Usafi wa vyoo taasisi za umma Dar

Michewen

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
24,564
32,207
Kiukweli Watanzania kwa ujumla suala la choo ni kitu cha mwisho kabisa katika UJENZI, hata USAFI, hapa naorodhesha taasisi 6 za umma zenye angalau vyoo bora & safi katika jiji la Dar es Salaam.

1. Hospitali MWANANYAMALA
2. Hospitali AMANA
3. RITA Makao Makuu
4. IMMIGRATION HQ Kurasini
5. MACHINGA COMPLEX
6. Uwanja wa Ndege -JNIA
 
Vyoo vya feri (kivukoni) navyo ni vichafu sana halafu viko finyu sana, marumaru zimebadilika rangi zimekuwa nyeusi. Ukiingia vyoo mbalimbali vya kulipia Dar hautakuta mabomba yanayotoa maji. Maji umewekewa kwenye ndoo, kuna uhakika gani na usalama wa hayo maji?

Hebu tutoke nje ya Dar vilevile. Serikali ilipiga marufuku wasafiri wa mabasi kuchimba dawa porini na ikajenga vyoo baadhi ya maeneo hususan palipo na mizani, vyoo hivyo ni vichafu sana.

Nakumbuka safari moja nikielekea Mbeya tulifika sehemu, kabla ya Kitonga, kuna choo cha serikali, abiria ilibidi kweda nyuma ya choo (porini) maana choo hakifai.
 
suala la usafi wa vyoo ni kwa watanzania wote, hasa vyuo vikuu nakumbuka pale UDSM Hall 7 watu walikuwa wanajisaidia chooni kwa kusimama juu ya sinki huku ametandika gazeti MZALENDO ama DAILY NEWS (Ukubwa wake unatosha kupokea kinye.si hata kiwe kingi vipi.
 
suala la usafi wa vyoo ni kwa watanzania wote, hasa vyuo vikuu nakumbuka pale UDSM Hall 7 watu walikuwa wanajisaidia chooni kwa kusimama juu ya sinki huku ametandika gazeti MZALENDO ama DAILY NEWS (Ukubwa wake unatosha kupokea kinye.si hata kiwe kingi vipi.

Kwanini wanatandika gazeti?
 
Wanatandika gazeti ili nnya iliyopo hapo kwenye sink isiwarukie maana wengi hawa-flash
 
hapo UDSM ni shida population ya zaidi ya "Wasomi" 20,000 lakini pa kujisitisri ni AIBU kubwa.
 
Wanatandika gazeti ili nnya iliyopo hapo kwenye sink isiwarukie maana wengi hawa-flash

Labda hawaflashi sababu hakuna maji. Au makusudi?
Hebu nikupe mfano; ikiwa unasafiri Dar - Moshi, kuna hoteli pale Kati ya Korogwe na Mombo ipo upande wa kulia. Mabasi yana mwaga abiria kwa wingi sana pale kujisaidia lakini hukuti choo kichafu.

Vyoo vyake ni visafi sana hakuna hata harufu. Nadhani ni kwa sababu maji yanakuwepo wakati wote. Maji ya bomba ni muhimu sana vyooni hasa vyoo vya watu wengi.
 
ni kweli huenda suala la maji ndo tatizo lakini hushangai katika taasisi hizo hizo VX/ Nissan Patrol za maboss zipo order 24/7. Je kipi cha umuhimu maji ama Shangingi la Mheshimiwa a.k.a Boss. Inashindikana nini kuchimba kisima ama kuleta maji kwa lori?
 
Vyoo vya feri (kivukoni) navyo ni vichafu sana halafu viko finyu sana, marumaru zimebadilika rangi zimekuwa nyeusi. Ukiingia vyoo mbalimbali vya kulipia Dar hautakuta mabomba yanayotoa maji. Maji umewekewa kwenye ndoo, kuna uhakika gani na usalama wa hayo maji?

Hebu tutoke nje ya Dar vilevile. Serikali ilipiga marufuku wasafiri wa mabasi kuchimba dawa porini na ikajenga vyoo baadhi ya maeneo hususan palipo na mizani, vyoo hivyo ni vichafu sana. Nakumbuka safari moja nikielekea Mbeya tulifika sehemu, kabla ya Kitonga, kuna choo cha serikali, abiria ilibidi kweda nyuma ya choo (porini) maana choo hakifai.
Idea za magu hizi zinavoanza vizuri na kufa ghafla.
 
Hebu geukieni vyoo tulivyo acha majumbani kwetu, na hasa kule kijijini tulikotoka. Wengi tumekua tukiona choo ni kama shimo la taka ambalo kwa kawaida halihitaji usafi.

Wengi humu tunatoka maeneo ambayo nyumba hazina vyoo. Mtu toka mdogo anajisaidia ziwani, ni wazi hata weza kutumia ipasavyo vyoo vya kisasa. Watu wamezoea kujisaidia vichakani toka wadogo...balaa. idadi ya kaya zenye vyoo bora africa sehemu nyingi ni chini ya 50%.

Pamoja na kutofanyiwa usafi, vyoo vya umma vina athiriwa sana na aina ya watumiaji. Katika hili wazungu walituacha nyuma kilometa nyingi sana.

Turudini vijijini tukajenge vyoo bora kwa wazazi wetu na shule zetu ili kizazi kijacho kijifunze kuthamini utunzaji wa vinyesi.
 
vyoo vingi vya umma ni JANGA la kitaifa
cc. Wakuu wa Taasisi & Kaya.
 
hivi hatuwezi kukamatia fursa hii, tukaanzisha vyoo vya kuhamishika/mobile toilets tunaweka sehemu za mikusanyiko kama stendi, hospitali, kwenye foleni n.k
 
Back
Top Bottom