Usaliti wa Dkt. Slaa ni upi?

Kumbuka tu 2010 Chadema ilisimama peke yake, halafu 2015 viliungana vyama vingapi.?

Ukitaka kujua mchango wa Dr Slaa Nenda kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa 2014......hapo ndio utajua hata kura na mafanikio ya 2015 mizizi ni 2014.

Huyo Lowasa amekuja kwenye shamba ambalo tayari limeshalimwa.
kwa nini unadhani shamba alililima slaa peke yake na sio na mbowe,zitto,mnyika,mdee,lissu?
 
Mbowe na Lowassa Nani msaliti?

Mbowe kawasaliti watanzania wapinzani waliokuwa wameujenga upinzani Kwa Hali na mali,

CCM mafail yote ya Lowassa wanayo na Lowassa ni mnyonge, kuna mengi hayasemi kuwahadaa watu,

Ila mbowe msaliti
I truly remember those days walahi!
Sisemi uwongo, walikuwa wamejipanga vizuri!
 
Nimekuwa nikisoma soma humu tokea 2015 kutoka kwa baadhi ya watu kuwa eti aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA na mgombea urais wa chama hicho mwaka 2010, Dkt. Wilbroad Slaa ni msaliti.

Eti ni msaliti kwa sababu aliamua kuachana na siasa baada ya CHADEMA kuamua kubadili gia angani. Pia, baada ya kuachana na siasa akakataa pia kumuunga mkono mgombea wa UKAWA, Edward Lowassa.

Sioni kabisa usaliti wa Dkt. Slaa hapo. Ninachokiona ni mtu mwenye msimamo na uadilifu na anayeongozwa na kanuni.

Hivi kweli kabisa mtu na akili yako timamu, kati ya Slaa na CHADEMA, unaweza kumwona Slaa ndiye msaliti?

Kama kuna msaliti basi msaliti huyo ni CHADEMA na si Dkt. Slaa.

CHADEMA walisaliti karibu kila kitu walichokipigania wakiongozwa na Dkt. Slaa. Ni CHADEMA ndiyo waliobadilika. CHADEMA ndiyo wasaliti.

Nyie wote mnaodiriki kumuita Dkt. Slaa kuwa ni msaliti ni vifuu tundu msiojielewa kabisa.
Yaani wewe Nyani mtu akishakuwa upande wa huyo ngosha mwenzako unamtetea tu. "I wish I kudu be IGP"!
 
Mimi kwangu nina mitazamo tofauti ni wengine kuhusu Dr. Slaa. Usipokuwa makini unaweza kumchukulia Slaa kama msaliti. Sikufurahishwa na Slaa alipoondoka cdm, tena kuondoka kwake akakutumia kama sehemu ya kuiumuza cdm kwa faida ya ccm. Ila hata ningekuwa mimi ningechukua maamuzi ambayo yangewashangaza wengi. Slaa alijiandaa kugombea urais cdm, na kweli alistahili hata kama asingeshinda lakini cdm ingebaki na msimamo wake. Lakini ninachomlaumu Slaa mpaka leo, hivi akija mtu kwenye chama chako kwakuwa humpendi ndio unaondoka. Kwangu naamini Slaa aliondoka cdm kwa kuzira baada ya kukosa nafasi aliyokuwa ameshajiandaa kuitumikia, ila kwakuwa cdm nao walifanya kosa kumpokea Lowassa ambaye alikuwa na kashfa, hapo ikawa rahisi Slaa kuhalalisha huko kuzira kwake. Hivyo mpaka sasa kwangu imebaki 50/50 kwamba Slaa aliondoka kwa kukosa nafasi ya kugombea urais, ama aliondoka kwa kutokutaka kubaki kwenye chama ambacho kimempa Lowassa nafasi adhimu ya kugombea urais wakati walimtuhumu kwamba ni fisadi. Yote mawali kwangu inaweza kuwa ni sababu ya Slaa kuondoka cdm.

