Urusi: Zuio la watu kutoka nje lapelekea jirani kuwaua wenzake 5 kwa madai kuwa walikuwa wakipiga kelele

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,509
9,296
42c85fe20c063ba732b3b5be8ee27231


Kila jambo huja na maajabu yake! Katika hali ya kushangaza, mwanaume mmoja anashikiliwa na polisi nchini Urusi kwa kosa la kuwafyatulia risasi na kuwaua watu watano kwa madai kuwa waligoma kupunguza sauti zao wakiwa karibu na nyumba yake, huku kukiwa na marufuku ya kutembea nchini humo.

Tukio hilo linadaiwa kutokea katiak Kijiji cha Yelatma katika mkoa wa Ryazan ulioko Magharibi mwa nchi hiyo. Eneo hilo liko katika marufuku ya kutoka nyumbani, wakati nchi hiyo ikiwa inapambana na kusambaa kwa virusi vipya vya corona (covid-19).

Kamati ya Upelelezi ya Urusi imeliambia Shirika la Habari la TASS kuwa Mwanaume huyo alianza kubishana na jirani zake akiwa amesimama kwenye kibaraza (balcony) ya nyumba aliyokuwa anaishi, wakati wao wakiendelea kuongea kwa sauti ya juu.

Ilieleza kuwa waliouawa ni pamoja na wanaume wanne na mwanamke mmoja. “Aliwataka vijana hao wanne na msichana mmoja ambao walikuwa wanaongea kwa sauti ya juu karibu na nyumba yake kuacha mara moja, lakini walipoendelea aliwafyatulia risasi na kuwaua wote,” ilieleza.

“Maafisa wa Polisi walifika katika eneo la tukio na kumkamata wanaume huyo mwenye umri wa miaka 32,” taarifa ya Idara ya Wizara ya Mambo ya Ndani ilikaririwa na TASS, Jumapili, Aprili 5, 2020.

============

A man in Russia has shot dead five people for talking loudly outside his house late in the evening.

Police said the shooting happened in the village of Yelatma, in the Ryazan region about 200km (124 miles) south-east of Moscow.

The area is currently under lockdown due to the coronavirus.

Investigators say the man initially complained to the group from his balcony, and an argument broke out. He then opened fire with a hunting rifle.

The four men and one woman “died of their injuries on the spot” at around 2200 on Saturday, the Investigative Committee said.

The suspect, who has not been named, was later arrested.

His apartment has been searched and the weapon seized.
 
Yote tisa kumi.naona mama umy anacheza na akili zetu.
Anatuambia wagonjwa wawili wamepona.
lakini bado idadi ya wagonjwa Tanzania inabakia bado 24..
Ina maana wagonjwa walikuwa zaidi ya 24?..

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
mi nachojua #covid19 haiwezi kuua watu wote nchi ikabaki empty kabisa ila ni uoga wa raia tu.

waachie waendelee na mishe kama kawaida wa kufa wafe wa kubaki wabaki Mungu ndiye ataamua
 
URUSI: ZUIO LA WATU KUTOKA NJE LAPELEKEA JIRANI KUUA WENZAKE KWA MADAI YA KUPIGA KELELE

> Mwanaume mmoja (32) anashikiliwa na Polisi kwa kuwafyatulia risasi na kuwaua Wanaume wanne na Mwanamke mmoja kwa madai kuwa waligoma kupunguza sauti zao wakiwa karibu na nyumba yake

Kiukweli naongezea nyama hapa watu wanaboa sana,kipindi nikiwa kwenye nyumba za pango kila baada ya siku nne nameza dawa za kichwa tena usiombe ukute pana wanafunzi wa Chuo wamepanga Utajuta!

Na hate kelele sana,ila pole kwa waathirika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa huyo jamaa angekuwa Bongo na nyumba zetu za kupanga,nyumba moja vyumba kumi na sita.si angeua watu 40 kwa makelele.!
 
HApo ukute kesi Hana mbele kuna utaratibu wa matumizi ya vifaa vinavyo Leta Kelele😁😀
 
Back
Top Bottom