MUONGOZO: Mambo ya kuzingatia unaponunua gari lililotumika ndani ya Tanzania

safi sana mtoa maada kuhusu ununuzi wa magari. siku hz kuna magari ya kisasa mengi sana hadi yanatuchanganya. je ni gari gani dogo la kutembelea linaweza kutembea umbali mrefu bila kuleta tatizo. mfano kutoka dar kwenda songea na kurudi. asante
 
Uzi umetulia sana... Hasa kwenye point yako ya 6 nilikua sina ujuzi nayo Asante kwa kunielimisha..
 
Pale kidogo chekundu nliletewa Gari mpk nkachanganykiwa maana kla dakika napgiwa sim nkaone duuh balaa nkaamua niagze tu
 
kwa ushauri wangu kama mtu anapesa ya kutosha ni kwenda tu show room na kuchagua kitu roho inapenda , lakini kama ni pesa zetu za kudunduliza basi lazima mtu ununue used kutoka kwa rafiki au jamaa so hayo mengine ni maerekebisho ya kawaida kutegemeana na hali ya gari husika.
 
Lazima nirudi,uzi mzuri Ila mimi sijui kwa nini mara nyingi watu wengi huwa wanaharaka.
Mtu hela yake unamwambia tulia twende taratibu utakuja kumuona na kigari chake huyooooo kesha nunua..
Baaada ya muda anakuulizia wapi kuna mafundi wazuri hahahahahaa.
Kaaaazi kweli
 
Usiogope Mwanangu mm nilipofikia Hatua ya kununua gari nilitulia sana kwanza kablayakununua mwaka 1 nilifanya window shopping karibuu
*3 then ilipofka nilikwenda Ma fund Dereva kutoka mkoani kwangu. Nikaanza mwenyewe window shopping kutoka manyanya yard hadi AAR hosp had US Embassy pale, Nikachua muda Wa sku zngne 3 Na mke wangu tukifunga nakumuomba Bwana atupe gari bora. Wapambe ni Wengi had ktk family take care. Baada ya maombi nikaenda yard pale AAR+ nikapata ki Carina changu bomba kiulaiiinii namwita fund kakikubali. Nikaacha ktambulisho changu cha kaz Kama dhamana nikaenda kulipia huku nyuma kuna mchaga m1 kakipenda. Maana ilikuea December 2015 lkn huku nyuma ktambulisho cha usalama kikawaogopesha wahindi wale hawakumpa mchaga. Hadi Leo kla anayekiona anaksifia Carina yang mpaka basi. Muombe mungu naye hatakutupaa. Carina hii ni roho ya paka namshukuru mungu. USIOGOPE
ilkuwa DEC 2015.....
 
Uzi mtamu huu na nimeukuta katika kipindi muafaka
Wadau nahitaji used spacio new model au altrnative ya toyota gx110 kwa mwenye msaada hapo.
 
Lazima nirudi,uzi mzuri Ila mimi sijui kwa nini mara nyingi watu wengi huwa wanaharaka.
Mtu hela yake unamwambia tulia twende taratibu utakuja kumuona na kigari chake huyooooo kesha nunua..
Baaada ya muda anakuulizia wapi kuna mafundi wazuri hahahahahaa.
Kaaaazi kweli

Mtu wa hivyo ni kuachana naye,
 
Baada ya kusikia watu wengi 'wakiumizwa' na 'kupigwa' wakiwa kwenye harakati za kutafuta usafiri uliotumika nchini, nimeona sio mbaya nikitoa ushauri ni jinsi gani unaweza kuepuka majanga kwenye zoezi hilo.

Naandika kama mnunuzi au muuzaji wa aina hio ya magari, kwahio siegemei upande wowote na ninachokiandika hapa sio sheria naweza kuwa sahihi au nisiwe sahihi ila ni imani yangu lipo litakalosaidia baadhi ya watu.