Kama Slaa ni msaliti ama la, hilo linategemea na utashi wa kila mtu kulingana na uelewa wake na sababu nyingine mbalimbali. Kilichonifanya nianze kumuona Slaa hana maana ni ile sentesi yake ya jana kuhusu Lissu. Kwa kweli Lissu hakumfanyia Slaa sawa wakati kajitoa cdm kwa zile lugha alizokuwa anamtolea, lakini Slaa kama padre mstaafau alipaswa kusahau baadhi ya mambo na kuacha kutoa lugha zitakazoonyesha kwamba yaliyomkuta Lissu ni mambo ya kawaida. Ukiachia mapungufu hayo niliyoyaona kwa Slaa sioni kama ni adui sana wa cdm kulinganisha na mambo mengine yanayoendelea ndani ya cdm kwa sasa.
 
Slaa hajabadilika.

Alimkataa Lowassa wakati Lowassa yupo CCM na akamkataa alipoenda CHADEMA.

Huyo ni mtu mwenye msimamo. Mtu mwenye kanuni.

Sioni kabisa usaliti wake.
ahaa wapi! influenced by mama mushumbu, baada ya kulazwa nje
 
Hahaha Dr.Slaa kama Dr.Shika tu kwa sasa, apewe airtime aka promote tatu mzuka wamuandalie ule USIKU WA DR.SLAA pale Dar live mbagala, akimaliza tumsahau.
 
Kumbuka tu 2010 Chadema ilisimama peke yake, halafu 2015 viliungana vyama vingapi.?

Ukitaka kujua mchango wa Dr Slaa Nenda kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa 2014......hapo ndio utajua hata kura na mafanikio ya 2015 mizizi ni 2014.

Huyo Lowasa amekuja kwenye shamba ambalo tayari limeshalimwa.
Waulize kwanini EL hakwenda ACT au NCCR? Sijui tumerogwa? Alafu wanavyokomaa sasa! Dr Slaa msaliti! Wametusaliti alafu wanapiga propaganda! Hata "kiongozi" wao Mange anajua vizuri huu usanii ila anawamezea tu ....ipo siku watajua uzuri sumu haijaribiwi kwa ulimi!
 
Usaliti wa Dr slaa umegawanyika katika makundi makuu matatu
1. Kukataa kubadili gia angani
2. Kukataa kumpokea lowasa
3. Kusimamia kile anacho kiamini.
Kabisa ....walichomfanyia yule mzee hadi akakimbia nchi baada ya kuanza kutegemea Policcm kumlinda ambao kwa wakati ule kujihakikishia ulinzi huo ilikuwa ngumu! Vijana aliowalea mwenyewe wanamgeuka na kumuita msaliti kisa kumpokea EL! Hii dhambi lazima iwatafune CDM hadi watubu hadharani! Karma ni hapa hapa ingawa si kitu kizuri ...
 
Hizi ndizo hoja mlizobakiwa nazo!

Kufirisika kihoja ni kubaya sana!

Umejuaje kama anatoa povu lakini pia hata kama anatoa povu, umejuaje anatoa povu kwa ajiri ya kupata uteuzi?

Ina maana wewe hutoa povu kabla hawajafanya uteuzi?

Baadhi ya watu wakisema ninyi ni makarai mnaanza kupiga kelele?
Ungekuwa na hoja ungeishasikilizwa. Bidii hiyo kaitumie kwenu kujenga chama chenu ili muachane na kuhangaika na kununua watu.
 
wakina mbowe wanafikiri kila mtanzania ni zuzu wakati wa Dr. Slaa kila mtu aliiamini chadema lakini leo Chadema hawaaminiki kutokana na kutokuwa na msimamo inaonekana nia yao si kuwakomboa watanzania bali ni kuingia ikulu na kuendelea kula bata ni heri tuwaweke kando hadi tutakapopata upinzani wa kweli
 

Attachments

  • upload_2018-2-8_1-41-6.jpeg
    upload_2018-2-8_1-41-6.jpeg
    56.4 KB · Views: 25
Back
Top Bottom