Usafi wa Mwanamke

Ikunda

JF-Expert Member
Jul 12, 2010
718
151
Hii ni kitu ya kucopy na kupaste, japokuwa hapa sio topic mpya ila ningependa kushare, tukumbushane tena, nanyi nyote

Habari zenu kina dada, mama na wadogo zetu.

Tungependa ku-share nanyi kuhusiana na jambo moja. Tafadhali tumia hii
kama changamoto kutaka kutafuta habari zaidi, kama sio kwaajili ya
kuhakiki tuliyoandika humu basi pia kwaajili ya kupata habari zaidi,
uelewe zaidi ili uweze kufanya maamuzi mazuri na sahihi kwa afya yako.

Sisi ni kina dada wasomi tu, unaweza hata kutuita "when I was". Basi
si unafikiri you know what you know and what you know is what it is!!
Mmh! Tuvunje ukimya, tuliongelee hili na tuelimike.

Mmoja wetu hizi habari alikua nazo lakini haikuwahi kumclick kwamba
wenzake labda hawana au hawana habari kamili au wana habari potofu.
Ongea na watu kadhaa ikaonekana kuna misinformation ya hali ya juu
kuhusiana na swala zima la....Kwa Bibi

Mtuwie radhi kwani tunaelewa kwamba kuna makabila ambayo huwafundisha
mabinti zao tangu wakingali wadogo juu ya hili. Na japokuwa kulikua
bado kuna asilimia kubwa ya wasichana ambao hawakuyajua haya na labda
hata wasingeyawaza, sasa hivi kumetokea mfumuko wa kitu kinaitwa kibao
kata!!! Funda nikufunde!! Hata kitchen party nazo. Huko ndugu zetu
ndio tunatumia kama jukwaa la kuelezana na kudanganyana hukusu...

Usafi wa uke!...wa ndani

Imani au uelewa uliokuwepo:
•Uke ni sehemu chafu chafu chafu sana tena yenye wadudu wa kutosha
yenye kunahitaji kusafishwa kila siku
•Uke unahitaji kusafishwa kwa hali ya juu zaidi mara baada ya siku za
hedhi au tendo la ngono
•Uke wapaswa kuwa mkavu wakati wote ute unakuwepo ukeni ni uchafu
usiopaswa kuwa pale
•Uke haupaswi kuwa na harufu hata kidogo. Harufu ni ishara ya uchafu au ugonjwa!

Kinachofanyika kutokana na imani hii ni kwamba uke husafishwa kila
siku nje na ndani. Hasa ndani kwa kutumia vidole na:
•Maji ya kawaida, labda vuguvugu
•Maji ya iliki
•Maji ya mchele
•Asali
•Rose water
•Vidonge vya kufyonza uchafu
•Maji yenye dettol
•Maji ya vinegar...

Ukweli ni kwamba:
•Uke ni mfumo unaojisafisha wenyewe kwa ndani na ni sehemu moja ya
mwili wako ambayo ni safi kuliko maelezo, safi kuliko midomo yetu.
Habari ndio hiyo.
•Mfumo huu husafisha damu ya hedhi na shahawa wenyewe, hauhijaji
msaada wa aina yeyote
•Uke wenye afya una bacteria, lactobacilli, ambao ni kawaida kuwepo
humo. Hawa hupambana na vijidudu visivyopaswa kuwepo huko kulinda uke
na mfumo wa uzazi kwa ujumla.
•Uke wenye afya sio mkavu, muda wote una ute usiokua na rangi (kama
maji), mwepesi na unaonata. Uzito, wingi na mnato wa ute huu hutegemea
na mabadiliko ya mwili wa mwanamke. (Jifunze tofauti ili ujue muda
inapaswa kumuona daktari)
•Uke wenye afya una harufu, ambayo ni nzuri, murua na isiyokera J.
Kama harufu itakua kali na inayokera (kama yai bovu) basi uke wako
hauko katika afya njema na unahitaji kumuona daktari.

Madhara ya kusafisha uke kama ilivyoainishwa hapo juu:

Ni kitu kimoja tu kinachopaswa kuingia kwa kibibi……ambacho ni babu
toshaaaaaaaa, vidole na vingine vyote vilivyoinishwa hapo juu it's a
no no situation na….

