Ushauri kwa huyu mwenzetu, muda wowote anaweza jiua

Mimi nina mshauri huyo kaka kwamba asikate tamaa, yeye ni mwanaume afanye mambo yake na amuombe mungu amsaidie,
Asiwaze sana kuhusu huyo binti hilo tukio liliomkuta,
Hizo ni moja kati ya changamoto za maisha & mapenzi kwa ujumla, aoneshe msimamo wake kama mwanaume ajikaze na kusonga mbele na safari.

Kumbuka kila mwana wa adamu aliyeumbwa kwa udongo na kuumwambwa na mwenyezi mungu, atapitia katika magumu na marahisi.

Na ikumbukwe kwamba jambo lolote utakalo mfanyia mwanadamu mwenzio basi ipo siku tu ni lazima na wewe utafanyiwa na inaweza ikawa ni zaidi.

Waswahili husema " malipo ni duniani "

Na wazungu husema " what's come around, gone around "
 
Kwanza nampongeza kwa uwezo wa kumsomesha mana elimu ni kitu cha msingi
Na pili asilieee akae atulie mana hivi vitu ni kawaida sana kutokea so usikate tamaaa
 
Kwani alijilazimisha amsomeshe ..alifanya hivo.kwa upendo tu kwa mwenzie na kaama uwezo alikua nao wa kufanya hivo ...ni dhambi ..
hawez kuchukia.wanawake wote sabaabu najua kuna ambao wapo hawana roho za kinyama na kishetani ambao wanaa ushirika na LUCIFER kama huyo dada.
Kabisa wengine tuna roho nzuri sana
 
Sasa analia nini mi ninavojua unapomfanyia mwanamke vitu kama ivo chukulia tu umempa kwa mapenzi sio unamsomesha demu alafu unataka umuoe izo fikra potofu we mpe kwa ajili ya mapenzi yenu ya muda huo ata mie nikimpata demu akawa ameshindwa kiasi flan cha ada nitampa kwa kuwa ni sehemu ya mapenzi yetu. Na sio kusema utamuoa izo fikra baadae zinawaumiza ila pole yake maana alichotegemea sicho kabisa
 
Mara nyingi wanaume bahili hawakutani na visa kama hivyo ila wahongaji kwao ni kawaida. Mwambie zinaa YATOSHA, aoe ili hiyo hamu ya kuhudumia amfanyie mkewe.
 
Habari za mchana wana jf

Tarehe 19/11/2016, siku ya Jumamosi kulikuwa na mahafali ya chuo kikuu flani (jina linahifadhiwa). Nilifanikiwa kufika chuoni hapo kusherehekea na mdogo wangu. Sherehe ilikuwa nzuri mpaka mwisho, muda wa sherehe ulipokwisha nilimuaga mdogo angu na kuanza kutoka getini.

Nilipofika getini nikakutana na kaka ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa mika 29 au 30 na sio mwanafunzi, huyu kaka alikuwa ameshika ua na anaonekana akiwa na msongo wa mawazo (stress). Kuna kijana mmoja akamuendea na kumuuliza juu ya hali yake, ghafla yule kaka akaanza kulia. Kundi la watu likazidi kuongezeka na kumsogelea na wakaanza kumuuliza yule kaka juu ya tatizo lake.

Kaka akaanza kueleza kwa masikitiko makubwa kwamba alikuwa na mpenzi wake ambaye amedumu nae tangu huyo dada akiwa kidato cha tano na sasa hivi ndio anahitimu chuo. Katika maisha yake amemsaidia sana huyo dada, alimpenda katika shida na raha akiamini kuwa ndie atakayemuoa, ilifikia kipindi jamaa alikuwa anatoa pesa ya matumizi kama mzazi wake, pia anadai kwamba bodi ya mkopo ilimpa mkopo kiasi kidogo sana kwahiyo huyo kaka alikuwa na wajibu kumlipia ada huyo mke mtarajiwa.

Siku moja kabla ya sherehe ya chuo kufika, yule dada alimchunia mpenzi wake bila sababu ya msingi na akafunga simu. Kaka akawa anapiga simu lakini haipatikani ndipo alipofunga safari ya kuja chuo kwa lengo la kumaliza mgogoro wao na kusherehekea pamoja. Kaka akajifungasha na zawadi za kutosha na kwenda chuo kwa huyo mpenzi wake. Alifika chuo na kumkuta binti akiwa amevaa joho akaenda mpaka sehemu aliyokaa na kumsalimu lakini binti akajibu akiwa amenuna.

Muda wa kutunukiwa ukafika na dada akatunukiwa degree yake. Kaka akaenda kumvisha taji na kumpa zawadi na hongera, ghafla akaona kuna jamaa akimkumbatia yule binti na kumkisi. Kaka akajipa moyo na kumuuliza yule binti kuhusu huyo kijana anayemkisi, binti akamjibu kwamba yule ni mume wake mtarajiwa, yeye hawezi kuolewa na kijana wa mtaani. Binti akachukua ua na kumpa huyo mpenzi wake wa mtaani na kumuambia hilo ua ndio faraja yake.

Haya maneno yalimgusa kila mmoja aliyekuwa akimsikiliza kijana anayesimulia huku akibubujikwa na machozi. Huyu kaka aliwaomba watu wamshauri juu ya hilo jambo lililomkuta. Nami nimeona sina budi kuliweka hili jambo hapa JF ili kama ni mpitaji mzuri wa hili jukwaa apate ushauri pia

Karibuni kwa michango yenu, nawasilisha.
Hivi wanawake wote hawa mitaani bado unawaza kufa kisa demu.!!!
Basi ushauri wangu ni huu:-
Kama utajiua basi R.I.P mpe hai Kanumba mwambie tangu aondoke Bongo movie imekufa!
Pia mwambie baba wa taifa huku hali ni mbaya na hatuna pa kukimbilia.!
 
Pole mkuu,ikiwa uligharamia kwa makubaliano ya uwepo wa mahusiano bas siku moja atakuona wew sio wa mtaani,ila kama hukuwahi kugusia ujumbe wa mahusiano basi unapaswa ujilaumu,,vip kwanza hata mzigo hujawahi kupewa????
 
Mwanamke hasomeshwiiiii ni kosa la jinai hilo xaxa avumilie yu...the world has a aay of repaying its debts to peoples
 
Back
Top Bottom