Urasimu wa TRA katika utoaji wa leseni za udereva na kisingizio cha 'Materials zimeisha'

Wadau,
Naandika haya kutokana na kutoelewa kinachoendelea kwa baadhi ya maeneo ambapo zoezi la ku renew leseni za udereva hua linafanyika pale inapohitajika.Imefika wakati unaaambiwa usubiri mpaka miezi 4 ndio leseni yako iwe printed.

Hii imenikuta Dodoma na pia mikoa ya kusini...baada ya kuuliza wahusika wanasema mashine zinasumbua.

Ushauri:

Kama mashine zimechoka ni vema mkafanyia matengenezo makubwa..ingawa mnabana cost ili kupata faida ila haileti maana printing tu ya leseni ichukue miezi kadhaa...
 
Tanzania ni ile ile... peleka na gari yajo ikakaguliwe, sio na TOYOTA, DT Dobie au fundi wako bali watoza faini!
 
hizi leseni ni wajibu wa serikali za mitaa,wapewe jukumu hili,TRA NI TAASISI kubwa ijikite zaidi katika kuthibiti vyanzo vikuu vya mapato vya nchi,mfano jee TRA inawajua watanzania wenye offshore accounts ambao hawalipi kodi pamoja na kujiingizia mapato makubwa?ni aibu kwangu kuona TRA inakimbizana na kodi za leseni ambazo local gorvt.ingekuwa ni wajibu wao ikiwa ni pamoja na usajili wa magari kwenye maeneo yao,means gari za mtwara zingekuwa na namba tofauti na za pale kagera,na hili lingesaidia utambuaji wa magari haya kuliko sasa nchi nzima ina mfumo mmoja na wala huwezi kutambua kuwa hii gari imeandikishwa pale Lingusenguse au kibosho
 
Bora umesema maana mimi nimerenew june mpaka sasa wanasema eti njoo mwezi ujao lakini kuna mtu amerenew august ndani ya wiki leseni ikawa imetoka, hapo ndo nachoka kabisa kwamba kuna nn?
 
Bora umesema maana mimi nimerenew june mpaka sasa wanasema eti njoo mwezi ujao lakini kuna mtu amerenew august ndani ya wiki leseni ikawa imetoka, hapo ndo nachoka kabisa kwamba kuna nn?

Upo mkoa gani kaka.
 
ili mimi limenikuta... TRA ni wababaishaji.

kazi ya kutengeneza kitambulisho kimoja cha leseni ya udereva haizidi hata dakika kumi.... hapo awali ilikuwa wiki moja tu mtu unapata leseni yako lakini siku hizi ni zaidi ya miezi 2 ndio unapata leseni...

nchi badala iendelee, kwa hili nchi inarudi nyuma kimaendeleo...
 
Dah the same to me nilienda renew tokea mwezi wa nane hadi leo bado

ukiipata leseni yako naomba unijulishe labda materials yatakuwa tayari yameshafika nnchini... inawezekana hayo materials yanakuja kwa meli...

taarifa zisizo rasmi hiyo meli iliyobeba materials imetekwa na alshabab nnchi somalia.... tuvute subira hadi iachiwe...
 
Poleni Sana japokuwa sioni umuhimu wa kulalamika kucheleweshewa kupewa leseni kwani hizo za zamani si mnazo tumieni hizo hizo muhimu uwe na Ile receipt ya tra ya kulipia leseni mpya. Trafki akikuomba leseni mpe Ile ya zamani pamoja na receipt ya tra basi ataelewa kuwa leseni yako ipo katika process. Acheni kulalamikia vitu vya kijinga
 
Kwani mkuu unapo-renew huwa hawachukui ile ya zamani kiongozi...?
 
hili ni tatizo au janga la kimyakimya alaf TRA wapo kimya pasipo kulitolea maelezo...
 
Back
Top Bottom