Unaporuhusu kitu chochote kisichotakiwa kuingia ndani ya uke wako,
unatoa nafasi ya kuharibu mfumo wake wa asili, na unajua ukishadisturb
mfumo wowote, athari zake ni chain reaction.
•Vidole vyako vinaweza kuwa na vijidudu (kumbuka uke ni msafi kuliko
vidole vyako) vijidudu hivyo vikashamiri na kuwashinda nguvu
Lactobacilli. Ukapata vaginal infections za kila namna.
•Kitendo hiki chaweza kupeleka vijidudu kwenye njia ya mkojo
ukasababisha UTI – Urinary Tract Infection
•Unawaua/kuwaondoa Lactobacilli na kuacha uke wako wazi na hatarini
kwa mashambuizi ya kila aina. Hakuna walinzi!!
•Mfumo wa uke usipofanya kazi vizuri ndio utaona ute mwingi kuliko
inavyotarajiwa au mkavuuuu kabisa.
•Uchafu wowote mwingine unashindwa kusafishwa naturally unalundikana
matokeo yake ofcousre infections na harufu mbaya.
•Amini usiamini ni sababu mojawapo inayoleteleza saratani ya shingo
ya uzazi.
•Mashambulizi mengine yanasaabisha utasa (infertility)
•Ute unakauka, na pale unapouhitaji (tenda la ndoa) hautakuwepo na
kusababisha michubuko ambayo inaongeza fursa za maambukizi ya magonjwa
ya ngono.

He? Sasa tusafishe vipi uke kuhakikisha una afya njema?
•Safisha nje tu kila siku unapooga au unapojisikia kwa maji safi na
mikono misafi. Nje ya uke kunahusisha mashavu na katikati yake.
•Waweza kutumia sabuni isiyokua na kemikali kali, japo haishauriwi pia
but Hakikisha sabuni haipenyi ndani kabisa

Yap that's it, no more!! Wewe safisha nje, ndani kutajisort kwenyewe.

Kwa ujumla tutahakikisha vipi afya njema ya uke? Ukiacha kusafisha? –
Hii ni topic nyingine kubwa na ndefu na yenye mijadala kibao.
Wataalamu naona wanaintervene.

 
Je! na sisi tunaopenda kuzamisha vidole huko tuwapo na madem zetu tunaweza kusababisha magonjwa?
 
"Uke wenye afya una harufu, ambayo ni nzuri, murua na isiyokera"eh ,haya ngoja niwaachie wenyewe,ila kusoma nadhani nnaruhusiwa!
 
tatizo wanawake wengi siku izi wanaona fasheni kujisafisha kwa style ya kuingiza vidole, na hata ukimwambia mtu kuwa kufanya hivyo sio afya, anapinga na kukuona kana kwamba wewe mchafu.kuna changamoto kubwa sana katika hiyo sekta ya usafi wa kwa bibi
 
Somo zur hata wanaume wanalihtaj. Sasa inakuwa vipi mwanaume akizamisha midole yake?
 
Mhhhhh! Sidhani kama hii kauli ina ukweli

•Uke ni sehemu chafu chafu chafu sana tena yenye wadudu wa kutosha
yenye kunahitaji kusafishwa kila siku

Niliwahi kusoma sehemu mbali mbali kama kinywa ni kichafu kuliko nanihii, Mkuu MziziMkavu hebu njoo hapa utoe somo kuhusu hii kauli.
 
Mjadala gani?? mbona unajianika hivi? sidhani walengwa wanasoms JF
Tujaribu kuwa na busarazaliwa. That is if wewe ni mwanamke kweli
 
Mjadala gani?? mbona unajianika hivi? sidhani walengwa wanasoms JF
Tujaribu kuwa na busarazaliwa. That is if wewe ni mwanamke kweli

Nakubaliana na baadhi ya maelezo yako, lakini mbona huwa tunafundishwa kujisafisha kwa maji baridi au ya mvua (hasa yanayokaa mtungini), je kuna manufaa au hasara yoyote kwa kufanya hivyo? Na je ni kweli ukioshea maji ya ndimu kwa bibi kuna kaza msuli jambo linalomfurahisha babu?:A S cry:
 
Mjadala gani?? mbona unajianika hivi? sidhani walengwa wanasoms JF
Tujaribu kuwa na busarazaliwa. That is if wewe ni mwanamke kweli

Walengwa mbona tupo na tumelipokea somo au walengwa we unamaanisha akina nani?wenye afya hawamwitaji daktari wanaomwitaji ni walio wagonjwa.
 
Japo mimi sio mtaalamu, ila kuna ukweli fulani. Mfano, kwani jicho linaoswaga lote? Iweje hicho kingo kioshwe chote! Ndio maana baadhi ya matatizo, hususani UTI hayatokwisha.
CHANGAMOTO: kutokana na elimu potofu, hawa ndugu zetu hawako tayari kubadilika. Ikiwa msichana hajui siku zinahesabiwaje, je hatakuwa tayari kujua mambo magumu kama haya! Mtoa mada ahsante...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom