Sexer
JF-Expert Member
- Oct 22, 2014
- 8,216
- 7,911
Urusi imesema leo kwamba inashughulika kupata msaada kutoka Marekani baada ya nchi hiyo kuripoti kupungua kwa kiwango cha visa vya maambukizi ya virusi vya corona kwa usiku mmoja hali ambayo haijawahi kutokea tangu Mei 1.
Hata hivyo, nchi hiyo ambayo idadi yake jumla ya walioambukizwa ni 290,678 ni ya pili kati ya nchi zenye maambukizi mengi zaidi baada ya Marekani imesema hali bado ni ngumu baada ya maafisa kuripoti visa vipya, 8,926 vya maambukizi.
Naibu waziri wa mambo ya nje, Sergei Ryabkov amesema Urusi inashughulikia suala la kupata msaada wa tiba kutoka Marekani ili kusaidia kukabiliana na kirusi hicho.
Jana iliripotiwa kwamba waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo alisema nchi yake itapeleka vifaa kadhaa vya upimaji na mashine za kusaidia upumuaji kuisadia nchi hiyo kuudhibiti mgogoro huo na kwamba vifaa hivyo tayari viko njiani.