Ushauri kwa huyu mwenzetu, muda wowote anaweza jiua

Yaaan kila siku hapa jf.. tunarudia yale yale... kuwa mchumba asomesh wi.
Ila kwa kuwa yamemkuta.. naomba kwa sasa atulie... aende kanisan akatubu amrudie muumba wake..
Ajitahid kuondoa mawazo ya huyo mwanamke kichwan kwake.. ndio ni ngumu lakin ajikaze. Ajenge maisha yake kwa sasa.
 
Habari za mchana wana jf

Tarehe 19/11/2016, siku ya Jumamosi kulikuwa na mahafali ya chuo kikuu flani (jina linahifadhiwa). Nilifanikiwa kufika chuoni hapo kusherehekea na mdogo wangu. Sherehe ilikuwa nzuri mpaka mwisho, muda wa sherehe ulipokwisha nilimuaga mdogo angu na kuanza kutoka getini.

Nilipofika getini nikakutana na kaka ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa mika 29 au 30 na sio mwanafunzi, huyu kaka alikuwa ameshika ua na anaonekana akiwa na msongo wa mawazo (stress). Kuna kijana mmoja akamuendea na kumuuliza juu ya hali yake, ghafla yule kaka akaanza kulia. Kundi la watu likazidi kuongezeka na kumsogelea na wakaanza kumuuliza yule kaka juu ya tatizo lake.

Kaka akaanza kueleza kwa masikitiko makubwa kwamba alikuwa na mpenzi wake ambaye amedumu nae tangu huyo dada akiwa kidato cha tano na sasa hivi ndio anahitimu chuo. Katika maisha yake amemsaidia sana huyo dada, alimpenda katika shida na raha akiamini kuwa ndie atakayemuoa, ilifikia kipindi jamaa alikuwa anatoa pesa ya matumizi kama mzazi wake, pia anadai kwamba bodi ya mkopo ilimpa mkopo kiasi kidogo sana kwahiyo huyo kaka alikuwa na wajibu kumlipia ada huyo mke mtarajiwa.

Siku moja kabla ya sherehe ya chuo kufika, yule dada alimchunia mpenzi wake bila sababu ya msingi na akafunga simu. Kaka akawa anapiga simu lakini haipatikani ndipo alipofunga safari ya kuja chuo kwa lengo la kumaliza mgogoro wao na kusherehekea pamoja. Kaka akajifungasha na zawadi za kutosha na kwenda chuo kwa huyo mpenzi wake. Alifika chuo na kumkuta binti akiwa amevaa joho akaenda mpaka sehemu aliyokaa na kumsalimu lakini binti akajibu akiwa amenuna.

Muda wa kutunukiwa ukafika na dada akatunukiwa degree yake. Kaka akaenda kumvisha taji na kumpa zawadi na hongera, ghafla akaona kuna jamaa akimkumbatia yule binti na kumkisi. Kaka akajipa moyo na kumuuliza yule binti kuhusu huyo kijana anayemkisi, binti akamjibu kwamba yule ni mume wake mtarajiwa, yeye hawezi kuolewa na kijana wa mtaani. Binti akachukua ua na kumpa huyo mpenzi wake wa mtaani na kumuambia hilo ua ndio faraja yake.

Haya maneno yalimgusa kila mmoja aliyekuwa akimsikiliza kijana anayesimulia huku akibubujikwa na machozi. Huyu kaka aliwaomba watu wamshauri juu ya hilo jambo lililomkuta. Nami nimeona sina budi kuliweka hili jambo hapa JF ili kama ni mpitaji mzuri wa hili jukwaa apate ushauri pia

Karibuni kwa michango yenu, nawasilisha.
Mkuu hii mahafali ilikuwa ya tumaini universty tatizo la kuchukua majukum ya wazaz/walez kwa mwenzetu ndio matokeo yake jaman humu wakuuu kila leo wana tahadharisha ni bora kubwia sumu kuliko kusomesha wat is so cslled mchumba
 
Pole yake,Mungu amtie nguvu hizi mambo hazinaga formula wala mjanga......wanaume mnaumia kwa kutumia /kuwekeza materials na wanawake wanaumiaga kwa kutumika utu wao inreturn mnawaacha kwa kashfa kubwa pia ni mambo ya kawaida ye sio wa kwanza wala wa mwisho,ila MUDA NI TIBA ,TUNAPOUMIA TUNAPONA KWA WAKATI HUO HUO
 
Hivi hapa duniani kati ya wanawake na wanaume wepi ni wengi? Nimewahi kusikia kwamba wanawake ni wengi zaidi. Sasa mimi sioni sababu ya huyo jamaa kutaka kujiua, yeye atafute tu mwanamke mwingine na asonge mbele na maisha yake. Kuna wanawake wengi sana tena wazuri wa maumbo na tabia wanaotafuta wanaume wa kuwaoa na hawajawapata bado.
Ukitaka kujua ukweli wa hili, huyo jamaa kama ni Mkristo azunguke kwenye "makanisa ya walokole" na atashuhudia mamia ya wasichana wanaokwenda kwa wachungaji ili waombewe wapate waume wa kuwaoa. Bahari imejaa samaki wengi sana, lakini inategemea ni wapi na ni wakati gani unatupa nyavu zako.
Namtakia kila la heri.
Hakika mkuu uko sawa, nakuunga mkono.
 