Njia muhimu za kufuata ili kupata gari unalotaka ni kama ifuatavyo:

1.Fanya utafiti mdogo juu ya gari unayoitaka: Uliza ujue gari unayoitaka inauzwa kiasi gani[makadirio]. Ukiweza kujua bei ya showroom au ukiagiza mwenyewe Japan halafu linganisha na bei utakayopewa hapa. Hili ni muhimu kwa sababu nimeshuhudia watu wananunua magari yaliyotumika Tanzania kwa bei ambayo ukiagiza mwenyewe unalipata kutoka japan au ukiongeza kidogo tu unapata la showroom.

2.Usiwe na haraka: Usiwe na haraka kabisa kwenye kutafuta gari. Utaletewa kila aina ya gari na usipokuwa makini utanunua gari bovu. Angalia taratibu angalau magari matano tofauti kwenye chaguo lako ndipo uamue, madalali watakusumbua ili mradi tu wapate cha juu.

3.Epuka madalali: Kama unaweza epuka madalali. Tafuta gari kwa kuuliza watu ulio karibu nao, ndugu jamaa na marafiki au unaofanya nao kazi au biashara. Hii ni nzuri chochote kikitokea una pa kuanzia. Madalali wengi hawajali maslahi yako wala ya muuzaji cha muhimu kwao ni cha juu tu. Gari ya 4m dalali atakuuzia 5-6m.

4.Tafuta Fundi: Ukilipenda gari lolote tafuta fundi akusaidie kulikagua,hata kama una idea na magari kuna vitu hutaviona ila fundi atakusaidia. Kuwa makini kuna mafundi huwa wanabonyezwa wakufiche hitilafu halafu baadae wanarudi kupewa chao ukishauziwa kanyaboya.

5.Epuka gari iliopigwa rangi: Epuka gari iliopigwa rangi siku chache kabla ya kuwekwa sokoni, wazoefu wanajua gari za aina hio ndio umuhimu wa fundi unapokuja. Gari inaweza kuwa imegongwa hivyo imenyooshwa na wanakuzuga kwa rangi inayong'aa. Siku hizi rangi hata 200,000 unapiga gari nzima ila ukinunua hilo baada ya mwezi rangi inababuka yote.

6.Epuka gari iliooshwa engine:Ukikagua gari ukiona imeoshwa engine ogopa sana. Mara nyingi gari zinaoshwa engine kuficha 'leakage',yaani oil na vitu vingine vinavyovuja kutoka sehemu mbalimbali za engine.

7.Jaribu gari wewe mwenyewe: Ni muhimu kuendesha na kuijaribu gari wewe mwenyewe hata ukienda na fundi. Ipitishe njia mbovu usikie jinsi ilivyo chini,chochote kinachogonga kuwa makini,usisikilize ukiambiwa ni tatizo dogo, kwanini hakurekebisha. Ingawa yapo matatizo madogomadogo ila kuwa makini.

8.Usiangalie Namba: Usibabaishwe na namba, eti hii C,D etc. Kuna gari namba A ziko vizuri kuliko namba C. Muhimu ni hali ya gari husika kwa muda huo.

9.Nenda TRA kujiridhisha: Ni muhimu kujua ukweli na status ya gari na mwenye gari. Jiridhishe anaekuuzia ndio mwenye gari. Akuonyeshe nyaraka zote halisi hata za kodi aliolipia.

10.Mwisho kabisa ukilipenda gari fanyeni makabidhiano kwa kuandikishana kwa mwanasheria. Ukiweza lipia benki na ubaki na risiti kama ushahidi wa malipo kupitia akaunti yake. Epuka kubeba cash kumpelekea muuzaji mahali alipo.

Haya machache naamini yanaweza kuwa msaada kwa watu wanaonunua magari yaliyotumika nchini,wengine mnaweza kuongezea mawili matatu na kurekebisha nilipokosea.



Umetoa Elimu nzuri saaaaana. Mwenye macho na some na kuelewa.
 
Back
Top Bottom