USHAURI:Kama namna naweza kuzuia na hali hii

Pole sana mkuu, wazazi wamekuzuia kisa DINI mmh hizi DINI hizi,

ushauri wangu ni mdogo tu wala sio mkubwa Ila naimani utakusaidia kwa hio usinipuuze

kwanza ikubari hali uliyonayo namaanisha kubari jinsi ulivyo huyo ni wewe huwezi kua mtu mwingine na yaliyotokea yameshatokea huwezi kuyafuta kwenye ukurasa wa maisha yako hizo page kwenye kitabu Cha maisha yako zipo tu na utazisoma na kuzisoma na kuzisoma kwa hio jikubari kwa hali uliyonayo na

pili jaribu kubadirisha mtazamo (hasi) ulionao kuhusu suala la ndoa (kuogopa ukipeleka mchumba basi watamkataa) kwa kubadirisha mazingira uliyopo yaan km upo Dar na hio situation ilikukumba Dar hama nenda kahamie sehemu ambayo roho na Nafsi yako vitakua na furaha na amani kumpata yule anaekufaa,

tatu maumivu wengi tumepitia Ila tumejifunza tumeumbiwa kusahau ingawa majeraha tunaishi nayo even though situation hazifanani, wewe ni wazazi wamemkataa mchumba mwingine mchumba kamgeuka kabla ya utambulisho anaoa mtu mwingine (usaliti) jeraha hili hakiponi kwa haraka ni kila siku zinazoenda kwa Mungu unaliangalia tu kovu lako
Naelewa nami nimekubali yameshapita sijataka kuwa na ukaribu nae sabbu ya sitaki kuharibu mahusiano yangu na yake sabbu nae bad hajaoa
Asante Kwa ushauri
 
Bora umenisaidia
Lakini unakwepa swali langu.

wewe Kuwa na maamuzi ya Akili usituchoshe kama unaona uislamu wako niwa maana sana komaa nao na tafuta wa dini yako kama unamashaka nao basi Njoo huku kwa Wakristo ule maisha mapya
 
Aaliyyah Sababu zipo kadhaa, kwanza unavuka mipaka fulani na automatically baraka ya kuiendea ndoa inaondoka, secondly inawezekana una dalili ya jini mahaba kuna faida anapata kwako so anakuvuruga ubaki single muda wote ili asikukose.

Ukiwa hujaelewa utaniPM nikiingia ntakupatia ushauri inshaallah.
 
Lakini unakwepa swali langu.

wewe Kuwa na maamuzi ya Akili usituchoshe kama unaona uislamu wako niwa maana sana komaa nao na tafuta wa dini yako kama unamashaka nao basi Njoo huku kwa Wakristo ule maisha mapya
Tusichoshane 😀sijaleta mada ya Imani usitoke nje ya mada
 
Kitu ambacho sitakuja kukisikiliza ni mswala ya IMANI ktk Ndoa. Bahati nzuri ni kwamba sina huo mpango wa kuoa ktk Maisha yangu. Otherwise nisingesikiliza lolote linalohusu Imani nikiwa nataka kufanya jambo linalohusu Maisha yangu.
 
Kitu ambacho sitakuja kukisikiliza ni mswala ya IMANI ktk Ndoa. Bahati nzuri ni kwamba sina huo mpango wa kuoa ktk Maisha yangu. Otherwise nisingesikiliza lolote linalohusu Imani nikiwa nataka kufanya jambo linalohusu Maisha yangu.
Sawa afande Rama tumekuelewa
 
Pole sana Aaliyyah

Kukataliwa kwa mara ya kwanza ndiyo chanzo cha haya yote. Na kukataliwa huko kuliambatana na jambo ambalo halikuwa na msingi wowote. Unaamini mlipaswa kuunganishwa na upendo baina yenu kuliko imani zenu. Kuachana kwenu kulichagizwa na mvutano wa nje, wala si maamuzi yenu binafsi.

Ukweli ni kuwa (hata kama utakataa hapa jukwaani), ulikuwa tayari kuufata upande wake ili kulinawirisha penzi lenu. Ukweli ni kuwa, hujapata mbadala wa kumpenda kama ambavyo ulimpenda mpenzi wako wa kwanza.

Hali hii inakuathiri na unapaswa kufanya yafuatayo;
1. Acha kufikiria kukataliwa kwa mchumba wako wa mara ya kwanza. Kubali kuwa, mmeachana na kamwe hamtokuwa pamoja.

2. Jiaminishe kuwa ndugu zako wana mapenzi mema zaidi kwako na wala hawakukataa kwa hila. Jikoleze kwa kufikiri kuwa familia inayojengwa kwa misingi ya imani mbili tofauti ina migogoro mingi. Aminisha nafsi yako kuwa imani yako ndiyo sahihi na nguzo katika ukuaji wa familia imara hapo mbeleni.

3. Usimlinganishe mpenzi wako wa sasa na aliyepita, vivyo hivyo kwa mapokeo ya nduguzo. Amini ya kuwa sasa huyu atapokelewa na hatua zaidi zitafuata.

4. Thubutu kumtambulisha mchumba wako wa sasa. Anza kwa rafiki zako kisha ndugu wa karibu kama kaka na dada. Sikilizia muitikio wao. Utakupa nguvu ya kumruhusu kwenda nyumbani. Zaidi, kubali wewe ukatambulishwe kwanza na hiyo itakupa msukumo wa wewe kumpeleka nyumbani.

5. Waza kuwa na familia. Jiaminishe ni wakati sahihi wa kuwa na mwenza na hata kupata watoto. Hii itakusukuma kuanza taratibu, kutambulisha ikitangulia.

6. Muombe Mungu kwa imani yako akupe wepesi na nguvu ya kuliendea jambo hili bila hofu yeyote.

7. Nikutakie kila la kheri na amini umeshafanikisha. Mungu akutangulie.
 
Back
Top Bottom