Pole yake,Mungu amtie nguvu hizi mambo hazinaga formula wala mjanga......wanaume mnaumia kwa kutumia /kuwekeza materials na wanawake wanaumiaga kwa kutumika utu wao inreturn mnawaacha kwa kashfa kubwa pia ni mambo ya kawaida ye sio wa kwanza wala wa mwisho,ila MUDA NI TIBA ,TUNAPOUMIA TUNAPONA KWA WAKATI HUO HUO
YES MDA NI TIBA
 
Habari za mchana wana jf

Tarehe 19/11/2016, siku ya Jumamosi kulikuwa na mahafali ya chuo kikuu flani (jina linahifadhiwa). Nilifanikiwa kufika chuoni hapo kusherehekea na mdogo wangu. Sherehe ilikuwa nzuri mpaka mwisho, muda wa sherehe ulipokwisha nilimuaga mdogo angu na kuanza kutoka getini.

Nilipofika getini nikakutana na kaka ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa mika 29 au 30 na sio mwanafunzi, huyu kaka alikuwa ameshika ua na anaonekana akiwa na msongo wa mawazo (stress). Kuna kijana mmoja akamuendea na kumuuliza juu ya hali yake, ghafla yule kaka akaanza kulia. Kundi la watu likazidi kuongezeka na kumsogelea na wakaanza kumuuliza yule kaka juu ya tatizo lake.

Kaka akaanza kueleza kwa masikitiko makubwa kwamba alikuwa na mpenzi wake ambaye amedumu nae tangu huyo dada akiwa kidato cha tano na sasa hivi ndio anahitimu chuo. Katika maisha yake amemsaidia sana huyo dada, alimpenda katika shida na raha akiamini kuwa ndie atakayemuoa, ilifikia kipindi jamaa alikuwa anatoa pesa ya matumizi kama mzazi wake, pia anadai kwamba bodi ya mkopo ilimpa mkopo kiasi kidogo sana kwahiyo huyo kaka alikuwa na wajibu kumlipia ada huyo mke mtarajiwa.

Siku moja kabla ya sherehe ya chuo kufika, yule dada alimchunia mpenzi wake bila sababu ya msingi na akafunga simu. Kaka akawa anapiga simu lakini haipatikani ndipo alipofunga safari ya kuja chuo kwa lengo la kumaliza mgogoro wao na kusherehekea pamoja. Kaka akajifungasha na zawadi za kutosha na kwenda chuo kwa huyo mpenzi wake. Alifika chuo na kumkuta binti akiwa amevaa joho akaenda mpaka sehemu aliyokaa na kumsalimu lakini binti akajibu akiwa amenuna.

Muda wa kutunukiwa ukafika na dada akatunukiwa degree yake. Kaka akaenda kumvisha taji na kumpa zawadi na hongera, ghafla akaona kuna jamaa akimkumbatia yule binti na kumkisi. Kaka akajipa moyo na kumuuliza yule binti kuhusu huyo kijana anayemkisi, binti akamjibu kwamba yule ni mume wake mtarajiwa, yeye hawezi kuolewa na kijana wa mtaani. Binti akachukua ua na kumpa huyo mpenzi wake wa mtaani na kumuambia hilo ua ndio faraja yake.

Haya maneno yalimgusa kila mmoja aliyekuwa akimsikiliza kijana anayesimulia huku akibubujikwa na machozi. Huyu kaka aliwaomba watu wamshauri juu ya hilo jambo lililomkuta. Nami nimeona sina budi kuliweka hili jambo hapa JF ili kama ni mpitaji mzuri wa hili jukwaa apate ushauri pia

Karibuni kwa michango yenu, nawasilisha.
Nikishasema kupenda kwa namna hii ni ujinga ukio piliza, binadamu mliyekutana wakubwa hauwezi mwamini kiasi hicho!!!!!
Na dunia hii watu innocent ndio wanao umia sana!!!
Pole sana kwake huyo jamaa, kapoteza pesa pamoja na mda so painful, lakini naweza kumwambia maisha bado yapo kuchwa sio mwisho wa dunia yeye sio wa kwanza kuachwa wala hatakuwa wa mwisho kuachwa
 
Hivi mbona tunapenda njia za mkato? Harama ya kusomesha mchumba hewa na harama ya mahari ipi kubwa??

Ndukiiiii
 
Watu wengine wanaroho ngumu sana!.
Mungu amtie moyo. Yeye ajiue wengine tunaendelea kula raha za dunia.
Yaani aache vyuku vyote hivi kwa ajili ya F*L* mmoja tu!
 
yaan toka secondary mpk chuo kikuuu!!! sasa si heri angejisomesha mwenyew...aisee kupitia hii akili za jamaa unaweza ukajua hata jamaa ni kada wa chama gan pia
Jamani!
Mapenzi nayo yana ukada?
 
Kha! hawakusikia mchumba hasomeshwi?

Yaani angeoa na mimba juu ndo angeendelea kumsomesha otherwise ni kutafuta maumivu tu
 
Ni kweli aisee!! Sijui kwanini tu watu huwa wanawachukulia wenzao for granted. Mtu anayejitolea kukufanyia jambo kubwa kiasi hicho ni wa kumpenda na kumheshimu sana.

Amuache aende tu, chozi lake Mungu atamlipia.

inaumiza sana, lakini sisi wanaume huwa hatukubali makosa yetu na kujirekebisha, unaweza kukuta huyu kila siku ana gubu kosa Dogo la mapenzi anasema unajua Mimi nakusomesha,sasa Dada kahitimu amechoka gubu,hii ni kote Iwe kwa gari,masomo,nyumba na nk,
 
Back
Top Bottom