Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

Status
Not open for further replies.
Mkuu ni mke wa kamishina Chagonja anafanya kazi pale NBC, UDSM Branch, ni mpepe sana huyu mama,
muongeaji kupitiliza na anapenda kutishia sana.

Kuna siku tulikwanguana nae na kigari chake alitoa maneno mpaka nikamfahamu, anyway nilimlipa kishkaji baadae ikawa issue mpaka nikabadili namba ya simu. Bora kaumbuka ilikuwa kila siku kuomba pesa, malipo ni hapa hapa dunian.
 
Kigogo,mke wa kigogo,mtoto wa kigogo ndio nini.?? Ina maana hata mahakamani watapelekwa kwa majina hayohayo.!!

Ukigogo siku hizi ni sifa ya juu kabisa ya kufanya mambo yasiofaa kujipatia hela na madaraka.Kama huwezi kusafirisha twiga mzimaa kwa ndege utakuwaje kigogo?
 
Hili ni tone tu ktk muktadha mzima wa uozo wa utawala usio wa sheria.

Au wanataka Kamanda Lissu atengeneze dossier kama ile ya majaji? Maana pamoja na uzito wake hatuoni mpaka leo sio Rais wala Werema au hata Pinda waliosema wala kufanya lolote kushughulikia aibu ile.

Huu mzigo wa CCM na serikali (pamoja na Taasisi zote TISS, Polisi na Mahakama) umekua mzito sana na lazima tuutue.

Aibu tupu kila kona kila siku. ENOUGH!
 
Kigogo,mke wa kigogo,mtoto wa kigogo ndio nini.?? Ina maana hata mahakamani watapelekwa kwa majina hayohayo.!!
Mku haya ndio magazeti yetu, na Zitton anasema eti hili ndio gazeti bora kuliko yote bongo, that way nalimiss sana MwanaHalisi lilikuwa linaweka mambo wazi, mpaka ZZK alilichukia.
 
Mkuu ni mke wa kamishina Chagonja anafanya kazi pale NBC UDSM Branch, ni mpepe sana huyu mama,
muongeaji kupitiliza na anapenda kutishia sana , kuna siku tulikwanguana nae na kigari chake alitoa maneno mpaka nikamfahamu... anyway nilimlipa kishkaji badae ikawa issue mpaka nikabadili namba ya simu. bora kaumbuka ilikuwa kila siku kuomba pesa... malipo ni hapa hapa dunian?

Mkuu ni yule Manager Jane? Kama ni yeye mbona namuona kama mpole hivi?
 
Lazima kijana mmoja au wawili waloibiwa wa brauzi hapa watufungukie.
 
Alisema mkewe alitoa fedha taslimu zisizopungua Sh1.5 milioni, mbali na gharama za kununua bidhaa na vifaa mbalimbali ambavyo wanafamilia hao wangetakiwa kwenda navyo mafunzoni.

Kwahiyo huyu anachotaka kutuambia ni kwamba alimruhusu mkewe akatoe rushwa ili wanafamilia wake wapate kazi?


 
Mh! Japo TAKUKURU imeonyesha udhaifu katika kutokomeza rushwa, sitaki kuamini kuwa imefikia hatua ya kuajiri watoa rushwa ili wakapambane na rushwa.

Iwe ni utapeli au la, vijana waliotoa rushwa wanatakiwa kukamatwa na kushtakiwa kwani kutoa rushwa ni kosa la rushwa
.
 
Mimi ninajua gazeti ni MwanaHalisi tu na ndiyo gazeti nililokuwa nanunua. Haya mengine ni kama vipepurushi vya kampeni tu.
 
Kwani ajira za usalama wa taifa toka mwaka 1999 alipokufa nyerere si zinatolewa kwa rushwa na upendeleo???au macho yangu yana makengeza??

Kwani ajira ya usalama wa Taifa siku hizi inaanzia Jeshi la Polisi????....... makubwa na madogo afadhali.
 
Mimi sijaelewa bado hapa mnachoshangaa ni kitu gani!? Duniani watu wanaishi kwa kutumia maarifa na siyo Juhudi, au mmesahau kamanda wa Polisi alivyotapeliwa Mamilioni kwa ahadi kwamba yule tapeli ana uwezo wa kumshawishi JK amteuwe kuwa IGP?

Kama utapeli unaanzia kwa kuihusisha Ikulu hapo unategemea nini? Pili Mzee Mwanakijiji nadhani hauna taarifa sahihi za namna ya ajira za Usalama wa Taifa zinavyopatika kwa sasa, ni kwamba hazitangazwi lakini watu ndani ya Idara ndio wanakuwa na hizo taarifa na mwenye ushawishi ndio mwenye uwezo wa kuingiza vijana wengi zaidi, hiyo ndio sifa kuu hakuna kigezo kingine chochote.

Nina watu wangu wa karibu wapo kwenye hiyo Idara ya Usalama wa Taifa ukiangalia IQ zao utabaki unasikitika kwamba hawakuwa na sifa hata za kuwa mgambo, hilo ndilo tatizo kuu la nchi yetu, watawala wameacha hata Idara muhimu zishikwe na wahuni, kwakweli inasikitisha sana mtu wa level ya Usalama wa Taifa mpaka leo hana know how ya kutumia computer achilia mbali Internet.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo huyo mheshimiwa sana Kamanda wa Polisi alijua mchezo mzima wa hao kina Baraka,ikiwamo kuomba rushwa wafanikishe vijana kuajiriwa,lakini bado alitoa ruhusa kwa mkewe kuendelea na huo mpango?

Kama ni hivyo basi nchi hii itazinduliwa na kiama! Kamanda wa Polisi anashiriki kutoa rushwa,Kamanda wa Polisi haamini katika haki bali pesa mbele,Kamanda wa Polisi hajiongezi na kutaka kufatilia kwa nini ajira kwa pesa,kamanda wa Polisi anakaa kimya ili watu wake wafaidike, kamanda wa Polisi.

ki ukweli Tanzania hakuna polisi, ni genge la wahalifu!!!
 
IGP anapata kigugumizi kutoa maamuzi ama kumuokoa chagonja, mke wake na mtoto wake kwa utapeli au kuokoa Idara ya Uslama wa Taifa. Chagonja ndiye anafuata kwa madaraka baada ya IGP ndani ya jeshi la polisi.

Ili kuisafisha Idara ya Usalama wa Taifa na kauli iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Idara hiyo, IGP anapaswa kuchukua hatua.
 
Mwizi anaitwa kigogo..... mkuu hii nchi yetu ya ajabu sana.!
 
Kama chagonja hayuko kwenye mpango wa kuidhalilisha Idara ya Usalama ya Taifa kwa nini amesita kuchukua hatua kwa anaodai wamemtapeli mke wake? Polisi mwenye cheo kikubwa kama chake badala ya kuchukua hatua analalamika kwa lipi? Mbaya zaidi anawataja kwa majina waliohusika kujifanya Maafisa Idara ya Usalama wa Taifa wenye fursa ya kutoa ajira.
 

Miaka iliyopita USALAMA wa TAIFA ndio waliokuwa WANAKUFUATA na Kukueleza kuwa WAMEKUANGALIA MWENENDO WAKO KWA MUDA MREFU

Unafaa kufanya KAZI USALAMA WA TAIFA; Walikuwa hawaajiri kama MAKAMPUNI MENGINE; Leo hii pamekuwa OFISI ZA AJIRA ? NDIO Maana hao

Waliompiga ULIMBOKA waliacha a lot of criminal items... NAONA WALISOMBWA na kumwagwa USALAMA wa TAIFA...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom