kumhusu aliyekuwa Rais wa Tanzania, awamu ya tano, Marehemu John P. Magufuli.

Lissu kwenye mkutano huo alidai kwamba, Marehemu Magufuli alikutwa na kiasi kikubwa cha pesa nyumbani kwake, takriban dola za kimarekani milioni 42, ambazo ni sawa na Tsh.bilioni 100 za kitanzania.

Madai haya nikiyatazama kwa makini, nayaona yana tofauti kubwa na mengine yanayohusu mkataba wa hovyo wa bandari, mkataba ambao wengi wetu tumeuona, hivyo kusema neno lolote kali kuhusu mkataba ule, sio mbaya kwasababu ushahidi wake upo hadharani.

Lakini madai ya kumhusu Marehemu Magufuli, haya Lissu ameyatoa naamini kwa kuzingatia zaidi maneno ya kuambiwa, na bahati mbaya zaidi, hao waliomwambia juu ya hili ni wana CCM, ambao either wako idara ya Usalama, au huko chamani.

Hawa wanajua siku zote, jukumu lao la kwanza, lililo muhimu zaidi kwao, siku zote ni kulinda maslahi ya chama chao, hivyo wako radhi kufanya chochote ili kuhakikisha wanalinda heshima ya chama chao, na viongozi wao.

Sasa kwa hali hiyo, endapo Lissu atatakiwa kuthibitisha mahakamani juu ya madai yake kumhusu Marehemu Magufuli, na ushahidi wake akataka kuupata toka kwa hao hao CCM, ambao wamekuwa wakimpa taarifa nyeti kwa siri, naanza kuona Lissu anaweza kujikuta mtegoni mbele ya safari.

Mahakamani siku zote tunatakiwa ku prove beyond reasonable doubt, huwezi kumtuhumu Magufuli kisha utetezi wako uegemee kwenye upotevu wa pesa za Plea Bargaining, au kwenye uporaji waliofanyiwa wamiliki wa Bureau de Change, kama ambavyo nimeona wengi wetu humu wakiutumia.

Kufikia hapo, CCM wanaweza kumuwekea mtego Lissu, kisha wakafanikiwa kummaliza kabisa kisiasa, pale ambapo ushahidi atakaoutaka ili kuutoa mahakamani, hao rafiki zake wa CCM watakapogoma kumpa ushirikiano, kwa kuogopa wasijulikane kwa wakubwa zao.

Namshauri Lissu awe makini na maneno ya kuambiwa kisha kuyatoa majukwaani, sio kwa hili la Magufuli pekee, bali hata na mengine yajayo, ahakikishe kabla hajazungumza anakuwa na ushahidi wa kutosha mezani, ili endapo akitakiwa kuupeleka mahakamani, iwe rahisi kwake kufanya hivyo.

Naandika haya nikijua fika Lissu ni mwanasheria mzuri, tena mwenye uzoefu wa kutosha mahakamani, lakini waswahili husema ndege mjanja siku zote hunaswa na tundu bovu, akumbuke yupo kwenye mchezo wa siasa, mchezo ambao hauna rafiki wala adui wa kudumu, rafiki wa leo, kesho anaweza kugeuka adui yako.

Pia soma: Lissu: Dola za Kimarekani Milioni 42 (takribani Tsh. Bilioni 100) zilikutwa nyumbani kwa Magufuli baada ya kufariki
 
Kamshitaki mahakamani,uiombe mahakama imwamuru alete ushaidi
Mimi nimetoa ushauri kwa mtu anayeonekana thamani yake kwa watanganyika ipo juu, hasa kwa aina ya siasa anazofanya, kutoficha kitu.

Muhimu ajue tu, kwa kadri anavyoongeza uungwaji mkono, pia ndio mbinu za kummaliza zinaweza kuwa zinapangwa chini chini dhidi yake.
 
Unadhani hajui anachokifanya? Nendeni Mahakamani mkaombe ushahidi.
Halafu anapiga kotekote, akipiga huku Chawa wanalia, halafu lile genge linahisi limepata fimbo ya kumchapia mama na chawa wake, wanaanza kujisogeza kwa Lissu, na wenyewe anawaponda.
Kwa kifupi Lissu hana rafiki, ukichagua ukweli ndiyo mnaweza kuwa marafiki.
Kwa sasa upande mmoja kuna CCM halafu upande mwingine kuna Lissu.
 
Mimi nimetoa ushauri kwa mtu anayeonekana thamani yake kwa watanganyika ipo juu, hasa kwa aina ya siasa anazofanya, kutoficha kitu.

Muhimu ajue tu, kwa kadri anavyoongeza uungwaji mkono, pia ndio mbinu za kummaliza zinaweza kuwa zinapangwa chini chini dhidi yake.
Binadamu yeyote ana mazuri na mapungufu, hivyo kwenye mazuri ya Magufuli tuache yasemwe na kwenye maovu yake yasemwe pia!.
 
Salaam.

Nimepata wazo la kumshauri Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Mheshimiwa Tundu Lissu juu ya taarifa zake anazotoa kuwalenga baadhi ya viongozi wa serikali ya CCM, hasa awapo kwenye majukwaa ya siasa.
Mkuu, Lissu ni mastermind.

Mara nyingi kama siyo mara zote huwa hazungumzi jambo kama hana backup ya ushahidi.

Lissu ni mtu wa kuzichanga karata zake vizuri mno akitaka kuzungumza hadharani swala lolote la Kitaifa.

Kwenye uzi wako ni kama umeshahitimisha kabisa kwamba jamaa hana ushahidi wa tuhuma alizozitoa dhidi ya Magufuli.

Ingawa siiungi mkono hiyo kauli yake dhidi ya marehemu tena ambaye yuko kaburini na hawezi kujitetea, hoja yangu ni kwamba TAML ni mtu makini sana.

Niwatikie j2 njema.
 
Unadhani hajui anachokifanya? Nendeni Mahakamani mkaombe ushahidi.
Halafu anapiga kotekote, akipiga huku Chawa wanalia, halafu lile genge linahisi limepata fimbo ya kumchapia mama na chawa wake, wanaanza kujisogeza kwa Lissu, na wenyewe anawaponda.
Kwa kifupi Lissu hana rafiki, ukichagua ukweli ndiyo mnaweza kuwa marafiki.
Kwa sasa upande mmoja kuna CCM halafu upande mwingine kuna Lissu.
Hapa ndio nikatoa mfano pia, kupiga upande wa mama hasa kwenye suala la bandari naona ushahidi anao, ule mkataba wa hovyo wa bandari.

Lakini kupiga upande wa hilo genge, kwa maneno matupu, ndipo nimemtaka awe makini, ahakikishe anakuwa na ushahidi wa kutosha mezani kwanza.
 
"AKIUMA UPANDE WA MIKATABA UNAONA LAHAA SANA,AKIUMA UPANDE WAKO NA MUNGU WAKO UNAONA HAFAI"
-Truth must told.
Upande wa mikataba tayari anao ushahidi wa kutosha, mfano ule mbovu wa bandari uliozitoa sadaka bandari zetu zote Tanganyika milele..

Lakini akiuma huo upande mwingine, ndio nimemtaka awe makini, asileweshwe na kelele za wafuasi wake wanaopenda kumsikia kila siku, wasiojali kama ana ushahidi wa kile asemacho au hana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom