Ushangiliaji wa mashabiki wa Wydad Casablanca, unatosha kabisa kuharibu saikoljia ya wachezaji wa timu pinzani

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,076
144,511
Hakika huu ndio ukweli na hii ni baada ya kuona clip mmoja mtandaoni. Mashabiki wa hii timu wana spirit ya ajabu katika kushangilia na kuna wahamasishaji kabisa wako kwa ajili hiyo.

Wingi wa mashabiki pamoja na spirit kubwa ya ushangiliaji, ni wazi hii ndio sababu tosha timu nyingi kula kichapo hawa jamaa wanapocheza katika ardhi ya nyumbani kwao kwani style yao ya ushangiliaji inatosha kabisa ku-demorolize timu pinzani na kuwaathiri kabisa kisaikolijia.

Uzoefu wa wachezaji unaweza tu kupunguza idadi ya magoli lakini sio kushinda. Huku ndio kucheza na kutafuta ushindi nje ya uwanja ambapo sisi kwetu ni kuloga badala ya mbinu kama hizi.

Hata hivyo, ukibahatika kuwafunga hawa jamaa kwao, basi utajijengea heshima kubwa sana katika Soka la Afrika.

Je, Simba wataweza kuandika hiyo historia na kujijengea hiyo heshima?

Binafsi naona ni vigumu sana ila lololote pia linawezekana.

Kazi kwenu Makolo.
 
Back
Top Bottom